PostGE2025 Balozi 16 kwa pamoja zaitaka Tanzania kuachia wafungwa wa kisiasa, kusitisha utekaji na kurudisha miili ya waliouawa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Tunarejea tamko la Mwakilishi Mkuu kwa niaba ya Umoja wa Ulaya la tarehe 2 Novemba 2025, na tamko la pamoja la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Norway na Uingereza la tarehe 31 Oktoba 2025, kuhusu uchaguzi nchini Tanzania.

Tumehuzunishwa sana kwa vifo na majeruhi wengi waliotokana na matukio ya wakati wa uchaguzi.

Tunatambua azma ya serikali ya kudumisha amani na utulivu wa nchi, na tunasisitiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi kutekeleza majukumu yao kwa uangalifu mkubwa. Tunarudia wito wetu kwa serikali kutekeleza ahadi zake za kimataifa za kulinda haki za msingi, ikiwemo, haki za kikatiba za kupata taarifa na uhuru wa kujieleza kwa Watanzania wote.

Taarifa za kuaminika kutoka mashirika ya kitaifa na kimataifa zinaonesha ushahidi wa mauaji nje ya utaratibu wa kisheria, kupotea kwa watu, ukamataji wa wetu kiholela na ufichaji wa miili ya waliopoteza maisha.

Tunatoa wito kwa mamlaka husika kukabidhi miili ya marehemu kwa familia zao haraka iwezekanavyo, kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa na kuhakikisha waliokamatwa wanapata misaada ya kisheria na matibabu. Zaidi, tunatoa wito kwa serikali kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti za awali za waangalizi wa uchaguzi wa AU na SADC ambazo ziliweka bayana mapungufu yaliyojiri wakati wa mchakato wa uchaguzi.

Tunakaribisha hatua ya Serikali ya kutambua kwamba kuelewa kiini na mazingira yaliyopelekea vurugu, ikiwemo vifo, ni hatua muhimu kuelekea upatikanaji wa haki na maridhiano. Uchunguzi wowote lazima uwe huru, wazi na shirikishi - ukijumuisha asasi za kirala, taasisi za kidini, na wadau wote wa kisiasa.

1764915019003.jpeg
 
Tamko la Pamoja kutoka Ubalozi wa Uingereza, Canada, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Denmark, Ufini, U.jpg
 
Back
Top Bottom