Maamuzi ya Waislamu Juu ya Mahakama ya Kadhi leo, Baraza la Iddi Msikiti wa Kichangani, Magomeni.

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Maada kuu katika Baraza la Iddi litakalo fanyika Leo Katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa zitakua zifuatazo.

1. Msimamo wa Waislamu Juu ya Rasimu ya Katiba iliodharau Maoni ya Waislamu.

2. Msimamo wa Waislamu juu ya Kulawitiwa kwa Masheikh wakiwa Mahabusu katika nchi ya Tanganyika kwa kutuhumiwa tu Ugaidi.

3. Mengineyo.

Hakuna siri, Mambo hadharani, nyote karibuni.
 
BISMILLAH RAHMAN RAHEEM

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Kwa Nini Waislamu Wamegawanyika Katika Makundi Tofauti Ya kuelewa Dini Yao

Wakati Waislamu wote wanamfuata Mtume mmoja na Qur-aan moja lakini kuna makundi mengi na tofauti yaliyogawanyika miongoni mwa Waislamu?


1. WAISLAMU NI LAZIMA WAUNGANE

Ukweli ni kwamba Waislamu wa zama hizi, wamegawanyika mapote tofauti. Kugawanyika huko hakuungwi mkono na Uislamu kabisa. Uislamu unaamini ya kwamba wauumini ni lazima waungane.
Kwani Qur-aan Tukufu inasema:
"Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyokuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye Akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema Yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto, Naye Akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu Anakubainishia ishara Zake ili mpate kuongoka".
Qur-aan inasema pia:
"Enyi mlioamini! mtiini Mwenyezi Mungu na mtíini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndio bora zaidi na ndio yenye mwisho mwema."
Waislamu wote ni lazima kushikamana na Kitabu na Sunnah sahihi na sio kugawanyika makundi makundi.


2. IMEKATAZWA KUGAWANYIKA NA KUFANYA MAKUNDI

Mwenyezi Mungu Anasema ndani ya Qur-aan:

"Hakika walio igawa dini yao wakawa makundi makundi, huna uhusiano nao wowote. Bila ya shaka shauri yao iko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda". [6:159]

Kwenye Aayah hii Mwenyezi Mungu Anasema ya kwamba yeyote yule asishirikiane na yule aliyeigawa dini yake katika makundi.
Lakini mtu akimuuliza Muislamu, ‘Wewe ni kundi gani?', jibu litakuwa ‘Mimi ni Sunni', au ‘Mie ni Ibadhi'. Na katika Masuni wengine hujiita Hanafi au Ash-Shaafi'iy au Maalik au Hanbaliy. Na humo tena utakuta mtu anajiita ‘Mimi Qadiriya', ‘Mimi Naqshabandiya' au ‘Mimi Shadhiliya'!


3. MTUME (SWALLA ALLAAHU ‘ALAYHI WA SALLAM) ALIKUA MUISLAMU

Anaweza kuulizwa Muislamu, "kipenzi chetu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa nani? Alikuwa Ibadhi, Hanafi, au Ash-Shaafi'iy, au Hanbali au Maaliki? Jibu litakuwa hapana alikuwa Muislamu kama vile Manabii na Mitume ya Allaah (Subhaanahu wa Taa'ala) kabla yake.
Imesemwa kwenye sura ya 3 Aayah ya 52 ya kwamba ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) alikuwa ni Muislamu.
Hata ukiangalia,kwenye sura ya 3 Aayah ya 67 ndani ya Qur-aan ya kwamba Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) hakuwa Myahudi wala Mnaswara lakini alikuwa Muislamu.

4. QUR-AAN INATUAMRISHA TUJIITE WAISLAMU

Asiyekuwa Muislamu akimuuliza Muislamu wewe ni nani, bila ya shaka atasema 'mimi ni MUISLAMU", sio Hanafi au Ash-Shaafi'iy...

Jawabu hili linapatikana ndani ya Qur-aan katika Surah Fusswilat 41 Aayah ya 33 ambayo inasema:
"Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu"?

Qur-aan inasema:
"Hakika mimi ni katika Waislamu".Kwa maana nyengine inasema "mimi ni Muislamu".

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliandika barua kwa mfalme na mtawala ambaye alikuwa si Muislamu kumtaka awe Muislamu. Kwenye barua hiyo kulikuwemo na Aayah ya Qur-aan iliyoko katika Surah ya 3 Aal-‘Iimraan Aayah ya 64 isemayo:
"Shuhudieni ya kwamba mimi ni Muislamu"

HITIMISHO
Waislam fahamuni ya kuwa madhila, misiba , majanga yanayowakuta waislam inatokana na sisi waislamu wenyewe baada ya kukengeuka na Quraan na sunnah za mtume ( swallallahu alayh wassallam) tumekuwa watu wa kupingana sisi kwa sisi jambo hili ndo sababu ya mgawanyiko kwa waislamu ndo maana tunakosa nguvu ya pamoja dhid ya maadui wa uislam tambua ewe muislam Ummah hautaepukana na hali hii ya uzalilishwaji wa waislamu mpaka waislam watapo fungamana na Quraan na sunnah kwa ufahamu uleule wa maswahaba RIDHWANILLAH TAALA ANHUM
 
Nipeni maazimio ya baraza,maana quran imatutaka kuwaheshimu viongoz wetu,msimamo mmoja
 
Hili baraza la Idd lina kazi kubwa yaani linajadili hata tuhuma za kulawitiwa jamaa wa uamusho sasa ushahidi watautoa wapi au watamwamini tu aliyelawitiwa????
 
Updates plz>

Mkuu Udates ni kama zifuatazo.

1.Shura ya Maimamu wa Misikiti yote Tanzania, Imetangaza Kura ya Hapana kwa Rasimu ya CCM, kutokana na Maoni ya Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi kudharauliwa. Mtoa Mada amedokezea kua Mwendo ni Ule ule Wa SENSA.

2. Maandamano ya Nchi nzima kufuatia Soon. Sio kwa Staili ya Kuomba kibali. Ulimwengu Mzima, Maandamano ya Kweli hua hayaombewi kibali wala njia ya Kupita. Staili ni ile ile ya SENSA.

3. Masheikh hawajafanyiwa vitendo vya kulawitiwa Magereza, bali wamefanyiwa vitendo hivyo wakiwa Mikononi mwa jeshi la polisi na vyombo vinginevyo vya Usalama. Miongoni mwa Udhalilishaji ni kitendo cha Sheikh Muslem mfasiri Mahiri wa Qur-an kuhojiwa akiwa Uchi. Nini cha kufanya katika hilo. Hilo suala limerudishwa Mikononi mwa Waislamu wenyewe kila mtu kwa nafasi yake.
 
Back
Top Bottom