Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Status
Not open for further replies.
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.

Je angepelekwa jela angevaa HIJABU????????? Hao BAKWANA na BASUTA ni MAGAMBA wa kiimani! wanapepelea mahakama ya KADHI!!!!!!!!!!!!

Ni hayo tu!!!!

Mimi nahisi busara hazikutumika pande zote.
BAKWATA hawakutumia busara kuhusisha tendo la mtu binafsi na chama. Picha zipo wazi. Mtu aliyemvua yule mama hijabu anajulkana, kama walikerwa na hilo wangelimshitaki muhusika kwa vyombo husika. Nasisitiza, aliyefanya lile tendo ni mtu binafsi hata kama anahusiana na chama.

Lakini ikiwa tunakubali kuwa chama ndio kilitenda yale, CDM itakuwa hawakutumia busara kwani walichukua hatua siyo. Kumvua hijabu, chupi au gauni hakutofanya CCM wawache kuchakachua. Ikiwa tendo alilofanya ni kosa la jinai, kwa nini wasimshitaki kwa vyombo vya sheria? Au tumefikia pahali imekuwa halali kujichukulia sheria mikononi mwetu? Hatuoni kwa kufanya hivi tunawahalalilishia pia wale wanaotia moto vibaka? Tukienda hivyo ikos siku nchi hii itakuwa haikaliki.

Ikiwa tunataka kujenga taifa lenye mfumo wa kidemokrasia, demokrasia hainipi uhuru wa kukupiga ikiwa umenipiga, bali sheria ndio hakimu. Kwa ufupi, BAKWATA na CDM walipaswa kufuata sheria

CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!

...acha hizo porojo zako mdugu yangu,ata mimi kiiman ni mwislam na ngependa nikupe ushauri wa bure,jaribu kupiga hatua moja mbele,tafakali mambo kwa kutumia akili alizokujaalia Mwenyezi Mugu, usikubali siku zote kukaririshwa mambo.Kama unakumbukumbu nzuri uko nyuma tuliambiwa CUF ni chama cha kidin,kwa-sababu tu CUF ya kipindi hicho ilikuwa na nguvu na mvuto wa kisiasa,leo Chadema iko ktk nafasi hiyo waliyokuwa nayo CUF ndo maana Chadema nao wapewa sifa hiyo mbaya ya kibaguzi.Kesho TLP nayo ikipata nguvu na kuwa na mvuto wa kisiasa bado nayo itapewa sifa hiyo hiyo mbaya ya ubaguzi,je utakuwa tayari kuendelea kuimba wimbo huo huo?,"badirika ndugu yangu"...hii nchi inaitaji kukombolewa na ukombozi wenyenye utafanikiwa kwa kushirikiana na si kwa-kubaguana kwa misingi ya dini zetu ilihali mateso ya maisha tunapata wote.Kama kuna mambo yatukwaza kiiman basi tukae na wenzetu tutakapokuwa tunajadiri katiba mpya tuwaeleze hili hatulitaki,hili liwe hivi,hili lirekebishwe nk.Lakin ukifuata hiza porojo za CCM utazidi kupotea,iwapi mahakama ya kadhi tuliyohadiwa ktk ilani ya uchaguzi ya CCM 2005?,yako wapi maisha bora? ...kaachin fikiri kwa kina utapata jibu...

Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.
Hapo kwenye red inadhihirisha sheikh Issa ni mtupu kichwani. DC anachaguliwa au anateuliwa? Hii tabia ya kutoa matamko kwa minajiri ya kuleta udini itawatafuna walioanzisha huu udini hapa Tanzania. Mfano mzuri ni picha hapa chini, Je tulipaswa kutoa tamko kama wakristo wote duniani au wanaume wote duniani kwa hichi kilichofanywa na polisi dhidi ya Lissu?? tundu lissu.jpg

Mimi nahisi busara hazikutumika pande zote.
BAKWATA hawakutumia busara kuhusisha tendo la mtu binafsi na chama. Picha zipo wazi. Mtu aliyemvua yule mama hijabu anajulkana, kama walikerwa na hilo wangelimshitaki muhusika kwa vyombo husika. Nasisitiza, aliyefanya lile tendo ni mtu binafsi hata kama anahusiana na chama.

Lakini ikiwa tunakubali kuwa chama ndio kilitenda yale, CDM itakuwa hawakutumia busara kwani walichukua hatua siyo. Kumvua hijabu, chupi au gauni hakutofanya CCM wawache kuchakachua. Ikiwa tendo alilofanya ni kosa la jinai, kwa nini wasimshitaki kwa vyombo vya sheria? Au tumefikia pahali imekuwa halali kujichukulia sheria mikononi mwetu? Hatuoni kwa kufanya hivi tunawahalalilishia pia wale wanaotia moto vibaka? Tukienda hivyo ikos siku nchi hii itakuwa haikaliki.

Ikiwa tunataka kujenga taifa lenye mfumo wa kidemokrasia, demokrasia hainipi uhuru wa kukupiga ikiwa umenipiga, bali sheria ndio hakimu. Kwa ufupi, BAKWATA na CDM walipaswa kufuata sheria
Mbona bakwata hawakutoa tamko dhidi ya tukio la yule mama wa CUF aliyefunuliwa hijab na maafande??

CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!

Dini imeingiaje humo ktk ugomvi wa DC na makamanda wa CDM? Kwani mkuu wa wilaya alikwenda msikitini pale kijijini? Acheni hizo tabia mtandio au hijabu inawakilisha mavazi na siyo dini,je mna uhakika gani huyo DC anaswali sana? Issue hapa ni kwann afanye kikao eneo ambako cdm walipaswa kufanya mkutano? Period.

kweli hapa hakuna great thinker hivi mtoa mada hajaweka source mmekubari kuingia ktk mjadala tena kwa matusi huo mtego

Mbunge wa CAF alikuwa Mwanamke alidhalilishwa kweli na Vyombo vya Usalama

1. Alipekuliwa na kuchekiwa na Polisi Mwanamme isivyopaswa na aliomba Mwanamke ampekue

2. Aliwekwa Rumande na Wanaume hata kubadili nguo ilikuwa shida

3. Alipigwa na kulazwa jela na wanaume kwa Wiki Moja

Kama ni upendo kwanini hawakukemea hali hiyo? Ina Maana hakudhalilishwa utu wake? au kwao yeye hafau sababu ni Mkristo?

Au ndio hiyo double standard ambayo nchi yetu chini ya CCM inataka kuibadilisha?

Kama hivyo vyombo vya kidini vanaanza kuangalia Mtu kwa udini ni dhambi hata kwa Mwenyezi Mungu...

Wanafikiri kwa kufanya hivyo mkuru atawafikiria kwenye mahakama ya kadhi, lakini nao ipo siku tu watajanjaruka na hao magamba wao wanaowabeba pasipokuwa makini, kama wewe ni muislamu halafu unategemea hawa watu wanaoitwa bakwata wakutetee pole sana, anza kujitetea mwenyewe kuanzia leo.

Nani apate pa kuanzia au unasema wao wapate pa kuanzia wamenyimwa mahakama ya kadhi sasa wanataka kumalizia hasira zao kwa CDM walie na muislam mwenzao aliyewanyima siyo CDM.

Asante mkuu kwa kumchana laivu bila chengachenga

Laiti kila mwanamke mwanasiasa angelalamika basi serikali isingekuwepo ......

makafari wanataka na waislam wavae kama anavyovaa huyo hawara wa slaa aliye zini mpaka akapata mtoto

Mimi nilisema jamani chama hichi ni hatari kwa uislam, wakipewa nchi hawa marufuku kuvaa hijabu, marufuku vipaza sauti misikitini, waislamu fungueni macho.
Kwa taarifa yako kama nikutoa matamko ya kipunguani na mimi natoa tamko kulaani vurugu zilizofanywa na DC yule na ningewataka BAKWATA na BASUTA kuomba radhi kwa wanachama wa CHADEMA kwa kosa la vurugu aliyofanya DC muislam.

hoja hapa ni kuvuliwa hijabu si kupigwa, Masheikh wana haki zote kulisemea hili la kuvuliwa hijabu kwa kuwa Fatuma ni mfuasi wa uislam

Nimepata njia ya kufanya uharifu, nitakuwa nikiwatumia wanawake waliovaa hijabu ili iwe ngumu kuwakamata kwasababu hijabu yaweza kuwavuka na itawakwaza waislam

kama somalia, waone kama hijabu inatakiwa.

hoja hapa ni kuvuliwa hijabu si kupigwa, Masheikh wana haki zote kulisemea hili la kuvuliwa hijabu kwa kuwa Fatuma ni mfuasi wa uislam
Okey kwa kuwa Fatuma ni muislam na amevamia mkutano(kaleta fujo), je CHADEMA wanapaswa kukemea tendo hilo la fujo ya fatuma na kuwataka BAKWATA na BASUTA kuomba radhi kwa wanachama wa CHADEMA kwa kosa lililofanywa na Bi. Fatuma coz ni muislam????

Hao mashehe wenyewe ni wizi lakini ukweli ni kuwa CDM inachukia Uislamu

Waislam hawaichukii CDM, (rafiki zangu wengi ni waislam), CDM haichukii waislam, ndo maana baadhi ya viongozi ni waislam.
Tatizo, CCM inatumia udhaifu wa waislam kuona kuwa kukandamizwa kwa waislam ni matokeo ya CDM, bila kujali kuwa CDM haijawahi shika dola.\
Waislam waseme ni nani aliwanyang'anya shule zao, CCM au CDM?
Waislam acheni kutumiwa. Wakataeni masheikh ambao wanapewa muongozo wa kuongea na CCM, kwani pamoja na kujipendekeza kwenu, nothing is done.

Si walisema wanaandama vp wameishia wap hao mashehe ubwabwa? waache kudilili na mahakama ya kadhi walioongopewa na ccm wanadakia mada ziszowahusu, na siku wakiandama naungana na kova kuwavunja mguu

Kova hawezi kuwapiga waumini wenzake hata cku moja chini ya serikali iliyo chini ya waumini wenzake fullstop.

Ndugu zangu Waislaam sijui ni lini wataacha kutumiwa vibaya na ccm. Swala la DC Kimario ni la kisiasa na si kidini na ikumbukwe Fatuma hakuvuliwa hijabu bali mtandio.Ccm wamekuwa mara nyingi wakiitumia misikiti kupandikiza chuki dhidi ya vyama vya upinzania hususan CDM.Kwanini Masheikh ambao ninaamini wameiva kiimani, wanatumiwa na ccm na bila uchambuzi wanakurupuka na kuongea bila tafakuri.Kwanini Waisilamu wamekuwa ni watu wakulalamika kwa mambo madogomadogo hata yasiyohusu imani yao? Kwanini Waisilamu wamekuwa wakidai wanaonewa kila uchao? Tatizo ni nini hapa? Sitaki kuamini kwamba Waislamu si waelewa,hapana, ni waelewa sana na watu wasomi tatizo viongozi wao wanakubali kuwa vibaraka wa ccm.Ndugu zangu Waislamu kueni macho sana na ccm itawafikisha kusiko.

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom