sensa ni ya kiserikali, na serikali haina dini, hivyo ni sahihi kwa kipengele hicho kutokuwepo.
Mimi kanisani kwangu tunajua kwa usahihi kabisa idadi ya wakristo kigangoni kwetu. Na askofu wa jimbo langu akiamuru apate idadi ya wakristo wote jimboni kwake anapewa ndani ya less than a week. Kwanini nyie mnaotaka idadi ya waumini wenu msitumie chain ya utawala wa dini yenu kupata idadi ya watu wenu?
Jamaa wamevurugwa kweli, kila jumuiya inatoa tamko lake. Mufti anasema hivi, mara Ponda anasema hivi, mara Jumiki inasema vile, kuna jumuiya ya wanahabari, kuna jumuiya ya wahadhiri, kuna jumuiya ya wanataaluma, kila mtu anaibuka kivyake kutegemea maslahi yameegamia wapi. Hilo la sensa, bado suala la uteuzi wa kadhi uliofanywa na mufti unawakoroga. Nadhani ingekuwapo mahakama ya kadhi, hao wanaotoa matamko wangeshakatana mikono!
Kwa mujibu wa sheria za sensa ni kosa la jinai kwa mwananchi kugoma kutoa taarifa,kutoa taarifa za uongo au kuharibu nyaraka za sensa.Sijui kma hawa wanaotaka kugomea sensa imani yao inaruhusu kutokutii sheria na mamlaka zinazowaongoza
Source:Channel 10(Mahojiano na mkurugenzi wa takwimu)
Kama wanajua ni kosa kugomea sensa kwanini wasiwakamate kwanza hao wanaohamasisha mgomo! Huyo mkurugenzi anadhani kwenda kuzungumza kwenye tv tu na huku wahalifu anawajua itamsaidia nini! Apeleke ujinga wake huko!