Balozi Tsere ataka Rais Samia kukaa na Wapinzani kama Kikwete ili kujadili Katiba Mpya

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,220
2,000

Balozi mstaafu, Patrick Tsere amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na kufanya mazungumzo na wadau wanaotaka Katiba mpya ili kupata mwafaka wa kitaifa.​

Kauli ya Tsere, aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Malawi imekuja wakati kukiwa na harakati mbalimbali za madai ya Katiba, huku Rais Samia, aliyeingia madarakani Machi mwaka huu akiwataka wenye madai hayo wamwache kwanza ajenge uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Tsere alisema angekuwa mshauri wa Serikali, angeshauri kuitwa kwa wote wanaotaka Katiba mpya kwa ajili ya kubadilishana mawazo ili kupunguza joto lililopo sasa.

“Mazungumzo hayo ya kirafiki tu, yanaweza kupunguza joto lililopo sasa, yaani ni kama ambavyo Jakaya (Rais mstaafu Jakaya Kikwete) alivyokuwa akifanya.

“Alikuwa akiwaita kina Mbowe (Freeman- Mwenyekiti wa Chadema) na kukaa nao pamoja si kupoteza ajenda, bali kupunguza tu joto,” alisema Tsere.

Huku akionyesha kusikitishwa na hatua ya kudhibitiwa kwa wanaodai Katiba mpya, balozi Tsere alisema, “leo hii hata mtu akisema hebu tupitie kidogo au tuzungumze kuhusu Katiba watu hawataki!

“Mimi nafikiri Rais awaite hao watu, yaani wadau wote kwa maana vyama vyote vya siasa kwa lengo la kuzungumza nao na ieleweke siyo kikao rasmi, bali ni kuzungumza kwanza kama rafiki.”

Juni 28 mwaka huu, wakati akijibu maswali mbalimbali ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini aliokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema: “Naomba nipeni muda nisimamishe nchi kwanza kiuchumi. Tuite wawekezaji wawekeze ajira zipatikane uchumi ufunguke, halafu tutashughulikia Katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara wakati ukifika”.

Balozi Tsere, ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ameifananisha vuguvugu ya sasa ya madai ya Katiba na ya madai ya Katiba mpya yaliyoibuka miaka ya 1990, kabla ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuunda Tume ya Jaji Francis Nyalali kuwauliza Watanzania utayari wao mwaka 1992.

Balozi Tsere alisema licha ya matokeo kuonyesha kuwa Watanzania wengi bado walikuwa wakihitaji mfumo wa chama kimoja, Mwalimu Julius Nyerere alishauri kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi.

“Taarifa ya Tume ilieleza kuwa asilimia 80 ya Watanzania hawakutaka vyama vingi na asilimia 55 ya hiyo 80 ya waliotaka chama kimoja ukiitafsiri ilikuwa inataka vyama vingi.

“Mzee Nyerere alikuwa na akili sana, akaishauri Serikali isiangalie hawa ishirini tu kwamba ndio wanataka vyama vingi na hawa asilimia 55 waangalieni maana hoja zao zinafanana,” alisema Tsere.

Alisisitiza kuwa, licha ya uchache wa waliokuwa wakitaka mfumo wa vyama vingi, bado walipewa nafasi.

“Sasa tukubaliane kwamba ni asilimia 20, kwani wachache hawapaswi kusikilizwa? Wanafaa kusikilizwa, hivyo turuhusu vyama vingi, nasema hicho kitendo alichofanya kwa maana ya ushauri aliotoa Nyerere ndio umeisaidia CCM ibaki mpaka leo madarakani,” alisema Tsere.

Alisema kama Serikali ya wakati ule ingekataa kuanzisha mfumo wa vyama vingi bado vuguvugu lingeendelea kama lilivyo suala la Katiba.

“Tunajaribu kunyamazisha lakini nafikiri huko mbeleni itafika tu litafumuka. Yaani huko siku za usoni itafika tu, tena kitu kidogo tu kinaweza kikapita na kufumua jambo hili kwa ukubwa.

“Mimi sipuuzi kabisa suala hili la Katiba na ingekuwa ni mimi ndio ningetoa huo ushauri ila nafahamu kuwa mamlaka iliyopo inajua mengi kuliko mimi ambaye nipo nje ya mfumo kwa sasa, kwa hiyo nimesema haya kwa namna ninavyoona mimi,” alisema.

Gazeti la Mwananchi.
1636791537766.png
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,607
2,000
kama kupunguza joto ni bora wasikutane, nini maana ya kupunguza joto inaweza kuwa sawa na punyet kwa kizungu ,hakitazaliwa kitu,sijui mmeiona hio janja ,sijui katumwa ili ionekane amesikilizwa kumbe ni mpango wa binadamu,mshindwe na mlegee,tunahitaji katiba mpya tume mpya ili Zanzibar nayo iondokane na makucha ya machogo.
 
Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
22,968
2,000
Ingekuwa enzi za Mwenye heri Mkuu wa kiti cha enzi KAYAFA angethubutu kusema alichosema angekimbia na Dera huyo Tsere kama si kupokwa hadhi ya ubalozi.

KAYAFA alijitafutia kifo cha bure kuutaka urais...

Eee mtakatifu KAYAFA utuombee!!
 
Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,666
2,000
Sijui kwa nini Ccm wanaogopa katiba mpya? Na huyu mama kwa vile anataka kugombea 2025 sidhani kama atakuja kukubali hoja ya katiba mpya!
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,186
2,000
kama kupunguza joto ni bora wasikutane, nini maana ya kupunguza joto inaweza kuwa sawa na punyet kwa kizungu ,hakitazaliwa kitu,sijui mmeiona hio janja ,sijui katumwa ili ionekane amesikilizwa kumbe ni mpango wa binadamu,mshindwe na mlegee,tunahitaji katiba mpya tume mpya ili Zanzibar nayo iondokane na makucha ya machogo.
Kwani zenji si ni nchi huru?
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,186
2,000
Ingekuwa enzi za Mwenye heri Mkuu wa kiti cha enzi KAYAFA angethubutu kusema alichosema angekimbia na Dera huyo Tsere kama si kupokwa hadhi ya ubalozi.

KAYAFA alijitafutia kifo cha bure kuutaka urais...

Eee mtakatifu KAYAFA utuombee!!
Wenye akili tu ndiyo watakuelewa kwa maombi hayo
 
Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,365
2,000
Sijui kwa nini Ccm wanaogopa katiba mpya? Na huyu mama kwa vile anataka kugombea 2025 sidhani kama atakuja kukubali hoja ya katiba mpya!
Uzuri ni kwamba, upinzani mkubwa alionao hivi sasa kuelekea 2025 upo ndani ya Chama chake mwenyewe.
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,936
2,000
Piga ua. Madai ya katiba mpya hayazuiliki. Uchafuzi wa 28/10/2020 "was a full catalyst for the process".
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,147
2,000
Ingekuwa enzi za Mwenye heri Mkuu wa kiti cha enzi KAYAFA angethubutu kusema alichosema angekimbia na Dera huyo Tsere kama si kupokwa hadhi ya ubalozi.

KAYAFA alijitafutia kifo cha bure kuutaka urais...

Eee mtakatifu KAYAFA utuombee!!
Nasikia wewe hata mumeo akishindwa kusimamisha ili akumbeto unamsingizia kayafa?
 
nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,936
2,000
Ingekuwa enzi za Mwenye heri Mkuu wa kiti cha enzi KAYAFA angethubutu kusema alichosema angekimbia na Dera huyo Tsere kama si kupokwa hadhi ya ubalozi.

KAYAFA alijitafutia kifo cha bure kuutaka urais...

Eee mtakatifu KAYAFA utuombee!!
Huyo katumwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom