Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...


Wanabodi,

Hatimaye Baraza jipya la Mawaziri ndio lianza kutangazwa sasa live kupitia TBC!
Endelea kufuatilia...

UPDATES:


  • Wizara ya maji imeunganishwa na Kilimo - Itakuwa Wizara ya Kilimo na umwagiliaji!
  • Kazi ajira na vijana - kitengo cha vijana kimehamishiwa michezo na utamaduni
  • Uwezeshaji wa wananchi (Baraza la uwezeshaji) - Ilikuwa wizara ya fedha, imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kulielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Waziri wa TAMISEMI atakuwa na manaibu wawili
  • Wizara ya Miundo Mbinu imepunguzwa, imegawanyika kuwa na Wizara ya Ujenzi (barabara na viwanja vya ndege) & Wizara ya Uchukuzi - Reli, bandari na usafiri wa majini
  • Magufuli atachukua wizara ya Ujenzi na msaidizi wake ni Mwakyembe
  • Sitta atakuwa waziri wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki
  • Membe ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje
  • Ngeleja ataendelea kubaki wizara ya Nishati na Madini
  • Wizara ya Mambo ya Ndani atakuwepo Nahodha akishirikiana na Kagasheki
  • Anna Tibaijuka atakuwa waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi
  • Hakuna jina la Januari Makamba wala Lowassa kama wengi walivyokuwa wakishuku

WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:

baraza_Page_1.jpg

baraza_Page_2.jpg

baraza_Page_3.jpg


hakuna jipya
 
Last edited by a moderator:
Nilishapredict kuwa hakuna jipya kwenye baraza hili jipya.
Kumrejesha Nagu ni another disaster.
kuna majina mengi humo yana walakini kuhusu uadilifu wao
 
Jamani Celina Kombani hata kiingereza hajui ataiwezaje wizara ya Katiba na sheria? Je atasaidiaje/kukwamisha harakati za kudai katiba mpya?

mama kombani ni msomi mwenye masters na anazungumza kiengereza vizuri acha dharau gurudumu!
 
hata hawa walionunuliwa na MAFISADI WAMEITWA....WACHA WAENDE KWANI IKULU ZAMANI PALIKUWA MAHALI PATAKATIFU LKN ENZI HIZI ZA KIKWETE NI MAHALI PA WAHUNI KM CLOUDS FM NA AKINA KIBONDE..........+PJ NA VIKARAGOSI VINGINE

Nawaona ma editors wa vyombo mbalimbali vya habari hadi clouds radio ndani ya nyumba, nadhani pia itakuwa live kwenye redio yao.
 

Wanabodi,

Hatimaye Baraza jipya la Mawaziri ndio lianza kutangazwa sasa live kupitia TBC!
Endelea kufuatilia...

UPDATES:

  • Wizara ya maji imeunganishwa na Kilimo - Itakuwa Wizara ya Kilimo na umwagiliaji!
  • Kazi ajira na vijana - kitengo cha vijana kimehamishiwa michezo na utamaduni
  • Uwezeshaji wa wananchi (Baraza la uwezeshaji) - Ilikuwa wizara ya fedha, imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kulielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Waziri wa TAMISEMI atakuwa na manaibu wawili
  • Wizara ya Miundo Mbinu imepunguzwa, imegawanyika kuwa na Wizara ya Ujenzi (barabara na viwanja vya ndege) & Wizara ya Uchukuzi - Reli, bandari na usafiri wa majini
  • Magufuli atachukua wizara ya Ujenzi na msaidizi wake ni Mwakyembe
  • Sitta atakuwa waziri wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki
  • Membe ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje
  • Ngeleja ataendelea kubaki wizara ya Nishati na Madini
  • Wizara ya Mambo ya Ndani atakuwepo Nahodha akishirikiana na Kagasheki
  • Anna Tibaijuka atakuwa waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi
  • Hakuna jina la Januari Makamba wala Lowassa kama wengi walivyokuwa wakishuku
WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:

baraza_Page_1.jpg

baraza_Page_2.jpg

baraza_Page_3.jpg



Very POOR FOCUS
 
Last edited by a moderator:
Naona Samuel Sitta ndio wamemmaliza kabisa


Sure.... wamempeleka magharibi kusikofikika!!!! Bora angebaki mbunge wa kawaida lbda tungemsikia ama angeamua kusinzia tu bungeni!!!! Siasaaaaaa....:yuck:
 
Source: Michuzi Post

BARAZA JIPYA LA MAWZIRI

1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe
Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira
2.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano) Samia Suluhu
2. Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
NAibu: Pereira Ame Silima
7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
15. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu😀r. Fenella Mukangara
24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge

Maoni Yangu:

Nimelipenda baraza la mawaziri kwa upande mmoja ila kuna maeneo yananipa mashaka kuyakubali.

Nimekubali sana the way alivyowapanga Magufuli, Mwakyembe, Anna Tibaijuka & Cyril Chami. Pia kuwaacha kwenye mataa kina Masha (tulikuwa na wasiwasi kuwa angemteua kwenye wabunge viti vyake na kumpa uwaziri), Meghji, Lowassa, January Makamba (tungezikoma kelele za Makamba - mwanangu ni waziri ati...!!) na Batilda Buriani (tulikuwa na wasiwasi kuwa angemteua kwenye wabunge viti vyake na kumpa uwaziri).

Ila nina wasiwasi wa mapokeo ya uteuzi wa Mkullo (kwa Ministry ya Fedha) and Makongoro Mahanga. Mkullo anajulikana kuwa victim wa chujio la Mkapa katika kung'oa mizizi ya ufisadi katika mashirika ya umma. Pia nina wasiwasi na uwezo wake kama waziri wa fedha kwa kuangalia namna ambavyo alishindwa kusimamia maswala kama kushuka kwa thamani ya shilingi ya kitanzania kwa kushirikiana na Bro. Beno Ndulu. Makongoro Mahanga; wengi wetu tunajua aliyoyafanya kwenye uchaguzi; mtu ambaye kashinda uchaguzi kwa kuchakachua kura tena kwa kushikwa na masanduku ya kura kunazidi ku-confirm uhalali wa uchakachuaji ndani ya CCM. Hii ni dosari kwa JK and inabidi aifahamu mapema.

Kwa upande mwingine, wizara ya mambo ya ndani mimi naona kapiga nje kidogo. Pale alipaswa kuweka mtu kichwa maji ambaye angekimbizana na jeshi la polisi katika kutokomeza ujambazi / uhalifu nchini. Kumweka Nahodha mkazi wa Zanzibar asiyefahamu challenges za uhalifu nchini kwa undani zaidi inanipa wasiwasi sana. By the way, Nahodha from Uwaziri Kiongozi to normal waziri...!!!! Wataalamu wa siasa mnisaidie..!!

Sitta naye angepaswa zaidi apelekwe kwenye wizara ya Sheria na Katiba. Jamaa kwa elimu ya sheria na uzoefu kwenye miswada ya sheria; angeweza kusaidia sana kwenye miswada ya sheria na kuweza kumdhibiti Mwanasheria Mkuu and Spika katika hili. I doubt uwezo wa Celina Kombani kukimbiza wanasheria nchini; wanaofahamu uwezo wake kielimu na kiuzoefu watupe data. Wataalamu wa siasa mnaweza kutusaidia

Hayo ni maoni yangu tu..!!
 
Kwa picha hiyo....swali...je,nani anaandaliwa kwa ajili ya uras 2015?
 
Nilishapredict kuwa hakuna jipya kwenye baraza hili jipya.
Kumrejesha Nagu ni another disaster.
kuna majina mengi humo yana walakini kuhusu uadilifu wao

Kwake yeye anaona ni sawa tu
 
Uteuzi si mbaya ila ni jambo moja lakini kudeliver ni jambo la lingine tusubiri tuone. Ila kwangu mie uteuzi huu si mbaya I think amekuwa more strategic na objective kapata ushauri mzuri. Sasa Je yeye mwenyewe atapunguza matanuzi ya kwenda nje kila kukicha kwa kodi zetu???

Afadhali angekuwa anaenda kila siku USA lkn angetupa Baraza dogo kuliko kuamua kukaa TZ na kuunda Baraza kubwa kama hili,huyu jamaa hajajifunza kabisa kwa nini mwaka 2005 alipata kura nyingi zaidi ya mwaka huu!

Rais makini huwezi kuunda Serikali ya watu 50 kwa nchi maskini kama hii!
 
Kwa Mtazamo wangu January Makamba angepewa wizara ya Maendeleo ya jamii wanawake na watoto, huyu mama Kilaza Sophia Simba ana nini na Mkwere? Halafu Jembe Prof Mwakyusa alikosea wapi? Prof Kichwa sana yule uliza aliofundisha Muhimbili miaka hiyo.
 
Sasa bongo itakuwa nyu yoki kikwelikweli.....mataa....lami kila kona....sky scrapper....thas worup
 
Sure.... wamempeleka magharibi kusikofikika!!!! Bora angebaki mbunge wa kawaida lbda tungemsikia ama angeamua kusinzia tu bungeni!!!! Siasaaaaaa....:yuck:

Hiyo ndio SI-HASA from being a HERO watu wanakufanyia zengwe hadi utaelekea sehemu ambayo kamwe hautasikika
 
This is very useful sio wengine wanaponda lakini hawatoi sababu za msingi.
mimi nimekubaliana na kikwete kwa hawa

mathayo david msuya : Mifugo na uvuvi
see his cv david mathayo david - wikipedia, the free encyclopedia hapa taaluma itamsaidia kuinua hali ya wafugaji



membe :

Profesa mnyaa
he is a technocrat in perspective of that post

wizara ya ardhi, nyumba na makazi :
Prof tibaijuka, this will bring her experiece from un on the same

ngereja
he did good job last term

magufu + makyembe
hakuna mikataba ya ovyo any more na hakuna uzembe wa makandarasi any more , hapa safi saaaana

maghembe
anaenda kutumia taaluma yake sasa kule kilimo

maji
mwandosys did a good job last term


mimi hao tu ndio nimekubali
 
JK na CCM yake wametudharau vya kutosha,wametuona wa TZ ni wajinga wasio weza kufanya lolote hata watendewe chochote kile;JK anahisi TZ ni yao pekee yao!

Kwa nchi maskini kama hii BARAZA LA MAWAZIRI LENYE WATU 50 NI LA KAZI GANI ?As a nation;We have to do something(peacefully)to show him "we're not stupid as he think"!

Haki ya Mungu we have to act immediately to stop him;Kwa uchumi wetu huu ulivyo "Baraza la Kishetani kama hili la kazi gani"?!

Ndaga
 
Back
Top Bottom