Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,369
- 17,935
Kwako Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa CHADEMA
Ni wazi CDM mnapoteza focus maana Kama alivyosema E Lowassa mwaka 2015 kuwa Chama chenu ni wana harakati zaidi kuliko wanasiasa. Wanaharakati huenda na matukio wakati wanasiasa huenda na mikakati.
Kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ambayo yamefanywa ndani ya kipindi cha miezi 3 au siku 100 katika utawala wa Rais SSH. Watanzania wote wanajuwa na wanaona nafuu ya maisha katika nyanja zote na wana matumaini na Rais. Sina haja ya kuyataja hapa ambayo Rais SSH amefanya kwa kuwa mengine hata Mbowe binafsi ni mnufaika wa moja kwa moja.
Sijapendezewa na Uongozi wenu wa juu wa CDM namna mnavyotaka KIUMSHURUTISHA Rais afuate VIPUMBELE vyenu badala ya vipaumbele vyake na Chama chake.
Hata kama kuna mapungufu katika vipaumbele vya Rais, naamini kuna namna ya kufikisha ujumbe kwa Rais kwa maadili na nidhamu. Kumbukeni Rais ni Taaaisi
Najuwa CHADEMA mumeomba kukutana na Rais, na Rais bado hajaonyesha atakutana nanyi lini. Hili nalo linakuwa shida kwa kuwa nyinyi akina Mbowe mnaona alipaswa aonane na CHADEMA kwanza kabla ya makundi mengine ambayo Rais amekutana nayo.
Juzi mwanachama wenu mmoja (MDUDE) ameachiwa na Mahakama ya Mbeya kwa makosa ya kusafirisha cocaine. Badala mumuache kwanza apumzike ili aboreshe saikolojia na afya ya akili, nyie mumemempandisha kwenye majukwaa na ameanza kumtishia Rais SSH.
Jana mkutano wa dinner wa akina Mama wa BAWACHA uliopangwa kufanyika pale Hekima Garden ulivunjwa na Jeshi la Polisi. Naomba mjue kuwa Serikali ipo, na hai hezewi.
USHAURI WANGU:
CHADEMA wakumbuke kuwa Rais SSH siyo Kiongozi wa CCM na CHADEMA pekee bali ni Kiongozi wa Watanzania wote walio kwenye vyama na wasio na vyama. Kazi ya Samia tumeiona kwa muda mfupi na tuna matumaini kuwa yuko kwenye MSTARI SAHIHI na kuna makubwa nchi yetu itapata chini ya Uongozi wake.
Ametupa Uhuru wa kuongea na kushauri kwa mujibu wa Katiba, tuutumie vizuri kwa masilahi mapana na nchi yetu.
Katiba Nzuri kweli tunaitaka na Rais SSH kasema tumpe muda kwanza aratibu mipango yake ya uchumi, then suala la Katiba litakuja. Kwa nini tusimpe benefit of doubt Rais wetu kwa hilo? Maana mtangulizi wake (Magufuli) alisema "Kwenye Kampeni zangu sikuahidi Katiba". Ila huyu Samia anasema tumpe muda tu, nyinyi hamutaki.
Na kwa miaka 5 CHADEMA walikuwa wanaongelea Tume Huru Ya Uchaguzi, kuibiwa kura za uchaguzi na kesi za kubambikizwa. Sasa ndiyo wameanza kudai Katiba naada ya DIKTETA Magufuli kufariki.
Nawashauri CHADEMA, waitishe Mkutano wao Mkuu ili waweke mkakati wa nini wanachokitaka na siyo kila mwenye kusimama jukwaani anataka cha kwake. Wawatumie vijana wao wasomi waandike dira yao na miongozo ya vitu gani wadai kutoka Seikalini.