njiwa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 13,259
- 7,108
wewe unafikiri kisipoingizwa waislamu mtapungukiwa nini?
Mengi sana...
wewe unafikiri kisipoingizwa waislamu mtapungukiwa nini?
Mengi sana...
Si kawaida yangu kuchangia nyuzi zenye chembe za udini lakini naiona hatari mbele yetu.
Nadhani Sheikh Ponda kuna vitu havielewi au anavipotosha
1. Tanzania haikujengwa na dini mbili, kwahiyo alipaswa pia kutueleza wale wasioamini au wale wenye imani tofauti na ukristo au Uislam wamewakilishwa kwa uwiano gani
2. Je uwepo wa watu wa dini moja kwa wingi unasaidiaje kubadili au kuboresha matokeo ya sensa
3. Hivi Ukiitwa John, William, Ahmad au Zuhura inatosha kuwa wewe ni muumini wa dini fulani. Ni wapi katika vitabu vya dini zote imeelezwa kuwa ili uwe mkristo au Mwislam wa kweli lazima uitwe Jonathan au Mohamed
Vipi kama ninaitwa John na wakati huo huo ni muumini mzuri wa dini za asili au nyingine, ina maana utukufu wangu mbele ya mwenyezi mungu una walakini. Ni kwa mantiki hiyo kigezo gani anatumia kupata asilimia 20?
Je mjumbe anayeitwa Gugumilo Kisaboko Njenga, Sheikh Ponda amemweka katika kundi gani la wajumbe wa tume
Kwa mwendo huu ipo siku Sheikh Ponda atahoji kwanini uwiano wa madaktari, wanasheria au Wahasibu usiwe 50/50.
Mimi nadhani ifike mahali watu wanaotaka kuligawa taifa kwa misingi ya kipuuzi kama hawa sasa wadhibitiwe.
Wadhibitiwe ili waseme ukweli kama dini zinavyoagiza na si kuchomeka hisia za kidini kila uchao.
Si kila mtu anaweza kufanya analysis na kupuuza, wapo wanaomwangalia Ponda kama Role Model
Kuna tatizo serikalini, viongozi wa dini zote siku hizi wameacha kazi za utumishi wa mwenyezi mungu na kujiingiza katika mambo yanayoleta mtafaruku katika jamii. Sina maana kuwa wasiseme la hasha! bali kauli zao sasa zinafanya mtu mwingine aziangalie dini kwa jicho la wasi wasi, narudia dini zote pengine ukiacha za jadi tusiowasikia
Hayo ya kila mtu kuangalia dini kwa jicho lake tuyaaache kila mtu ashughulikie lakini hili la utaifa tusilikalie kimya,hii ni mbegu hatari.
....sheikh ponda, na wengine wote wa aina yake, wanaojiona ni wateule wa kuwaongoza "kondoo" wa kiislam, pamoja na bakwata na taasisi zingine zote za aina hiyo za kiislam hawajawahi na hawatawahi kuwaunganisha waislam wa nchi hii kuwa kitu kimoja kwa mtindo wa kuwatenganisha waislam haohao ktk makundi..nina shaka kuna kitu kikubwa, na wao ni kivuli...hawaeleweki...lkn pia, nina shaka nyingine...dini imekuwa biashara inayolipa ( tumejifunza hili kutoka kwenye kauli za viongozi wetu wa dini zote)...na kuna maneno mitaani, kwamba, wakati mwingine serikali hukabiliana na upinzani wa mambo kwa mtindo wa "penye uzia..."...inawezekana (sina ushahidi ktk hili, ni hisia tu..ingawa ukipatikana ushahidi sintashangaa pia), kwamba sheikh ameona hilo na yuko kwenye "uwekezaji"..unategemea nini kwa sheikh na taasisi ambayo mpaka kesho imeshindwa kuwaunganisha waislam kukubaliana ktk kitu chepesi, na rahisi kama kutazama mwezi ulioandama ili "waumini" waanze, ama kufunga sawm ya mwezi wa ramadhan, au washeherekee kumalizika kwa mfungo wa ramadhani...! kuwaunganisha waislam wote kugomea sensa ya taifa au kushirika sensa ya taifa ni jambo gumu kama vile ilivyokuwa vigumu kwa kiwango cha takribani kushindikana, kuwavuta waumini kujaa misikitini alfajir kwa wingi kama inavyojaa kwenye sala za ijumaa....Mbona wote huyo sheikh Ponda na Mufti wana wasemea Waislamu. Kama kweli ni msimamo wa Waislamu wa Tanzania (na si taasisi tu) ni wapi walifanya survey yoyote ya kujua waislamu wanataka nini? Hamuwezi amui kitu kama taasisi halafu mdai ni msimamo wa waislamu. Je kama waislamu walio wengi wana pingana nao? Fanyeni utafiti wa nini Waislamu wanacho taka kisha toeni matokeo ya uchunguzi huo na mseme Waislamu asilimia fulani wana msimamo fulani. Otherwise waache kusingizia ni msimamo wa Waislamu wote na waseme ni ni msimamo wa taasisi zao binafsi.
nDIO HOJA ZENU ZA KILA. MNAOGOPA MKIJUA WAISLAM WAPO WENGI HALAFU NYINYI NDIO MLIOSHIKA NCHI YENYE UFISADI WA KUTISHA. HAMNA JENGINE MNALOOGOPA.
Hapa mimi ninavyoona ni kwamba, waislam kwenye jumuiya hizo ndiyo walitoa msimamo wao kuhusu sensa au kwa lugha nyepesi ni, huo si msimamo wa waislam wote Tanzania bali ni msimamo wa waislam wachache kwenye hizo jumuiya.Naona Mufti Simba amesahau kuwa kuna jumuia tofauti zinazo endesha mambo ya Kiislamu hapa Tanzania, pia kupitia jumuia hizi ndio ulipo tolewa msimamo wa waislamu juu ya sensa, sasa naona hivi sasa Simba anaona kama Bakata ndio kama chama tawala cha kiislamu, hivyo na penda kutoa rai yangu kwa Simba kwamba tumeshwa choshwa na serekali hii, pia tumesha choshwa na yale bakwata inayo fanyia waislamu.
Haiwezekani mufti Simba kutoa maamuzi mazito kama hayo bila kuhusisha jumuia nyingine. Nafikiri wakati umefika sasa kwa Bakwata kutazamwa kwa jicho la pili.
1. Je bakwata inafanya kazi za nani?
2.Je bakwata inawajibika kwa nani?
Haki ongezwi kitu hapa mkuu wenu kasha longa hoja hazina mantiki
Hawa watu sijui uwape nini ili waridhike!!!!
Waislam wajihesabu wenyewe, then idadi itakayopatikana ndo itakuwa idadi ya waislam hapa Tanganyika. na sisi tutakuwa na idadi yetu yaani wakristo na wapagani.
ndiyo mkaaamua kuunda vitaasisi viiingi ili muwe na umoja zaidi au?
uliona wapi kiongozi wa kiislam akachaguliwa na rais .. na sio waislam wenyewe.. simply mufti ni muwakilishi wa serikali ndani ya waislam ... niya yao moja tu! kutugawa na kupata total control ya waislam na tumestuka hilo kitamboo yaaani
nakuonea huruma!!!!!!!!kINACHOFURAHISHA ZAIDI HARAKATI ZA WAISLAM HAZIFANYWI NA MMUFTI WALA BAKWATA. UDINI WATZ WALIOIBUA SIO BAKWATA. SENSA NOOOOOOO. WATAFANYA WAKIRISTO NA WAPAGANI