Baraza la Iddi: Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu wenyewe - Kikwete

binafsi nimeiona hotuba kuwa ya kawaida sana, labda inatokana na hotuba hiyo kutokidhi matarajio yangu kwani pamoja na kwamba jukwaa lilikuwa ni la kidini zaidi lakini mimi nili husisha na ule utaratibu wa rais kuhutubia taifa mwisho wa mwezi japo hatujamskia kwa miezi kadhaa. Despite of mambo mengi yaliyotokea katikati na ambayo bila shaka watz wenzangu wangependa kuskia rais wao anasemaje leo nilitega sikio kuona kama rais angeua ndege wawil kwa jiwe moja yaani kujibu risala ya walio mualika lakini pia kikidhi haja ya wale pia wasioweza kuandaa jukwaa na kumualika rais na hivyo kupaza sauti zao kupitia risala. Hapa raisi anapaswa kujua matatizo yanayoikabili sehemu kubwa ya raia wake kwa kipindi chote ambacho hajaweza kuwahutubia, japo hotuba yake isingekuwa dawa lakini yaweza kurudisha matumaini yaliyopotea. Labda basi kuna hotuba ya kitaifa itafuata baada ya hii, kama hakuna basi sikufurahishwa sana na hotuba ya leo
pale ameenda kuhutubia baraza la iddi lakini pia kwa kutumia hadhira ile ilitaka taifa lipate ujumbe kwani mambo aliyoyazungumza pale ndio misingi ya amani tuliyonayo! Jaribu kusifia mtu akifanya vizuri hata kama humpendi

we ulitegemea awajibu nini? Maana hawa Waislamu wamezoe kulalamika wanatengwa na Serikali inapendelea wakristo kitu ambacho sio kweli...
Wanapata misaada mingi tu matokeo yake wanaishia kujenga misikiti tu bila kuangalia katika sekta za kijamaa kama Hospitali, Shule, maji nk
alichosema na kuwajibu hao waislamu ni stahili yao, naa,ini wataanza kuamka toka usingizini

Afanye matendo kuthibitisha maneno yake yana ukweli wowote au la! Vinginevyo JF ina hotuba nzuri kuliko hizi hotuba zinazotuchosha kila siku

Mtoa thread hii nakuomba ukome kuweka conclusion kwamba '...........mtazamo wetu utakuwa positive...." Kama ni mtazamo wako usiandike wetu tafadhali. Tena umeniharibia sana Eid yangu kwa leo.

Pole mi siyo Magamba ila siyo extremist na niko tayari kum judge mtu otherwise kama ameonyesha kujua makosa yake akatubu na kuanza kuishi na kufanya mambo kwa mustakabali wa jamii husika

Pole mi siyo Magamba ila siyo extremist na niko tayari kum judge mtu otherwise kama ameonyesha kujua makosa yake akatubu na kuanza kuishi na kufanya mambo kwa mustakabali wa jamii husika

Unakataa we siyo magamba?

Tafsiri rahisi ni kwamba upo tayari kumpa kura mgombea wa CCM ilimradi asiwe Kikwete

Sitaipigia CCM kura kwa kauli ya siku moja mkuu na wala hii hotuba haibadilishi msimamo wangu kuhusu nitakayempa kura kwani tunahitaji mabadiliko mkuu hii rangi ya Kijani na ile mishati ya Kijani as a matter of fact inanitia kichefu chefu sana inatakiwa rangi nyingine

Sio siri, JK ametugeuka, haya hayakuwa maneno yake wakati anafanya Kampeni.

JK Kigeugeu eheeee, JK kigeugeu Ehehhhee

mumthamini nani? Mmwamini nani? Anawageukia! Kigeugeu! Eeeeee! Kigeugeu. Anawageukia!

Baada ya hotuba hii ambayo wengi imewafurahisha,
inabidi aendelee kuwafurahisha raia wake vivi hivi hata ktk mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa muda mrefu na yeye kama Rais amekaa kimya, otherwise hotuba ni ya kawaida na ya kisiasa tu

Waislam wakirudishiwa shule zao, si wataongeza Nchi kushuka kwa elimu, maana hadi sasa zote wanazoziongoza zinashika mkia matokeo za sekondari. Mi naona waendelee kutumia hizi za kwetu kama pugu, kibaha, ilboru na mengine ili walau wapande kidogo kielimu. Baada ya miaka 50 tena wajipange upya.

Gadafi amekuwa akitoa misaada mingi Afrika na Tz ,ila sijawahi sikia amesaidia kujenga shule au chuo,kwanini Bakwata hakumshawishi Gadafi awajeenge shule kuliko kudai shule ambazo kiuhalisia ni chache sana..!

Baada ya mpango kujenga misikiti kufanikiwa wangemshawishi Gadafi ajenge shule ili kusaidia kupunguza umaskini wa elimu?

Binafsi sikupenda niliposikia JK atahutubia taifa kutoka msikitini. Anyway leaving that behind, hii hotuba imekuwa muhimu sana. Kulikuwa na "leadership vacuum" kwenye haya mambo yanayohusu serikali na dini, hasa Kadhi, MoU etc. Nafurahi ameyasemea kwa vizuri sana. At last kina FaizaFoxy et al, watatulia.

Anawajua vizuri ila alikua anasubiri wampe kura za utawala wa kipindi cha pili ndo awaambie ukweli.
Thats why I hate siasa!

Mdondoaji kipi kimefanywa kwa upendeleo hapo mbona zote alizoongea ni point ziko wazi. Kwa mfano hivi leo serikali ikiamua kurudisha shule za mashirika na taasisi mbali mbali ili ziongozwe kwa utaratibu wa taasisi hizo we unafikiri dini nyingine zitasomesha wanafunzi wapi kama si shule za kata. Wewe umesikia walionyanganywa shule nyingi ni waksristo na hawajawahi omba warudishiwe ila waliokuwa na shule kiduchu ndo wanasema warudishiwe. Mkuu huoni hapa rais amekuwa na huruma tu na akatumia busara kuwaeleza kuwa madai yao yakitekelezwa itakula kwao.

On a positive note kuhusu swala la shule kurejeshwa kwa wahusika siliafiki kwani mimi ni liberalist (yaani naamini uhuru wa mtu) sidhani kama ni sahihi kurudisha shule kwa viongozi wa dini halafu ziendeshwe kidini kwani utawanyima haki watoto wengine wasioko katika dini husika. Kwa mfano wahindu na wapagani nao wakoseme wapi zikirudishwa shule kwa taasisi za kidini?

On a negative side nasubiria nisome kwa ufasaha speech yake kuhusu suala la mahakama ya kadhi kwani halieleweki anapopakusudia ni wapi. Kikubwa naweza kusema anasupport kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ila je ni mahakama ipi anayoitaka yeye nasubiria speech yake niisome kama unayo tunaomba utuwekee. Ila nimeongea na baadhi ya viongozi wa waislamu hapo mjini kwakweli hawakufurahishwa na tamko hilo sasa sijui kama hawakufurahishwa kweli au ushabiki we will see ila nawasiwasi CCM inaelekea kufa kabisa kwani ngome yake kuu ni kwa waislamu kupitia bakwata na wakiipoteza hiyo I guarantee CCM inaanguka kwa kupoteza kura maeneo yote ya pwani, kusini na katikati na magharibi mikoa ya Tabora, shinyanga na Kagera na Kigoma. Sasa ukiangalia na nguvu ya Chadema kaskazini CCM 2015 inaanguka sijui wacha nisubiri statement yake in writing .

Kikwete kanifurahisha sana kwenye hotuba yake.

1) Mahakama ya kadhi ruksa.

2) MOU kama ya makanisa na Serikali ruksa kwa Waislaam na anawaambia mmechelewa toka 1992 mlikuwa wapi? Letenii maombi yenu na nyinyi mpewe MOU yenu.

Kanifurahisha kweli kweli. Sasa Waislaam tushindwe wenyewe tu.
JK Kama Kinyonga vile, Waislam tunaloooh, TunajuUUUUTA kumualika leo

Nduguzangu waislamu shule mlizonazo ndo zinashikaga mkia kwenye matokeo kwanini mlizonazo msizinyanyue kwanza kielimu ?

Back
Top Bottom