Baraza la Iddi: Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu wenyewe - Kikwete

Binafsi nimeiona hotuba kuwa ya kawaida sana, labda inatokana na hotuba hiyo kutokidhi matarajio yangu kwani pamoja na kwamba jukwaa lilikuwa ni la kidini zaidi lakini mimi nili husisha na ule utaratibu wa rais kuhutubia taifa mwisho wa mwezi japo hatujamskia kwa miezi kadhaa. Despite of mambo mengi yaliyotokea katikati na ambayo bila shaka watz wenzangu wangependa kuskia rais wao anasemaje leo nilitega sikio kuona kama rais angeua ndege wawil kwa jiwe moja yaani kujibu risala ya walio mualika lakini pia kikidhi haja ya wale pia wasioweza kuandaa jukwaa na kumualika rais na hivyo kupaza sauti zao kupitia risala. Hapa raisi anapaswa kujua matatizo yanayoikabili sehemu kubwa ya raia wake kwa kipindi chote ambacho hajaweza kuwahutubia, japo hotuba yake isingekuwa dawa lakini yaweza kurudisha matumaini yaliyopotea. LABDA BASI KUNA HOTUBA YA KITAIFA ITAFUATA BAADA YA HII, KAMA HAKUNA BASI SIKUFURAHISHWA SANA NA HOTUBA YA LEO

Sio siri, JK ametugeuka, haya hayakuwa maneno yake wakati anafanya Kampeni.
JK Kigeugeu eheeee, JK kigeugeu Ehehhhee

Hakika leo JK ametoa hotuba ambayo mi binafsi imenifurahisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Ila nina wasi wasi kuwa huenda haikupokelewa vizuri na viongozi wa dini ya kiislamu kwani hawakuonyesha sura za furaha.
Pamoja na mimi kuwa CHADEMA nampongeza aliyemwandikia hotuba ya leo JK. Mimi pia nimebaini leo ameonekana "more serious" na aliweka maslahi ya nchi mbele katika kila alichokizungumzia. Nampa Big up kwa hilo. Laiti angekuwa hivi siku zote yeye na CCM yao wasingepoteza mvuto kwa kasi ya ajabu kama ilivyotokea. Yaelekea sasa amewapata washauri makini na si mavuvuzela waliompotezea dira. Kumbe sasa nimeanza kubaini tatizo si JK bali wapambe nuksi waliokuwa wakimzunguuka muda wote na yeye kuwaamini na kuchukua ushauri wao! Wanaodhani JK "anachukiwa" kutokana na yeye kuwa mwislamu ni wajinga wasioelewa kitu, ukweli ni kwamba watanzania hawamchukii JK bali jinsi anavyoliongoza taifa letu kiajali ajali. Ni aibu, tena ni fadheha kubwa kwamba serikali inayogawa mabilioni ya shilingi kila mwezi kuwalipa matapeli wa kuzalisha "Umeme" imeshindwa kabisa kununua vinu vyake vya kuzalisha nishati hiyo ambayo bei yake ni kama gharama ya kuwalipa matapeli wanaozalisha "umeme hewa" huo kwa miezi miwili au mitatu hivi. Tena ni fedheha isiyo kifani kwa nchi kuadhimisha miaka 50 ya kujitawala tukiwa giza totoro kisa? nchi imetapeliwa na vibaka uchumi waliojichimbia ndani ya chama ambacho wakati fulani kilikuwa mfano wa vyama vya kutetea wanyonge Afrika na dunia nzima!

• Thanks
Reactions: Ame
Leo kwa mara ya kwanza nimemsikiliza na kumuelewa....... Dah! amewakatisha tamaa sana akina Faiza na Malaria Sugu, kuhusu mahakama yao.... teh teh teh huyo ndiye JK mr. Kigeugeu

rudisheni basi kadi za chadema mchukue za ccm, si mlikimbia ccm kwa udini wenu kwa kuwa tu waislam watarejeshewa kadhi.

Nimefuatilia kwa karibu hotuba ya JK iliyorushwa LIVE na TBC katika baraza la Idd pale msikiti wa Gaddafi Dodoma. Nilikuwa natafuta tu channel yenye habari nzuri ila nilipofungua TBC nikamkuta Live na nikasema nisikilize angalau kwa DK 2 kwani siku nyingi nilikuwa sipotezi muda wangu kuangalia hotuba na mzee wa kaya.

Kwa mara ya kwanza tangu nianze kumsikia JK leo ameongea kwa ujasiri kama rais wa nchi kuwajibu sio waislam tu bali viongozi wengi wa dini including za Kikristo. JK ameonyesha tabia ambayo sijawahi iona tangu aingie madarakani kwa kuongea kwa ujasiri na msisitizo na serious huku akimwaangalia machoni Sheikh Mkuu kuhusu serikali kukataa kurudisha shule zilizokuwa za dini na suala la mahakama ya kadhi.

Issue hapa siyo mambo aliyoongea ila alivyoongea ameni bariki sana kwani nimejisikia nikilazimika kusikiliza hadi mwisho hotuba ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa na hadhi ya ki urais tofauti na hotuba zoote alizowahi kufanya.
Katiba hotuba hii JK hakuwa nacheka cheka kama ilivyo kawaida jambo ambalo limefanya niamini kwamba amepata mwana saikolojia wa kumpa shule ya essentials of public speech.

Issues hizi nzito ameongea kama rais bila kuzunguka, kutetereka wala kuuma maneno huku wakuu wa dini hiyo wakimwangalia kwa kutoonyesha kuridhika na wengine wakaanza kunongonezana.

Mzee wa Kaya usiishie hapo bali anza kwa usiriazi huo kupambana na mafisadi, majairo, kushughulikia umeme na masuala mengine yanayodidimiza taifa. Naamini kwa spidi hiyo hiyo mtazamo wetu kwako lazima utakuwa positive!!

haya jamani nafikiri mmeona wenyewe jinsi rais alivyojaaliwa khekima tunaomba kura zenu ili ccm iendelee kutawala 2015 ili kuimarisha misingi hiyo aliyoieleza rais kwenye baraza la idd leo mjini dodoma.
mm ninawasiwasi kama tutawapa nchi hii chadema 2015; misingi hii itavunjika na tanzania hapatakuwa tena mahali pazuri pakuishi!! ccm oyee!!!!!!!!
Tumia rangi zinazosomeka. Hayo uliyoandika rangi ya manjano nimeshindwa kusoma hata neno moja.

Kikwete kanifurahisha sana kwenye hotuba yake.

1) Mahakama ya kadhi ruksa.

2) MOU kama ya makanisa na Serikali ruksa kwa Waislaam na anawaambia mmechelewa toka 1992 mlikuwa wapi? Letenii maombi yenu na nyinyi mpewe MOU yenu.

Kanifurahisha kweli kweli. Sasa Waislaam tushindwe wenyewe tu.

• Thanks
Reactions: Ame
nafuatilia hotuba ya mh raisi kikwete kwenye baraza la iddi kuoitia tbc 1.

Kwa kweli amejitahidi kuainisha ukweli wa mambo hususan katika sekta ya elimu,

japo naona kuna ma ustaadh wanamuangalia kwa roho mbaya kweli

toe hiyo avatar tafadhali

hasa hasa anaposema baba wa taifa hili mwalimu nyerere alitaifisha

shule zote za dini na mashirika ziwe za serikali ili elimu itolewe bila ubaguzi.

Kudos j.k

n.b:

Mimi ni chadema, ila kiongozi wa ccm akisema jambo likanigusa hakika sitaacha kumfagilia.

Siasa sio uadui na kuona maovu ya mwenzako tu bila kuona mazuri wajameni.
toa hiyo avatar tafadhali

Pamoja na mimi kuwa CHADEMA nampongeza aliyemwandikia hotuba ya leo JK. Mimi pia nimebaini leo ameonekana "more serious" na aliweka maslahi ya nchi mbele katika kila alichokizungumzia. Nampa Big up kwa hilo. Laiti angekuwa hivi siku zote yeye na CCM yao wasingepoteza mvuto kwa kasi ya ajabu kama ilivyotokea. Yaelekea sasa amewapata washauri makini na si mavuvuzela waliompotezea dira. Kumbe sasa nimeanza kubaini tatizo si JK bali wapambe nuksi waliokuwa wakimzunguuka muda wote na yeye kuwaamini na kuchukua ushauri wao! Wanaodhani JK "anachukiwa" kutokana na yeye kuwa mwislamu ni wajinga wasioelewa kitu, ukweli ni kwamba watanzania hawamchukii JK bali jinsi anavyoliongoza taifa letu kiajali ajali. Ni aibu, tena ni fadheha kubwa kwamba serikali inayogawa mabilioni ya shilingi kila mwezi kuwalipa matapeli wa kuzalisha "Umeme" imeshindwa kabisa kununua vinu vyake vya kuzalisha nishati hiyo ambayo bei yake ni kama gharama ya kuwalipa matapeli wanaozalisha "umeme hewa" huo kwa miezi miwili au mitatu hivi. Tena ni fedheha isiyo kifani kwa nchi kuadhimisha miaka 50 ya kujitawala tukiwa giza totoro kisa? nchi imetapeliwa na vibaka uchumi waliojichimbia ndani ya chama ambacho wakati fulani kilikuwa mfano wa vyama vya kutetea wanyonge Afrika na dunia nzima!
Nadhani ni huyu kijana mpya aliyemchukua wizara ya mambo ya nje juzi kumwandishi spichi. Sasa tungoje matendo kwa sababu hata ukisoma hotuba yake ya kwanza bungeni ilitoa matumaini makubwa.

Nimekaa nikimsikiliza JK katika baraza la Eid. Huyu bwana hana lugha ya kidiplomasia na sijui kwa nini Mkapa alimpa uwaziri wa mambo ya nchi za nje!!! Kimsingi ananiboa sana. Ukiangalia hata sura za mashehe wetu, wanaonekana wamekata tamaa kabisa. Anyway, binafsi ninajuta kumpigia kampeni kabisa ktk uchaguzi mkuu. Sasa ninakubaliana na statement ya jamaa mmoja inayosema, IF YOU THINK GADDAFI IS BAD, TRY JK

Alikuwa sahihi na nimempenda sana mkuu wangu wa nchi. kuna maswala ya kuzunguka na mengine ya kutumia lugha rahisi ili kufanya ueleweke kwa tafsiri moja. ukitumia lugha ya diplomasia unafanya kupatikana kwa tafsiri zaidi ya moja. ni bora watu wakaelewa kama embe ni embe na si kutumia lugha ngumu. kuhusu shule za waislam kurudishwa pia amesema vizuri sana. nyingi ni za wakristu. zikirudishwa iza waislam ambazo ni chache na wakristu watake zao ambazo ni nyingi itakuwaje? he was right.

Nimefuatilia kwa karibu hotuba ya JK iliyorushwa LIVE na TBC katika baraza la Idd pale msikiti wa Gaddafi Dodoma. Nilikuwa natafuta tu channel yenye habari nzuri ila nilipofungua TBC nikamkuta Live na nikasema nisikilize angalau kwa DK 2 kwani siku nyingi nilikuwa sipotezi muda wangu kuangalia hotuba na mzee wa kaya.

Kwa mara ya kwanza tangu nianze kumsikia JK leo ameongea kwa ujasiri kama rais wa nchi kuwajibu sio waislam tu bali viongozi wengi wa dini including za Kikristo. JK ameonyesha tabia ambayo sijawahi iona tangu aingie madarakani kwa kuongea kwa ujasiri na msisitizo na serious huku akimwaangalia machoni Sheikh Mkuu kuhusu serikali kukataa kurudisha shule zilizokuwa za dini na suala la mahakama ya kadhi.

Issue hapa siyo mambo aliyoongea ila alivyoongea ameni bariki sana kwani nimejisikia nikilazimika kusikiliza hadi mwisho hotuba ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa na hadhi ya ki urais tofauti na hotuba zoote alizowahi kufanya.
Katiba hotuba hii JK hakuwa nacheka cheka kama ilivyo kawaida jambo ambalo limefanya niamini kwamba amepata mwana saikolojia wa kumpa shule ya essentials of public speech.

Issues hizi nzito ameongea kama rais bila kuzunguka, kutetereka wala kuuma maneno huku wakuu wa dini hiyo wakimwangalia kwa kutoonyesha kuridhika na wengine wakaanza kunongonezana.

Mzee wa Kaya usiishie hapo bali anza kwa usiriazi huo kupambana na mafisadi, majairo, kushughulikia umeme na masuala mengine yanayodidimiza taifa. Naamini kwa spidi hiyo hiyo mtazamo wetu kwako lazima utakuwa positive!!

Huitaji kujua yaliyomo ndani moyo wa mtu hadi uangalie matendo yake. Siku zote JK mlikuwa mnamuona rais legelege leo hii kwavile kawaumiza waislamu yaliyo moyoni mwao unasema ndio rahisi amekamilika kweli wajinga ndio waliwao. Let me see hii movie itaisha wapi kwani wakati wewe unafurahia ujue mwengine anaumia halafu unasema Tanzania kisiwa cha amani . St Augustine aliwahi kusema an unjust law or society is similar to no law or society of lawlessness wait and see.

Amefanya vyema. Kwa vizazi vipya msiwe na hofu wala shaka kihusu mahakama hii ya kadhi kwani ilikuwepo wakati tunapata uhuru na iliendelea mpaka mwaka 1963 ilipopigwa marufuku.

Mahakama ya kadhi haikuwahi kuwapo tanganyika tangu enzi zile unazosema. kulikuwa hakuna kadhi bali kulikuwa na liwali. jk.

Bila shaka sasa upo tayari kumpa kura yako 2015

Anavuta shuka kukiwa kumepambazuka....I listened to part of it...what irks me in his 'hotuba's' ni kuadress watu kama watoto wadogo, trying to be a mr goody goody and Only serious akiongea kwa lugha ya kiingereza...'Tumewakamata wakiwa wanaenda hapo Brazil...tume bla bla... No offence but his speech delivery is always softened and miss that EDGE you wish leaders should have...and what IRKS the most, that style is consistent when he has to address Tanzanians

Back
Top Bottom