Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Katiba inayopendekezwa na Mahakama ya Kadhi

Standalone

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
676
576
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.

Vidokezo:
1. Kwa dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuihusisha serikali wala waumini wa dini nyingine.


2. Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu; na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe. Aidha, Katiba Inayopendekezwa haijajibu bado matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali (Muundo wa serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya Rais, uwiano wa mihimili ya dola n.k).
"Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu," linasema tamko hilo.

jukwaa-la-wakristo2-1024x556.jpg

Kwa tamko lote tafadhali gonga kiambatanisho chini.

======================



attachment.php

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA, MAHAKAMA YA KADHI NA HALI YA USALAMA NA AMANI YA NCHI.

Sisi Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo Tanzania linaloundwa na Taasisi za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) tuliokutana leo tarehe 10.03.2015, tumepata nafasi y a kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.

Baada ya kutafakari yote hayo, Jukwaa limefikia maazimio yafuatayo:

Kuhusu uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi: Suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka mi singi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini. Pia mjadala unaoendelea unavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Ibara ya 19.

Kwa kuendelea kujadili suala hili katika Il ani za Vyama vya Siasa, Majukwaa ya Kisiasa na Bungeni, limeligawa Taifa letu, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi. Mahakama ya Kadhi imekuwa likiendelea kutumiwa na wanasiasa kama mtaji wao wa kujipatia madaraka kwa gharama za kuleta chuki za kidini.

Kw a dhamiri safi, Jukwaa linatamka wazi kuwa mjadala unaoendelea kati ya Serikali na vikundi vya kidini kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kikatiba na kisheria ufungwe na badala yake ziachiwe taasisi husika za kidini kuamua juu ya masuala hayo bila kuih usisha serikali wala waumini wa dini nyingine.

Kuhusu Katiba inayopendekezwa: Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu; na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe. dha, Katiba In ayopendekezwa haijajibu bado matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali (Muundo wa serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya Rais, uwiano wa mihimili ya dola n.k). Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipit ishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi.

Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake!!! Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezw aHivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wing i kupiga kura ya HAPANA kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu.

Hali ya usalama wa nchi ulivyo sasa: Jukwaa linasikitishwa na viashiria pevu vya ugaidi vilivyoanza kujitokeza nchini kwa takribani miaka mitano iliyopita. Kumekuwa na vitendo vinavyoashiria kuchipuka kwa ugaidi kama vile uvamizi wa vituo vya polisi, kuporwa silaha na mauaji ya polisi, mafunzo ya kareti katika nyumba za Ibada, mafunzo ya itikadi kali za kidini kwa watoto (Kilimanjaro), tukio la Amboni Tanga, mauaji ya v iongozi wa dini (Buselesele, Zanzibar, Arusha), uchomaji wa nyumba za Ibada na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini.

Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino): Jukwaa linasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (m aalbino) na ukatili unaosababisha ulemavu wa kudumu wa maalbino katika nchi yetu. Hali hii inatishia utulivu, amani na umoja wa kitaifa tuliokuwa nao kama taifa la mfano barani Afrika. Jukwaa linawaasa wananchi kuacha tabia hii ya kuua albino. Jukwaa linaa mini kuwa kukosekana kwa uwajibikaji wa viongozi wa serikali na kuongezeka kwa wigo wa kipato kati ya walionacho na wasionacho kunachangia ongezeko la vitendo hivyo viovu. Jukwaa linajiuliza: mbona tembo na ng'ombe wakiuawa operesheni maalum zinafanyika na viongozi wanawajibika, kwa nini maalbino wakiuawa viongozi hawawajibiki?

Kutokana na hayo yote, Jukwaa linatilia shaka dhamira thabiti ya uongozi wa Chama Tawala na Serikali yake katika kuvitokomeza vitendo vya kigaidi, mauaji ya albino na uvunjifu wa am ani unaoendelea hasa kutokana mikakati hafifu na udhaifu mkubwa uliojitokeza wakati wa kuyashughulikia masuala hayo. Kwa kuwa Chama Tawala na Serikali wameshindwa kusimamia misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani; umoja na utulivu; Jukwaa linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza Taifa badala ya kutanguliza mazoea, mapokeo, itikadi na usha biki wa chama fulani cha Siasa.

YATOSHA KWA SIKU MAOVU YAKE: MATHA YO 6:34

Imetolewa na:
attachment.php




SIO WAISLAMU WOTE WANATAKA MAHAKAMA YA KADHI, NIMEIKUTA HII BARUA SEHEMU WALAU KUBALANSI STORY
KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.
1.Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.
2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.
3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.
4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?
5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.
6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!
7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.
8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.


KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.
10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.
11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.
12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani
ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!
WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.
14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:
(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.
(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu
ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!
16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.
WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.

TAMKO LA MAASKOFU LAENDELEA KUUNGWA MKONO

CHAMA CHA WALIMU WAUNGANA NA MAASKOFU WAIZIKA RASMI KATIBA PENDEKEZWA YA KIKWETE


Gratian-Mukoba1.jpg

CHAMA cha walimu nchini (CWT)kimewakata Walimu wote nchi kuipigia kura ya Hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la Katiba kwa madai katiba hiyo imeshindwa kuonesha njia ya kutatua matatizo ya walimu nchini ambayo yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.Anaaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo.

Kuibuka huko kwa (CWT) kunakuja siku chache kupita baada Mwamvuli wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, ambalo ni jumuiko la pamoja la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT

Kuandaa Tamko la ambalo limesomwa jana kila kanisa nchini kwa kuwataka waamini wa dini ya Kikristo kuipigia kura ya hapana Katiba pendekezwa, pindi itakapofika kwao,wakidai katiba hiyo pendekezwa imekuwa na gilba nyingi sana katika kutengenezwa kwake.

Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT) Gration Mukoba mda huu jijini Dar es Salaam,amesema chama hicho kimeshatoa maagizo kwa viongozi wa chama hicho ngazi ya Mkoa na wilaya kuwahamasisha waalimu kuipigia kura ya hapana Katiba inayopendekezwa na Bunge la Maalum Katiba.

"Sisi walimu tumeshasema tangu mwanzo hatuitaki hii katiba,maana imeshindwa kuweka misingi ya kumsaidia mwalimu ambaye amekuwa anakumbana na matatizo mengi ikiwemo malipo duni na kutokuwa na vitendea kazi"amesema Mukoba.

Mukoba ameongeza kuwa mwalimu makini hawezi akawa katika upande wa kuiipitisha katiba ambayo anadai itakuwa kaburi kwa walimu na watanzania kwa ujumla.

Aidha, Mukoba ameonyesha masikitiko yake kwa Kauli aliyoitoa jana AskofuMkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama PolycarpKardinali Pengo ya kuupinga tamko hilo la Jumuiya ya Kikiristo ambapo Askofu Pengo anasema Tamko hilo limekosa utashi wa kiroho.

Akizungumzia Kauli hiyo Rais huyo CWT amesema ni wazi kiongozi huyo wa Dini anaitetea Serikali ambayo anasema imeshachoka na inahitaji mapinduzi ya Fikra.

*******Muendelezo Wa Habari*******
TAMKO LA TAASISI YA MASHEIKH NA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA KUFUATIA KAULI YA MAASKOFU KUINGILIA MADARAKA YA BUNGE NA KULITAKA LISIJADILI JUU YA MAHAKAMA YA KADHI


1. Hivi karibuni ndugu zetu, viongozi wenzetu wa Dini ya Kikristo chini ya "mwamvuli" wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, wametoa Tamko la kuitaka Serikali isitishe Mchakato wa Mahakama ya Kadhi kwa kuondoa muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02 wa Mwaka 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislamu, Sura ya 375(The Islamic Law(Restatement) Act, Cap.375) na ambao unatarajiwa kujadiliwa katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea hivi sasa Dodoma, ikiwa ni ahadi ya Serikali iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda mwishoni mwa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba.

2. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imelipitia Tamko hilo la Jukwaa la Wakristo Tanzania kwa umakini mkubwa na baada ya tafakuri ya kina juu ya kadhia hii, Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inaweka bayana yafuatayo:-

3. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imesikitishwa sana na Tamko la Maaskofu chini ya Jukwaa la Wakristo Tanzania kuingilia kwa hila madaraka ya Bunge na kutaka kuifanya Serikali iliyotoa ahadi kupitia Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ionekane imewadanganya Waislamu ili Waislamu waichukie Serikali yao. Ikumbukwe kwamba Ahadi ya Marekebisho ya Sheria kuitambua Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara ni Ahadi ya Serikali.

4. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inawanasihi na kuwaomba Maaskofu wawaachie "uhuru" Wabunge Waumini wa Dini ya Kikristo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waujadili muswada huo bila ya shinikizo la kiimani la kuukataa.

5. Mbinu zozote za kuwashawishi Wabunge kiimani kutekeleza Maazimio ya Maaskofu chini ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, huo ni "udini" ambao ni hatari sana kwa Umoja na Mustakabali wa Taifa letu.

6. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inawakumbusha Maaskofu kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina Vyombo vya Uchunguzi na Utafiti vyenye uwezo wa kubaini maeneo yanayovunja Umoja wetu wa Kitaifa, na hata mambo yanayopingana na Katiba ya nchi yetu tuliyo nayo sasa na ile inayopendekezwa. Kamwe Maaskofu si sehemu ya vyombo hivyo. Ni vizuri wakaendelea kuongoza Ibada na kazi hizo za Uchunguzi wakawaachia walioaminiwa kuzifanya.

7. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inachukua fursa hii kuwakumbusha Maaskofu na Watanzania kwa ujumla kwamba "Hofu" ya kuwepo Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara ni hofu "bandia", kwani kesi zinazohukumiwa kwa mujibu wa Sheria ya Kiislam zinazohusiana na Ndoa ya Kiislamu, Talaka, Miirathi, Wasia, Waqfu na Malezi ya Watoto zinapatiwa uamuzi (hukumu) katika Mahakama zilizopo na kwa miaka kadhaa na wala Maaskofu hawajapata kudai ziondolewe kwa kuwa ni za kidini.

Ieleweke kuwa wanachoomba Waislamu ni kubadilishiwa Hakimu ili aje Kadhi ambaye ana taaluma na uelewa mpana wa Sheria ya Kiislamu. Je, ni vipi kasoro ya Dini ionekane baada ya kuletwa Kadhi atakayezipatia hukumu za kesi hizo na isionekane sasa wakati zipo Mahakamani kwa Hakimu anayezikosea hukumu hizo?

8. Kuhusu hofu ya Maaskofu kwamba, kwa kuwa baadhi ya Taasisi za Kiislamu hazikubaliani na Mamlaka ya Mufti wa Tanzania kwenye masuala yao, na hivyo kuijumlisha hoja hiyo kama hoja ya kutaka muswada huo uondolewe kwa ujumla wake, tunapenda kuwakumbusha na kuwataka viongozi wa kikristo wayaache mambo ya ndani ya waislamu yashughulikiwe na waislamu wenyewe.

Kadhalika wakumbuke kauli yao " Ya Kaizari mpe Kaizari, na ya Mungu mpe Mungu" na hivyo basi waiache Serikali na Bunge kutekeleza majukumu yao bila ya kuingiliwa kiimani. Viongozi wa Kikristo watambue kuwa Waislamu wanajua migongano na mifarakano iliyopo ndani ya makanisa lakini waislamu hawajathubutu kuyaingilia mambo ya ndani ya wakristo kwa namna yoyote na wamewaachia Wakristo watatue matatizo yao wao wenyewe.

Viongozi wa Kikristo waache kuwadanganya Waislamu kwa "huruma ya mamba" na ikiwa kweli Viongozi hawa wa Kikristo ni wasikivu wa sauti ya Baadhi ya Taasisi za Kiislamu wangefanyia kazi madai ya uwepo wa "Mfumo Kristo" yaliyotolewa hadharani na Taasisi hizo.

9. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania itashangazwa sana iwapo Serikali itaamua kuuondoa Bungeni Muswada unaolenga kuitambua Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara kwa kisingizio cha kupingwa na baadhi ya Taasisi za Kiislamu na chembilecho itadhihirika wazi kuwa Serikali imeuondoa Muswada huo kutokana na shinikizo la Jukwaa la kikristo, kwa kuwa ni Serikali hii iliyoamua kuendelea na mchakato wa SENSA mwaka 2012 pamoja na kupingwa na baadhi ya Taasisi za Kiislamu.

10. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inawaomba Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wazingatie viapo vyao vya kuitumikia nchi hii na watu wake kwa uadilifu na bila ya kuathiriwa na shinikizo la kiimani lililotolewa na Maaskofu kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania waupokee Muswada huo na waupime kwa hoja na kutoa majibu yenye hoja, na kamwe wasikubali wagawanywe kiimani kwani jaribio la kuligawa Bunge kiimani ni jambo la hatari linalotishia kuligawa Taifa la Tanzania.

11. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania haina pingamizi na dhamira ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwafahamisha "wenye hofu" na uwepo wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara kuwa Mahakama hiyo haina madhara yoyote kwa Umoja, Mshikamano na Mustakabali wa Taifa la Tanzania. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inaahidi kumpa ushirikiano wowote atakaouhitaji katika utoaji wa elimu hiyo.

12. Mwisho, Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania inawaomba Waislamu wote nchi nzima kuwa watulivu na kuendelea kuiombea nchi yetu isiingie katika machafuko yoyote.

Wabillahit Tawfiiq



 

Attachments

  • TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA.pdf
    175.8 KB · Views: 1,289
  • katoriki.JPG
    katoriki.JPG
    7.8 KB · Views: 39,284
  • katoriki2.JPG
    katoriki2.JPG
    6.5 KB · Views: 16,136
Haya si yale yale ya wale walioyasema waliosusia Bunge Maalum la Katiba? Hakuna jipya hapa.

Hii katiba ya maharamia ya ccm haitapita waislamu mmewadangmanya mtawapa mahakama za kadhi hamjatekeleza mtegee kura za HAPANA kutoka kwa waislamu CCM imeshapoteza dira
 
Mkuu Lizaboni Jukwaa la wakrsto Tanzania wametoa maoni yao ambayo kwa kiasi kikubwa ni kilio cha waTanzania wote wenye moyo safi.

Mosi Mahakama ya kadhi inatumiwa na wanasiasa kama mtaji wa kujipatia kura katika uchaguzi mkuu bila kutazama madhara yatakayoweza kulipata taifa iwapo mahakama hiyo itapitishwa na kuwa sheria.

Pili mimi sijali sana muundo wa serekali iwapo muundo huo utatupatia majibu ya namna serekali ya Tanganyika na serekali ya Zanzibar na mipaka yake,michango ya uendeshaji wa muungano.

Tatu katiba mpya lazima ijibu tatizo la maadili ya viongozi si kama ilivyo sasa tume ya maadili ya viongozi haina meno,haitoi maamuzi tunaweza kusema bila shaka yoyote vikao vyake havina tafauti na vikao vya kitchen party.China imepiga hatua kubwa kwasababu suala la maadili kwao ni suala la kufa au kupona.

Nne tunaka Rais mwenye madaraka yenye mipaka hatutaki Rais mwenye madaraka makubwa utadhani anamwakilisha Mungu.Tunataka wabunge wabaki kuwa wabunge,mawaziri wawe mawaziri......Tunataka ukomo ktk nafasi za ubunge,udiwani na nafasi zote za kuchaguliwa.Tumechoka na style za J Makweta au Mzindakaya.

Katiba lazima itoe majibu pasipo ubabaishaji,hila,ghiliba...



 
Katiba ya chenge na maCCM sio katiba ya wananchi... Hata wakilazimisha tutaanza kuandika katiba upya siku tukimng'oa mkoloni mweupe CCM!!
 
Back
Top Bottom