Hati ya utambulisho ya Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Ali Jabir Mwadini amewasilisha nakala ya Hati ya Utambulisho kwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Ulaya na Mambo ya Nje nchini Ufaransa Bw. Mathieu Carmona, tarehe 17 Oktoba, 2023.

Katika mazungumzo yao Bw. Carmona ametambua uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa na kuahidi kumpatia Balozi Mwadini ushirikiano wa kutosha. Aidha, Balozi Mwadini naye ameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Ufaransa.

20231017_143439.jpg
20231017_143448.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom