Balozi wa Tanzania Nchini India Ametoa Ufafanuzi Sakata la Binti Wa Kitanzaia Anayedaiwa Kufukuzwa Ubalozini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ubalozi wa Tanzania nchini India umetoa ufafanuzi kuhusu Mtanzania, Sayuni Eliakim aliyedaiwa kushindwa kusaidiwa ubalozini hapo kupata hati ya kusafiria ili arudi Tanzania.

Ubalozi huo umetoa ufafanuzi ikiwa ni siku mbili tangu taarifa hizo zilizodai Sayuni aliyedaiwa kunyanyang’anywa hati ya kusafiria na mwenyeji wake kuwa alikosa huduma ubalozini hapo na kumtaka arudi ajaze maombi hayo kwa njia ya mtandao.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 28, 2023 na Balozi wa Tanzania nchini humo, Anisa Mbega ambaye amesema kuwa Sayuni alizidisha muda wa kibali chake cha ukaazi nchini humo, hivyo kuna ugumu katika mchakato wa kumrudisha Tanzania.

“Sayuni Eliakim aliingia nchini India mwaka 2018, na kukaa kwa muda mrefu hadi kujikuta muda wake wa ukaazi umepita. Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji za India, raia wa kigeni ambaye amepitisha muda wake wa ukaazi, haruhusiwi kutoka nchini India, isipokuwa kwa utaratibu maalum uliowekwa.

“Utaratibu huo ni pamoja na kuomba ruhusa ya kutoka nje ya nchi (Exit Permit). Maombi ya ‘Exit Permit’ yanatakiwa kufanyika katika mji ambao mhusika anaishi (kwa upande wa Sayuni mji anaoishi ni Bangalore). Sayuni alielekezwa kuhusu utaratibu huo na maombi yake hadi hivi sasa yanaendelea kufanyiwa kazi,”amesema Balozi Anisa.

Balozi Anisa amesema wanaendelea kumsaidia Sayuni kwa kumpatia Hati ya kusafiria ya dharura (ETD).

Aidha, Ubalozi umetoa rai kwa Watanzania kujiepusha na kuchukua tahadhari na watu wasio waaminifu wanaowalaghai kuhusu kuwepo kwa nafasi za ajira zisizo na ujuzi kwa raia wa Tanzania nchini India.

View: https://www.instagram.com/p/Cwe4JaoN7sX/
 
Jukumu la undugu ni kumpambania ndugu yako kwa namna yoyote..hao ubalozi ni wajinga tu

Mmarekani au mzungu ata hafanye nini nchi za watu wapo tayari hata kuonga ili atoke

Sio hii mitoto ya ccm yalioka kwenye balozi zetu yana roho mbaya
 
Ubalozi wa Tanzania nchini India umetoa ufafanuzi kuhusu Mtanzania, Sayuni Eliakim aliyedaiwa kushindwa kusaidiwa ubalozini hapo kupata hati ya kusafiria ili arudi Tanzania.

Ubalozi huo umetoa ufafanuzi ikiwa ni siku mbili tangu taarifa hizo zilizodai Sayuni aliyedaiwa kunyanyang’anywa hati ya kusafiria na mwenyeji wake kuwa alikosa huduma ubalozini hapo na kumtaka arudi ajaze maombi hayo kwa njia ya mtandao.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 28, 2023 na Balozi wa Tanzania nchini humo, Anisa Mbega ambaye amesema kuwa Sayuni alizidisha muda wa kibali chake cha ukaazi nchini humo, hivyo kuna ugumu katika mchakato wa kumrudisha Tanzania.

“Sayuni Eliakim aliingia nchini India mwaka 2018, na kukaa kwa muda mrefu hadi kujikuta muda wake wa ukaazi umepita. Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji za India, raia wa kigeni ambaye amepitisha muda wake wa ukaazi, haruhusiwi kutoka nchini India, isipokuwa kwa utaratibu maalum uliowekwa.

“Utaratibu huo ni pamoja na kuomba ruhusa ya kutoka nje ya nchi (Exit Permit). Maombi ya ‘Exit Permit’ yanatakiwa kufanyika katika mji ambao mhusika anaishi (kwa upande wa Sayuni mji anaoishi ni Bangalore). Sayuni alielekezwa kuhusu utaratibu huo na maombi yake hadi hivi sasa yanaendelea kufanyiwa kazi,”amesema Balozi Anisa.

Balozi Anisa amesema wanaendelea kumsaidia Sayuni kwa kumpatia Hati ya kusafiria ya dharura (ETD).

Aidha, Ubalozi umetoa rai kwa Watanzania kujiepusha na kuchukua tahadhari na watu wasio waaminifu wanaowalaghai kuhusu kuwepo kwa nafasi za ajira zisizo na ujuzi kwa raia wa Tanzania nchini India.

View: https://www.instagram.com/p/Cwe4JaoN7sX/

nilishaishi nje sana, balozi za Tanzania ni tofauti kabisa na balozi kama za marekani na wengine wakizungu. kwa watanzania, huwa hawana msaada hadi uwaaibishe au waone umewatangaza kama hivi, na hata ukitembelea ubalozi wao huwa wanaamini umeenda kuomba msaada, hivyo cha kwanz akufanya huwa ni kujikung'uta,kumbe pengine hata hauhitaji msaada wa kipesa kabisa. wanatakiwa kujirekebisha, wapo kule kwa kodi zetu, tumewaajiri, wapo kwa ajili ya maslahi yetu hata kama mtu atakuwa amefanya makosa wanatakiwa kuwepo pale kwa ajili yake kumsaidia. mnachotakiwa kujua ni kwaba, hawa mabalozi ni hawa wafanyakazi wa umma walioko kwenye maofisi yetu hapa bongo na wakiteuliwa kwenda nje huwa wanaenda na nyodo hizi hizi na kiburi hiki hiki, kama unavyoweza usihudumiwe vizuri kwenye ofisi za umma hapa bongo hii inaenda hadi kwenye balozi zetu kwasababu ni hawahawa tu, yaani ni hawahawa.
 
Back
Top Bottom