Balozi wa India Nchini Tanzania amuaga rasmi Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt. Stergomena Tax

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Balozi wa India Nchini Tanzania Amuaga Rasmi Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt. Stergomena Tax

Tarehe 03 Januari, 2024 Balozi wa India nchini Tanzania, Mheshimiwa Binaya Srikanta pradhan amemtembelea Waziri wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Dkt.Stergomena Lawrence Tax (Mb), ofisi kwake Upanga, jijini Dar es Salaam.

Ujio wa Balozi na ujumbe wake, ulikuwa na lengo la kuaga rasmi baada kumaliza muda wa kufanya kazi hapa nchini Tanzania. Wakati wa mazungumzo baina yao, Mheshimiwa Waziri alimpongeza kwa dhati kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya kwa kipindi chake chote alichofanya kazi ya kuiwakilisha nchi yake hapa nchini, katika kudumisha na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na India, kupitia maeneo mbalimbali hususan yahusuyo Sekta ya ulinzi.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amemweleza Balozi kuwa katika kipindi chake, alifanya kila aina ya jitihada za kuhakikisha kuwa Serikali ya India inaendelea kushirikiana na kuisadia Tanzania kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo hususan kwenye sekta ya Ulinzi.

Hata hivyo, Mheshimiwa Stergomena amemhakikishia Balozi huyo kuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi kwa ujumla, itaendelea kushirikiana na Serikali ya India kupitia nyanja mbalimbali za kiulinzi hususan kwa mambo yale yote waliyokubaliana na bado utekelezaji wake unaendelea. Vile vile, Dkt. Stergomena amemtakia Mheshimiwa Balozi safari njema ya kurejea nchini kwake.

GC8eySXW4AAz58O.jpg
 
Back
Top Bottom