Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Labda wizara elimu ataimudu maana yy mwalim muda mrefu sana pale udsm chemical and processing eng....kule mawasiliano alilazimishia tu

Hamna chochote, labda angepewa Magufuli... Tena huyu na udokta wake ni mbumbu la kupndukia kiutendaji... Wizara ngum, yataka IRoN MAn to HandLe
 
Tutegemee kufunga mikanda viunoni for 5 years!
 
Mkulo mhhhhh! But Comrade ameenda Tamisemi, huo uchaguzi wa 2015 tutegemee kuona makucha ya kazi aliyoibobea, lol!
 
Baraza jipya la Mawaziri,Hili hapa!
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe

Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira

2.Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia

3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano) Samia Suluhu

2. Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa

4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi

2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu

5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika

Naibu: Aggrey Mwanri

Naibu: Kassim Majaliwa

6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo

Naibu: Gregory Teu

NAibu: Pereira Ame Silima

7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha

Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki

8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani

9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi

10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo

Naibu: Benedict Ole Nangoro

12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Naibu: Charles Kitwanga

13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye

14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige

15. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima

16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli

Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe

17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu

Naibu: Athumani Mfutakamba

18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami

Naibu: Lazaro Nyalandu

19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa

Naibu: Philipo Mulugo

20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda

Naibu: Dr. Lucy Nkya

21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga

22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu

23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi

Naibu😀r. Fenella Mukangara

24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta

Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah

25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe

Naibu: Christopher Chiza

26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya


Kwa mara ya kwanza ninampongeza Mh Mkwere Jakaya Kikwete, amejitahidi kuunda baraza zuri kutokana na kundi la chaka la watu wabovu. Tutegmee mabadiliko

Kuna watu ni watendaji na si bla bla wako ndani ya baraza lake. Binafsi nimefurahia kuwepo kwa Dr Mwakyembe, Prof Mwandosya, Dr Mponda kwenye Afya, jamaa ni mchapa kazi sana na hana chembe ya Ufisadi. PhD yake ni ya kwenye mambo ya Global health. Sidhani kama ataleta mauza uza ya bajaj. Wengine ni akina Magufuli, Nyalandu, Matayo, Tibaijuka, Omar Nundu.

Kama kawaida na magarasha amerudisha, sitegemei chochote kwa Makongoro, Sophia, Nagu, Lukuvi, Mkulo na Ngereja


Mtazamo wa Mchungaji huu
 
Eti ni engineer na awamu iliopita aliwa Industry Director for the Government........!!! Duuh

Siwalaze, labda unaongelea mtu mwingine. La kama si hivyo, basi kumbuka waliyosema wahenga kwamba, Jambo usilolijuwa ni kama usiku wa giza. Wakati mwingine ni vyema kukaa kimya endapo huna la kusema.
Omari Nundu Ni Engineer (Aeronautical Engineering) by profession. Na mpaka leo hii bado ni President wa International Civil Aviation Organization (ICAO).


Omari Rashid NUNDU
UNIVERSITY EDUCATION AND ACADEMIC INTEREST


· BSc (Hons) in Aeronautical Engineering - Glasgow University (1971-75)

​

Final year Honours majors included:

1. Mathematics 1V,


2. Aerospace Dynamics 1V,


3. Fluid Mechanics 1V,


4. Aerospace Structures 1V and


5. Gas Dynamics and Thermodynamic Machines 1V.

​

Final Year Honours Dissertation: "Turbulent Airflows Around Buildings"

· MSc in Air Transport Engineering - Cranfield University (1978/79)

Thesis: " The Measurement and Control of Airliner Fleet Dispatch Availability"

· Current Research work: "Optimisation of Air Traffic Flows under Free Flight Concept in All Phases of Flight"




2.0 WORKING EXPERIENCE ​


· 2008: President of the Air Navigation Commission

  • 2007: First Vice President of the Air Navigation Commission.
· 2006 – to date: Member of the Air Navigation Commission.

· 2004 – 2005: Observer on the Air Navigation Commission

· November 2003 – to date: Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to ICAO

· November 2002 – to date: Director of International Affairs, Tanzania Civil Aviation Authority.

  • April 1992 - October 2002: Head of Civil Aviation Sector, Southern African Development Community (SADC).
· May 1989 to 31 March 1992: Senior Management Consultant responsible for the aviation programme, Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI).

· 1982 – May 1989: Director/Co-ordinator of Special Projects and Project Manager of Kilimanjaro Aircraft Maintenance Facilities (KIMAFA)

· 1977 – 1982: Superintendent Technical Planning and Services, Air Tanzania Corporation.

· 1975 – 1977: Aircraft Maintenance Engineer and Planning & Development Engineer, East African Airways Corporation

· October 1975: Assistant Executive Engineer (aircraft), Ministry of Transport and Communications, Tanzania..

*Kwa kifupi, huyu mzee anastahili kabisa kuwemo kwenye baraza hili la mawaziri.
 
Tulipe balaza muda wa siku 100 tuone performance yake, sina shaka wala wasi wasi na watu kama Magufuri kwenye wizara ya Ujenzi. Najua sasa kipere kimepata mkunaji, ila akina Sophy, Nagu, Kawambwa, Membe, Mkulo, Celina. Mwinyi, Ngereja na jamaa yao Malima hawa hawana record nzuri ya kusifiwa, ni watu wa mazoea na kutafuta sababu za kujitetea kukwepa uwajibikaji!
 
Hongera sana Jk, umnifurahisha nakunipa kidogo matumaini, ila tunalia bado na Ruge Mutahaba,huyu ana nini kwako. kwanini husikii kilio cha wasanii, kwanini bwana mdogo huyu akuharibie sifa ?
 
Yaani hawa ndo watu makini na wachapa kazi alioahidi kutupatia siku alipohutubia bunge??? Kwa kweli sikio la kufa halisikii dawa. Yaani hili la baraza la kuiangamiza CCM. wait and see

...I have the same bad feeling!
 
kulikoni ambapo hapajajazwa? ni bado hajachagua?
ila nimefurahi kuona majina mengi nisiyoyajua
 
kidogo Jk kakonga nyoyo za watu kwa upande wa magufuli na kuchagua vijana na kuachana na wazee. nampongeza kawaondoa watu kama Msola ambao hawana jipya zaidi ya kuendekeza kusujudiwa. Naamini kuna mtu amemtonya JK kuhusu mwenendo wa Msola.

Mkuu mbona una hasira sana na Msola? Si afadhali Angemuweka Msola Elimu kuliko aliyewekwa?
 
Lowassa kukosa uwaziri haihalalisha kuanza kuchambua baraza hili kwa madhehebu........ukiacha ukatoliki ...kuna madhehebu karibu 100 ya protestants ..tukitaka kila kundi ...itakuwa ngumu..

waislamu pia kuna sunni,shia,answar sunna etc.......

Kikwete amejitahidi kadiri ya uwezo wake ku balance hili la dini......the situation is fragile na amejitahidi....kasoro hazikosi Ikiwemo ukubwa wa baraza ...bado ni kubwa ..na kuna wazanzibar wamepewa wizara ambazo si za muungano..mfano mawasilioano [kule zanzibar wanayo wizara hiyo]...

Pia mtu kama sitta amekuwa undermined amepewa tu ili kum contain..ningekuwa mimi ni yeye nisingekubali uteuzi....back bench kungekuwa kwa heshima zaidi kwa siitta kuliko wizara isiyo na umuhimu mkubwa ya afrika mashariki aliyopewa...

uteuzi wa magufuri na tibaijuka unatia matumainidini
 
Nafikiri si vema kusema Sitta au Mwakyembe wamepozwa. Siku zote Kulaumu ni Kazi nyepesi kuliko kutenda.....tuone nao wao watatenda nini....!!!
 
Nilisema: huyu jamaa mshamba. Hivi kweli anajua matatizo ya Watanzania? anajali taabu zao? Ana akili timamu kweli? Watu 50 wanfanya nini katika nchi maskini ya kutupwa kama Bongo? Akh, sijui nimweke katika kundi gani- immature, opportunist, dumb, don't care or just hayawani?,
Jamani Watanzania huu ni wakati wa ku take action. Mpaka lini tutaendelea kuwaachia watu ovyo kufanya experiments zao juu ya miili yetu? Tuwape siku 100 kwanza tusipoona dalili za kudeliver tuanze vituko. Enough is enough!
 
Nilisema: huyu jamaa mshamba. Hivi kweli anajua matatizo ya Watanzania? anajali taabu zao? Ana akili timamu kweli? Watu 50 wanfanya nini katika nchi maskini ya kutupwa kama Bongo? Akh, sijui nimweke katika kundi gani- immature, opportunist, dumb, don't care or just hayawani?,
Jamani Watanzania huu ni wakati wa ku take action. Mpaka lini tutaendelea kuwaachia watu ovyo kufanya experiments zao juu ya miili yetu? Tuwape siku 100 kwanza tusipoona dalili za kudeliver tuanze vituko. Enough is enough!
Mimi nadhani JK amejitahidi sana kuunda Baraza la Mawaziri lenye uwezo wa kuleta ufanisi kwa kiwango kikubwa. Muundo wa Baraza hili ni mzuri. watu makini zaidi wameingizwa kwenye uongozi wa nchi. Ila bado siasa ina nafasi yake katika utawala wa nchi za kiafrika. ndio maana kuna sura ambazo tunadhani zisingekuwepo.

Ukubwa au udogo wa Baraza hili la mawaziri si tatizo sana. Maana limepungua kidogo. Na kama tatizo ni gharama, hata wakiwa wachache wanaweza kutumia pesa nyingi katika uendeshaji wa serikali bila kuleta ufanisi wowote. Siamini kuwa viongozi wasiozidi 20 (nyongeza ya Baraza linaloonekana kufaa) wanaweza kusababisha upungufu mkubwa sana katika matumizi ya serikali.

Tutakapoweza kuwa na Katiba inayoweza kutoa mwelekeo wa aina na ukubwa wa Baraza la mawaziri, labda ndipo tatizo lolote juu ya uundwaji wa Baraza la mawaziri, litakapopata ufumbuzi.

Sina uhakika kama kuna lolote linaloweza kufanywa endapo hawatatimiza matarajio ndani ya hizo siku 100.

Katiba ya nchi inamruhusu Rais kuteua mtu yeyote mwenye sifa za Ubunge kuwa Waziri katika Wizara yoyote kadiri anavyoona inafaa.

Tunachofaa kufanya ni kuwaombea waweze kutekeleza wajibu wao vyema na kwa uadilifu mkubwa ili Taifa liweze kusonga mbele. wakishindwa, hakutakuwa na faida yoyote kwa mTanzania yeyote.
 
Back
Top Bottom