BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

kama unajua waislam ni wajinga na hauna fikra ya kuwafanya wawe wajanja kama nyie, huo ni ubinafsi wakufikiri kuwa labda nyie ni watu maalum, nafikiri wakristo mlichaguliwa wajanja kuliko waislam, ukizaliwa tu mkristo unakua mjanja, na ukizaliwa muislam unakua mjinga looooooooh.

Jamani ni yesu yupi anaefundisha ustawi wa ukristo ni kwa kuwadhulum waislam.

kama watanzania ustawi wa taifa zima ni muhimu ifikie wakristo waone kuna sehemu waislam wanataka msaada hata sera zetu zi akisi hali zao, si sahihi kumuona mtu akiwa muislam ni mjinga juha duh?

tusiwe bias
 
[Mkuu, ahsante kwa taarifa. Umenisaidia sana. Awali nilikuwa sijui kwamba kumbe sensa ni kwa mujibu wa maelekezo ya UN. Na kwa sababu hiyo ni lazima kufuata format ya madodoso ya UN yanayotaka kujua kuna misikiti na makanisa mangapi na pia idadi ya waumuni na madhehebu yao!!!???[/QUOTE]

unajua nimesema UN kwa sababu sababu za serikali kutoweka kipengele cha dini ilikuwa wanafata standard za kimataifa ndo maana tunasema mbona mwongo wa UN unataka kipengele kiwepo kwa hiyo wao wanatudanganya. hiyo ndo hoja nawala si kua tunafata madodoso ya UN.
 
waislam wamekataa kuhesabiwa kwenye kongamano lilofanyika jumapili jijini Arusha
wakitoa msimamo wao wamesema hawaoni umuhimu wa kuhesabiwa bila kipengele cha DINI kwani kilikuwepo kikaondolewa bila maelezo sasa waislam wanataka kipngele hicho kirudi tupate takwimu sahihi ambazo zitatumika na wadua wa maendeleo na jamii mbalimbali, kinnachoshangaza ni kwamba watahesabu nyumba za ibada bila kuwahesabu wanaosali humo. idadi ya misikiti na makanisa yanini wakati wanaosali humo hawahesabiwi.

waislam waweke bango la "Hatuhesabiwi" kwenye milango yao

mwongozo wa sensa wa UN unaelekeza kipengele cha dini na dhehebu kiwepo angalia website yake un.org

Babie Wana niruhusu nami niweke kipande hiki kutoka kitabu changu,"Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..." kipande hiki nimepitia sensa pamoja na mambo mangine:

Theluthi mbili ya Waislam wote wa Afrika ya Mashariki wanaishi Tanzania [1]ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote katika Afrika ya Mashariki, yaani Kenya, Uganda na Tanzania. Hii ni pamoja na Zanzibar nchi ya Kiislam yenye Waislam takriban asilimia tisini na tisa na kuna wakati ilikuwa ndiyo kitovu cha maarifa ya Kiislam katika Afrika ya Mashariki na Kati. Kutokana na sensa ya mwaka 1957, kwa kila Waislam watatu walikuwepo Wakristo wawili. Kwa wakati ule hii ilionyesha kuwa Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi katika nchi zote Kusini ya Ikweta. Lakini katika sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili na Waislam asilimia thelathini na Wapagani asilimia thelathini na saba. Sensa hii inaonyesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania. Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislam wamepungua nchini au kwa nini ghafla Wapagani wameongozeka katika nchi ya waumini.

Hii ndiyo ilikuwa sensa ya mwisho iliyokuwa ikionyesha mgawanyo wa dini. Inaaminika kuwa matokeo ya sensa hii yalifanyiwa mabadiliko kwa ajili ya sababu za kisiasa pale ilipobainika kuwa Waislam Tanzania walikuwa wengi kupita Wakristo. Upo ushahidi kuwa mwaka 1970, ilipobainika kuwa Waislam ni wengi Tanzania serikali iliiamrisha Idara ya Takwimu kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970.[1]

Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania umewatupa nje Waislam, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa. Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika Tanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti. Katika nchi za Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria,[1]uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano na mzozo.

Tatizo hili lipo Tanzania. D.B. Barret [1]anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo. Takwimu zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%. Takwimu za Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%. Lakini takwimu za Africa South of the Sahara,[1]zinaonyesha Waislam ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982. Kwa kuwa utafiti wa Waislam wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa, suala la wingi wa Waislam katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislam wenyewe.[1]

Mgao wa madaraka na kugawana vyeo haikupashwa kuwa sababu ya migongano na mifarakano katika Afrika. Lakini kwa bahati mbaya sana hii imekuja kuwa sababu ya mifarakano katika serikali za wananchi wenyewe. Jambo hili limekuwa ni suala nyeti kwa sababu ukabila, udini na kujuana ni kitu muhimu katika serikali za Afrika. Mgawanyo wa madaraka na wingi wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii. Kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha ubaguzi toka zama za ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislam hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.

Ukristo ni dini mpya Tanzania kwa kuwa uliingizwa katika karne ya kumi na nane na wamisionari. Kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya ukoloni. Kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kushirikiana na kuwa tiifu kwa serikali ya kikoloni. Chini ya ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga uhusiano maalum kati yake na serikali pamoja na Mkristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni. Waislam wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya mtawala.

Mwafrika Mkristo akawa mnyeyekevu kwa serikali wakati wa ukoloni na baada ya kupatikana kwa uhuru akaja kushika madaraka ya serikali. Waislam wakatengwa na kuteswa katika ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hivyo kuwaondolea fursa ya maendeleo.

Kuwepo kwa Waislam kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislam wasimame kuutokomeza ukoloni. Baada ya uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na serikali, uliojengwa na tabia ya Kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa serikali ulilelewa vyema na umeisaidia sana Kanisa. Kanisa likaweza kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasiwasi.

Kutokana na uhusiano huu maalum Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu kutokana wa Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na serikali ya kikoloni kisha na serikali ya wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika uongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama katika Tanzania. Katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania.
 
Babie Wana niruhusu nami niweke kipande hiki kutoka kitabu changu,"Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..." kipande hiki nimepitia sensa pamoja na mambo mangine:

Theluthi mbili ya Waislam wote wa Afrika ya Mashariki wanaishi Tanzania [1]ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote katika Afrika ya Mashariki, yaani Kenya, Uganda na Tanzania. Hii ni pamoja na ñ nchi ya Kiislam yenye Waislam takriban asilimia tisini na tisa na kuna wakati ilikuwa ndiyo kitovu cha maarifa ya Kiislam katika Afrika ya Mashariki na Kati. Kutokana na sensa ya mwaka 1957, kwa kila Waislam watatu walikuwepo Wakristo wawili. Kwa wakati ule hii ilionyesha kuwa Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi katika nchi zote Kusini ya Ikweta. Lakini katika sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili na Waislam asilimia thelathini na Wapagani asilimia thelathini na saba. Sensa hii inaonyesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania. Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislam wamepungua nchini au kwa nini ghafla Wapagani wameongozeka katika nchi ya waumini.

Hii ndiyo ilikuwa sensa ya mwisho iliyokuwa ikionyesha mgawanyo wa dini. Inaaminika kuwa matokeo ya sensa hii yalifanyiwa mabadiliko kwa ajili ya sababu za kisiasa pale ilipobainika kuwa Waislam Tanzania walikuwa wengi kupita Wakristo. Upo ushahidi kuwa mwaka 1970, ilipobainika kuwa Waislam ni wengi Tanzania serikali iliiamrisha Idara ya Takwimu kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970.[1]

Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania umewatupa nje Waislam, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa. Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika Tanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti. Katika nchi za Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria,[1]uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano na mzozo.

Tatizo hili lipo Tanzania. D.B. Barret [1]anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo. Takwimu zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%. Takwimu za Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%. Lakini takwimu za Africa South of the Sahara,[1]zinaonyesha Waislam ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982. Kwa kuwa utafiti wa Waislam wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa, suala la wingi wa Waislam katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislam wenyewe.[1]

Mgao wa madaraka na kugawana vyeo haikupashwa kuwa sababu ya migongano na mifarakano katika Afrika. Lakini kwa bahati mbaya sana hii imekuja kuwa sababu ya mifarakano katika serikali za wananchi wenyewe. Jambo hili limekuwa ni suala nyeti kwa sababu ukabila, udini na kujuana ni kitu muhimu katika serikali za Afrika. Mgawanyo wa madaraka na wingi wa wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii. Kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha ubaguzi toka zama za ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislam hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.

Ukristo ni dini mpya Tanzania kwa kuwa uliingizwa katika karne ya kumi na nane na wamisionari. Kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya ukoloni. Kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kushirikiana na kuwa tiifu kwa serikali ya kikoloni. Chini ya ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga uhusiano maalum kati yake na serikali pamoja na Mkristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni. Waislam wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya mtawala.

Mwafrika Mkristo akawa mnyeyekevu kwa serikali wakati wa ukoloni na baada ya kupatikana kwa uhuru akaja kushika madaraka ya serikali. Waislam wakatengwa na kuteswa katika ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hivyo kuwaondolea fursa ya maendeleo.

Kuwepo kwa Waislam kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislam wasimame kuutokomeza ukoloni. Baada ya uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na serikali, uliojengwa na tabia ya Kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa serikali ulilelewa vyema na umeisaidia sana Kanisa. Kanisa likaweza kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasiwasi.

Kutokana na uhusiano huu maalum Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu kutokana wa Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na serikali ya kikoloni kisha na serikali ya wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika uongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama katika Tanzania. Katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania.

hizi propaganda za kijinga zitaisha lini? Umeongea kwamba kanisa lilisomesha watu wake sasa tatizo liko wapi? unataka mtu asiyesoma apewe uhasibu?
 
Wandugu mi napita tu kwenye udini sina mchango,kwangu mimi waislamu na wakristu damudamu.
 
Msio Waislaam mbona mnaogopa hilo? mnachohofu nini?
 
Ona sasa mmeharibu kabisa huu uzi, badala ya kuchangia mmeingizamo hayo mambo yenu
 
waislam wamekataa kuhesabiwa kwenye kongamano lilofanyika jumapili jijini Arusha
wakitoa msimamo wao wamesema hawaoni umuhimu wa kuhesabiwa bila kipengele cha DINI kwani kilikuwepo kikaondolewa bila maelezo sasa waislam wanataka kipngele hicho kirudi tupate takwimu sahihi ambazo zitatumika na wadua wa maendeleo na jamii mbalimbali, kinnachoshangaza ni kwamba watahesabu nyumba za ibada bila kuwahesabu wanaosali humo. idadi ya misikiti na makanisa yanini wakati wanaosali humo hawahesabiwi.

waislam waweke bango la "Hatuhesabiwi" kwenye milango yao

mwongozo wa sensa wa UN unaelekeza kipengele cha dini na dhehebu kiwepo angalia website yake un.org[/QUOTEA]

UDINI UTATUMALIZA i.e BOKO HARAM,AL-SHABAB,UAMSHO etc
 
hizi propaganda za kijinga zitaisha lini? Umeongea kwamba kanisa lilisomesha watu wake sasa tatizo liko wapi? unataka mtu asiyesoma apewe uhasibu?
maju huyo ndiye Mohamed Said, msomi anayedai kuwa kwa kiwango chake cha usomi ni wachache sana humu JF wangekuwa na ujasiri wa kusimama na yeye uso kwa uso. Tatizo linakuja pale anapojikuta uso kwa uso na hoja za kisomi kuhusu porojo zake za kichochezi zilizojikita katika udini na kutakiwa kuzijibu, huyooo...ghafla usomi wake huyeyuka na kubakiwa na sifa moja tu kuu ya uchochezi.

Bahati mbaya kwake JF si kama huko kwingineko anakoweza kuzipaka rangi porojo zake zionekane kama za kweli huku akipigiwa makofi na wachovu wenziye. Hapa mara nyingi badala ya kutoa somo anajikuta yeye ndio anaishia kupewa somo, kweli JF kiboko na kama mtu hukuangalia utaingia moto lakini ukatoka baridiii!

Hayo ndiyo humkuta huyu mchochezi kila anapojaribu kupandikiza hizo mbegu za fitina na chuki kupitia huu mtandao, hatupati ng'o! Masikini Mohamed Said, toka aanze akiwa kijana na hivi sasa anazeeka bila mafanikio yoyote katika njama zake hizo...maisha yake yote analoa jasho akiusukuma ukuta ambao hata hausogei! Pole!
 
Last edited by a moderator:
Naomba niwaelimishe kidogo Wakuu wenzangu..Point ya kuwa UN wanataka tuweke kipengele cha Udini basi na sisi ndo tufuate hivyo ninamashaka na hilo.Hivi leo UN wangetaka tuweke kipengele cha Ndoa za Jinsia Moja Je tungekiweka tu kwa sababu UN wametaka? UN Wangetaka tuweke kipengele cha Ukabila Je tungekiweka tu kwa sababu UN wametaka tuweke?
Ni imani yangu kuwa pamoja na UN kusema hivyo bado kila nchi Ina taratibu zake.Kwetu sisi watanzania suala la Udini na Ukabila si kipaumbele cha serikali hivyo sioni sababu ya hicho kipengele kuwepo kwani hakitatusaidi kufanya maendeleo yoyote ya kijamii zaidi ya kuleta Chuki na Ubaguzi
 
Ukristo ni dini mpya Tanzania kwa kuwa uliingizwa katika karne ya kumi na nane na wamisionari. Kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya ukoloni. Kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kushirikiana na kuwa tiifu kwa serikali ya kikoloni. Chini ya ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga uhusiano maalum kati yake na serikali pamoja na Mkristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni. Waislam wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya mtawala.

Mwafrika Mkristo akawa mnyeyekevu kwa serikali wakati wa ukoloni na baada ya kupatikana kwa uhuru akaja kushika madaraka ya serikali. Waislam wakatengwa na kuteswa katika ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hivyo kuwaondolea fursa ya maendeleo.

Kuwepo kwa Waislam kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislam wasimame kuutokomeza ukoloni. Baada ya uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na serikali, uliojengwa na tabia ya Kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa serikali ulilelewa vyema na umeisaidia sana Kanisa. Kanisa likaweza kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasiwasi.

Kutokana na uhusiano huu maalum Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu kutokana wa Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na serikali ya kikoloni kisha na serikali ya wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika uongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama katika Tanzania. Katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania.

Kiongozi vipi tena? siku hizi wanasema akili za mbayuwayu lazima uchanganye na zako. Ok ukristo uleletwa na ukoloni, je uislam uliletwa na nini? au uislam asili yake hapa hapa bongo? Mtu akisoma post yako na kama hajawahi kufika Tanzania atadhani waislam wamefungiwa kwenye "zoo" - hawana uhuru wa kufanya chochote. Kumbe rais rais ni muislam, makamu wa rais ni muislam, jaji mkuu ni muislam, IGP ni muislam, mkuu wa usalama ni muislam, the list is long.

Haya unaonekana kusema kuwa waislam ni wengi - good. Sasa kwanini wasitumuie huo wingi ni kijichanga ili wawekeze kwenye mambo ya kuinua maisha? Waislam hawana hospitali hata moja nchini, chuo kikuu ndicho hicho wamepewa mezani na bado kuendesha ni mtihani! Ukiachana na juhudi za mtu mmoja mmoja kama Mzee Mustafa Sabodo na wengine wa aina yake, sijawahi kusikia jumuiya ya kiislam inazidua mradi mkubwa wa kijamii i.e maji, umeme etc. Shida nini? Sensa?

Sujui kwenye Quran imeandikwaje lakini kwenye biblia imeandikwa hivi; "asiyefanya kazi na asile".
 
hizi propaganda za kijinga zitaisha lini? Umeongea kwamba kanisa lilisomesha watu wake sasa tatizo liko wapi? unataka mtu asiyesoma apewe uhasibu?

Maju,

Ungeweza sana kutoa fikra zako kunipinga bila ya kutumia neno "ujinga" hilo ni tusi.

Mimi si mjinga na hiyo haijapata kuwa sifa yangu.

Jenga hoja tujadiliane bila ya matusi kwani huu ni mjadala tu hatugombani.
Kwa ajili hii hapana haja ya mtu kumtukana mtu khasa kwa hii sifa tuliyojipa sie wenyewe, "The Great Thinkers."
 
maju huyo ndiye Mohamed Said, msomi anayedai kuwa kwa kiwango chake cha usomi ni wachache sana humu JF wangekuwa na ujasiri wa kusimama na yeye uso kwa uso. Tatizo linakuja pale anapojikuta uso kwa uso na hoja za kisomi kuhusu porojo zake za kichochezi zilizojikita katika udini na kutakiwa kuzijibu, huyooo...ghafla usomi wake huyeyuka na kubakiwa na sifa moja tu kuu ya uchochezi.

Bahati mbaya kwake JF si kama huko kwingineko anakoweza kuzipaka rangi porojo zake zionekane kama za kweli huku akipigiwa makofi na wachovu wenziye. Hapa mara nyingi badala ya kutoa somo anajikuta yeye ndio anaishia kupewa somo, kweli JF kiboko na kama mtu hukuangalia utaingia moto lakini ukatoka baridiii!

Hayo ndiyo humkuta huyu mchochezi kila anapojaribu kupandikiza hizo mbegu za fitina na chuki kupitia huu mtandao, hatupati ng'o! Masikini Mohamed Said, toka aanze akiwa kijana na hivi sasa anazeeka bila mafanikio yoyote katika njama zake hizo...maisha yake yote analoa jasho akiusukuma ukuta ambao hata hausogei! Pole!

Ningefanya mnakasha na wewe lakini umenivunja nguvu kwa hiyo lugha yako.
Jitulize, panga hoja kisha tujadiliane.

Ondoa lugha kali inaharibu utamu katika majadiliano.
 
Kiongozi vipi tena? siku hizi wanasema akili za mbayuwayu lazima uchanganye na zako. Ok ukristo uleletwa na ukoloni, je uislam uliletwa na nini? au uislam asili yake hapa hapa bongo? Mtu akisoma post yako na kama hajawahi kufika Tanzania atadhani waislam wamefungiwa kwenye "zoo" - hawana uhuru wa kufanya chochote. Kumbe rais rais ni muislam, makamu wa rais ni muislam, jaji mkuu ni muislam, IGP ni muislam, mkuu wa usalama ni muislam, the list is long.

Haya unaonekana kusema kuwa waislam ni wengi - good. Sasa kwanini wasitumuie huo wingi ni kijichanga ili wawekeze kwenye mambo ya kuinua maisha? Waislam hawana hospitali hata moja nchini, chuo kikuu ndicho hicho wamepewa mezani na bado kuendesha ni mtihani! Ukiachana na juhudi za mtu mmoja mmoja kama Mzee Mustafa Sabodo na wengine wa aina yake, sijawahi kusikia jumuiya ya kiislam inazidua mradi mkubwa wa kijamii i.e maji, umeme etc. Shida nini? Sensa?

Sujui kwenye Quran imeandikwaje lakini kwenye biblia imeandikwa hivi; "asiyefanya kazi na asile".

Umetaja majina.
Hayo ni machache sana katika uendeshaji wa nchi.
Inabidi uangalie ni watu wa dini gani wamehodhi fursa za utendaji wa kila siku na uadilifu wao katika kutoa haki sawa kwa jamii.

Ndiyo maana unaona Kanisa linapewa na serikali fedha nyingi kuendeleza miradi yake chini ya MoU kitu ambacho sisi Waislam hatuna. Sasa vipi mtu atusimange kwa kukosa msaada huo na kumtaja Sabodo.

Ama kuhusu kujipanga na kufanya mambo ya maendeleo Waislam hawana fursa na uhuru wa kufanya hivyo kama ndugu zao Wakristo kwa sababu serikali imepanga kuvunja bidii hizo.

Nadhani unakijua kisa cha Sheikh Hassan bin Amir (mmoja wa masheikh waliokuwa mstari wa mbele katika kimjenga Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika), mgogoro wa EAMWS na kuvunjwa kwake na Nyerere kwa shinikizo la Kanisa Katoliki ilipodhihiri kuwa wanajenga Chuo Kikuu. Hii ilikuwa mwaka 1968 ilipoundwa Bakwata ambayo Waislam wameikataa kwa kuwa haikuundwa na Waislam bali Nyerere.

Waislam tumefanya mengi katika hali hii ya kukandamizwa na Kanisa na Serikali yake.

Tumefanya juhudi za chinichini kupambana na serikali na kanisa hadi hapa tulipofika.
Hapa tulipo leo ni safari iliyotuchukua miaka 40.

Hakuna Muislam ambae hajui kuwa ipo dhulma.

Hii leo Bakwata haina watu wana ofisi na kushikilia mali za Waislam.
Nadhani unashuhudia harakati nyingi sana nchi nzima ambazo Bakwata wala hawatajwi.

Tumejenga shule nyingi pembezoni mwa kila msikiti nchi nzima kwa jasho letu wenyewe na juu ya hayo tunafanyiwa hujuma.
Hivi sasa tuna matatizo makubwa na NECTA kwa kuhujumu watoto wetu.

Serikali tumeifahamisha hilo kuwa hiyo NECTA ni mmoja wa mkono wa Kanisa.
Serikali iko kimya.

Majibu ya shida zetu zinatolewa na waumini wa Kikristo ndani ya JF.

Unaweza kuyapata hayo katika sehemu ya tatu ya kitabu changu, "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..."
Hayo yote ulosema majibu yake yamo humo.

Ukipenda naweza nikakuwekea sehemu yote ya tatu hapa jamvini ila nachelea ni ndefu mno singependa kuwachosha wasomaji.

Mimi sikusema kuwa Waislam ni wengi nimeeleza kwa kufanya rejea za wasomi wengine na kati ya hao wapo walosema Waislam ni wachache na Wakristo ni wengi.

Nakushukuru sana kwa mchango wako mzuri ambao umenifanya nami nihamasike kukujibu lau kwa muhtasari.
 
Unajua hawa wagalatia wanajijua wako wa chache ni ikifahamika hivyo kwa wakati huu itakula kwao hasa kwa wakati huu.Kwa hiyo wanachofanya wao ni kupinga tu hata kama wanajua ni muhimu kufanya hivyo
 
Kwako Mohamed Said, hivi kipengele cha dini kikiwekwa then matokeo ya sensa yakasema waislamu ni wengi kuliko wakristo, nini kitafuata?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom