Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Status
Not open for further replies.
Hawa masheikh nao wamedanganywa mahakama ya kadhi badala walaani kikwete kuachinjia mbali mahamakama ya kadhi sasa wanaingilia mambo mengine,tutawaona kikwete atapowapiga mabomu pindi watakapo andamana kudai kadhi
 
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea!

Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha.

Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!
 
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.
Waambieni waandamane maana la Kadhi limekuwa zito mno kwao.
 
Si walisema wanaandama vp wameishia wap hao mashehe ubwabwa? waache kudilili na mahakama ya kadhi walioongopewa na ccm wanadakia mada ziszowahusu, na siku wakiandama naungana na kova kuwavunja mguu
 
Jamani, mfahamu ya kwamba hawa bakwata si wawakilishi wa waislamu Period! Pia mtambue kwamba, waislamu makini walishawatenga zamani. Waliokuwepo ni waganga njaa fulani hivi wanaotumiwa kwenye mambo kama haya!

Namna ya kupata nafasi za viongozi katika BAKWATA ni sawa na uchaguzi wa NEC ya CCM. Uchaguzi wake hufanyika Dodoma, mfadhiri ni ccm, ukumbi wa ccm, kampeni kama za ccm na kila kitu!
 
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!
Nani awaombe radhi pelekeni huko eti mtatangaza mgogoro mkubwa mtangaze mara ngapi, ulitaka aachwe afanye uhalifu kwa vile kavaa hijabu ni uislam gani unafundisha kuchakachua, mhalifu ni mhalifu hata kama kavaa hijabu tena wavaa hijabu ndio wezi wakubwa wa waume za watu. Tumechoka kuwalea andamaneni muone kuna vijana kule Moshi hawafanya mazoezi kwa vitendo kama hamjaacha kandambili barabarani na kanzu zenu.
 
Mimi nilijua tu ya kwamba CCM wamezungumzia Hijabu kwa maana maalum. Na nilijua kwa uhakika waislaam watakuja hapa na kupiga makelele kuhusiana na mwanamke kuvuliwa Hijab lakini bila weledi wa maudhui ya uvaaji wa Hijab. Sababu sii kuvuliwa Hijab kwa sababu hata unapokwenbda kupiga picha ya passport mwanamke hulazimika kuivua Hijab..

Tukio hilo halikutoa kwa kwa sababu ya imani, sera au ilani ya chama kupinga uvaaji wa Hijabu. Hii inadhihirisha wazi CCM wanatafuta siasa za majitaka na hao masheikh wa BAKWATA na BASUTA ni maamuma wanaotumiwa na CCM pasipo kufikiria kwanza..

Kinachokatazwa kisheria ni kukataza wananwake wasivae Hijabu, na Chadema hawana tatizo na Hijab wala haki ya wananwake kuvaa hijab isipokuwa hijab ilimtoka kama vile viatu vilivyotoka...na mbona msizungumzie viatu vyake!
 
Hawa watu bwana, wanaacha mambo ya msingi yanayowagusa waislamu wote i.e kadhi wanang'ang'ana na DC. By the way, wanaanza lini kutumia haki yao ya kikatiba kuandamana mpaka kieleweke?
 
Kama mtandio unaitwa hijabu basi hijabu haina maana.

Asojua maana, haambiwi maana, nyie pambaneni na waislamu mmewatafuta siku nyingi nadhani hapa mtapata pa kuanzia
 
Mm ni muislamu kwanza na-declare interest lakini siungi mkono kitendo cha hawa wanaojiona viongozi wa dini yetu kuwa wanatoa matamko ya kipuuuzi km haya, Chadema ni ya waislam na wakristo i.e watanzania.

Dini hairuhusu muislam kufanya vikao vya uhalifu (wizi) kisa eti kavaa hijabu. Ina maana leo sheikh mkuu akimbaka mtoto wa miaka tisa akiwa kavaa kanzu na kibaraghashia tutaacha kumshika? DC kwanza hajavuliwa hijabu hawa viongozi wetu wanatumiwa na wanasiasa mafisadi kiasi cha kufanya cc waumini wao kuwadharau.
 
Mbunge wa CAF alikuwa Mwanamke alidhalilishwa kweli na Vyombo vya Usalama
1. Alipekuliwa na kuchekiwa na Polisi Mwanamme isivyopaswa na aliomba Mwanamke ampekue
2. Aliwekwa Rumande na Wanaume hata kubadili nguo ilikuwa shida
3. Alipigwa na kulazwa jela na wanaume kwa Wiki Moja

Kama ni upendo kwanini hawakukemea hali hiyo? Ina Maana hakudhalilishwa utu wake? au kwao yeye hafau sababu ni Mkristo?
Au ndio hiyo double standard ambayo nchi yetu chini ya CCM inataka kuibadilisha?

Kama hivyo vyombo vya kidini vanaanza kuangalia Mtu kwa udini ni dhambi hata kwa Mwenyezi Mungu...
 
Hawana ubavu ndugu zangu hao,kwani ilani mbili zote za CCM zimewapiga chang la macho pamoja na kujidai jihadi wajaribu waone msanii wa ubongo wa fleva atakavyowakata miguu,wantishia tu wao kwa wao wanafanyiana unafiki, kiukweli waislamu pamoja na dharau mbaya ya kuongopewa na CCM hawana ubavu wa kuidai haki yao ya mahakama ya kadhi kama wanavyojiongopea kuwa ni haki yao ya msingi kupitia imani yao.

Na mshikaji kishawachana laivu,wajaribu basi kubisha waone. Sasa kuingiza hoja ya hijabu wakati bibi yule aliidondosha mwenyewe kwa wasiwasi wake inatoka wapi jamani? Jipangane mudai mahakama ya kadhi wala si kuingilia mambo ya siasa.
 
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam.

Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana.

Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!

Kuwa kama mtu mwenye akiri timamu na unaejua maadili ya uislam kwa mwanamke katika kujihifadhi. Usikurupuke kochochea mambo ya udini kipuuzi.
 
Mm ni muislamu kwanza na-declare interest lakini siungi mkono kitendo cha hawa wanaojiona viongozi wa dini yetu kuwa wanatoa matamko ya kipuuuzi km haya, Chadema ni ya waislam na wakristo i.e watanzania. Dini hairuhusu muislam kufanya vikao vya uhalifu (wizi) kisa eti kavaa hijabu. Ina maana leo sheikh mkuu akimbaka mtoto wa miaka tisa akiwa kavaa kanzu na kibaraghashia tutaacha kumshika? DC kwanza hajavuliwa hijabu hawa viongozi wetu wanatumiwa na wanasiasa mafisadi kiasi cha kufanya cc waumini wao kuwadharau.

Niambie tofauti kati ya Kanzu na Hijab, muislamu?
 
Next time tuna mvua chupi. Mbona ohio mademu wanajiuza huku wamevaa baibui. Bakwata mmefuria,jipangeni upya ndomana mmetumika kueneza propaganda ya udini na ccm wakati wa uchaguzi 2010.
 
Bornvilla said:
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!

Bornvilla,

..haya ni masuala ya kisiasa, na ni vizuri kuacha kuingiza dini humo.

..Waislamu wasiingie kwenye mtego wa kumtetea huyu mama ambaye bila shaka alikuwa akishiriki ktk uhalifu wa kisiasa.

..wako wenye kustahili utetezi wa Waislamu lakini siyo huyu mama.
 
Asojua maana, haambiwi maana, nyie pambaneni na waislamu mmewatafuta siku nyingi nadhani hapa mtapata pa kuanzia
Nani apate pa kuanzia au unasema wao wapate pa kuanzia wamenyimwa mahakama ya kadhi sasa wanataka kumalizia hasira zao kwa CDM walie na muislam mwenzao aliyewanyima siyo CDM.
 
Wadau tuwekeeni picha za huyu mama huko nyuma kama alikuwa anavaa hijabu ama lah! Pia niliona ile picha aliyokuwa kwenye magazeti, ile si hijab iliyokuwa kwenye mafundisho ya kur'an.

Hao viongozi wamebebeshwa zigo na wao wamelibeba kama lilivyo, wasijue ndani kuna nini!
Nasikitika wanavyokishushia hadhi chombo hicho muhimu cha waislamu
 
Sidhani hii kama ni kweli,kama kweli imetoka Bakwata basi hawa jamaa hawajui wanalofanya,juzi Mwenyekiti wa chama hichi kawatoa nishai tena kwenye hafla ya Idd leo wanakitetea ? kama DC alikosewa suala liko mahakamani na litashughulikiwa huko,Bakwata wala mtu mwingine haruhusiwi kuliongelea kwa sasa.
 
Mbona hawakusema chochote wakati yule Mbunge wa CUF mwanamke aliyedhalilishwa zaidi ya kuondolewa hijab Bakwata hawakusema chochote?

Au ndio Ubaguzi umeshaanza Mwanamke akiwa hana jina la kiislamu it is ok kwa yeye kunyanyasika?

Is this a double standard?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom