Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Status
Not open for further replies.
Ivi kweeli tofauti ya hijab na mtandio ni nini? Okay hata kama kuna tofauti ivi ukimkamata mto mwenye makosa na akiwa amevaa hijabu, kanzu, bagalashia, au kola ya kiaskofu ndo umwache.?
Mi nazan tufike mahali tujue hakuna mtu aliye juu ya sheria ktk nchi hii. Kama wabunge haswa wa upinzani wanavyonyanyaswa mara kwa mara bila kujali hadhi yao ya ubunge( uwakilishi wa wananchi) iweje leo mteule tu wa rais anakamatwa kwa kuhusika ktk kuvuruga uchaguzi anatetewa kwa kisingizio cha mavazi ya kidini.

Tunakoelekea itafika mahali hata jambazi akikamatwa kavaa tasbihi au rozari basi watu mtataka kuandamana
hiyo roho ya udini na ishindwe ktk nchi hii. Na hao watu wanao ikuza na walegee kabisa.amen

Mimi nilisema jamani chama hichi ni hatari kwa uislam, wakipewa nchi hawa marufuku kuvaa hijabu, marufuku vipaza sauti misikitini, waislamu fungueni macho.

Ivi kweeli tofauti ya hijab na mtandio ni nini? Okay hata kama kuna tofauti ivi ukimkamata mto mwenye makosa na akiwa amevaa hijabu, kanzu, bagalashia, au kola ya kiaskofu ndo umwache.?
Mi nazan tufike mahali tujue hakuna mtu aliye juu ya sheria ktk nchi hii. Kama wabunge haswa wa upinzani wanavyonyanyaswa mara kwa mara bila kujali hadhi yao ya ubunge( uwakilishi wa wananchi) iweje leo mteule tu wa rais anakamatwa kwa kuhusika ktk kuvuruga uchaguzi anatetewa kwa kisingizio cha mavazi ya kidini.

Tunakoelekea itafika mahali hata jambazi akikamatwa kavaa tasbihi au rozari basi watu mtataka kuandamana
hiyo roho ya udini na ishindwe ktk nchi hii. Na hao watu wanao ikuza na walegee kabisa.amen

Na huo ndio upuuzi ambao wanataka kutulazimisha tuukubali...Ningewaona watu wa maana sana na weledi wa dini zao kama wangekuwa mstari wa mbele kupinga maovu!! Ila kama wanatetea maovu kwa kisingizio cha dini, sitakosea kuwaita agents of evils!

Mimi nilisema jamani chama hichi ni hatari kwa uislam, wakipewa nchi hawa marufuku kuvaa hijabu, marufuku vipaza sauti misikitini, waislamu fungueni macho.

Kweli mkuu??? Unatumia busara kuyasema haya au kuna inducement behind????

kuna kazi kubwa sana ya kuuelimisha huu UMMA wa kizazi cha mtoto wa kijakazi.

Kaka hivi unadhani hawaelewi? Wanaelewa vizuri sana ila tatizo ni hizo ajenda nyingine walizo nazo. Kwanza, za kisiasa ili pili kwa siasa waweze kufikia ajenda nyingine ya kidini. Hata hizo chokochoko zisizo na mbele wala nyuma ni kujaribu kulipeleka taifa huko.

Siamini na wala huwezi kunishawishi niamini watu aina ya viongozi wao wanaotoa hayo matamko, n.k. hawaelewi harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendelea nchini na duniani kote na ukweli ni upi na uongo ni upi bali WAMEKUBALI KUTUMIKA hata ikiwezekana kwa kuusimamia uongo kwa faida ya dini yao na makundi yao badala ya taifa.

Kwao kila kitu kinatazamwa kwa jicho la dini kwanza hata kama ni kiovu! UFISADI kwao hauna tatizo as long as umetendwa na mtu wao na pengine umekuwa na "faida" fulani kwa dini yao! Bora hata wangenyamaza lakini wanaposimama hadharani kutetea inaleta shida zaidi. Kumbuka walivyomtetea Osama kisa ni dini yao bila kujali uovu alioutenda; walivyomtetea Idd Amin kisa ni dini yao bila kujali aliyoyatenda; walivyoitetea Taliban bila kujali waliyoyatenda; wanavyojaribu kila siku kumtetea kiongozi yeyote nchini bila kujali kasoro zake alimradi ni wa dini yao; na hivi sasa wanavyomtetea DC bila kujali alichokuwa anakifanya nyuma ya pazia alimradi ni mwenzao. Na chama fulani (kama viwili hivi) kwa kujua "udhaifu huu wa kujitakia" wameamua kuutumia ipasavyo kwa malengo yao japo ni ya kitambo tu.

Siamini kama kimsingi dini yenyewe iko au inaelekeza hivyo; badala yake inasimama katika haki daima bila kujali mwenye kustahili au kukosa haki hiyo ni nani - awe wa dini husika au "kafir". Inapotokea viongozi wakuu wa dini kama hawa kutohukumu kwa haki kwa kuwa tu itapingana na matakwa ya mitazamo au dhamiri zao (of course mbaya) au itikadi zao basi taifa liko katika wakati mgumu sana.

Inaonekana watu wengi wanazungumzia suala hili bila upeo wa kina juu ya uislam na misingi yake.Ujue uislam ndio uchangie mada kama hizi sio kukurupuka ......Huu sio ushabiki wa ccm na chadema......Kuheshimu imani ya mwingine ni kuheshimu na kuujali utu wako.

na sisi wakristo tunaipa bakwata na basuta siku saba watuombe radhi kwa kushindwa kuwadhibiti waumini wao walijazana jela za tanzania kwa uhalifu wao na viongozi wa dini kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuwaelekeza nini cha kufanya.

na polisi wawaombe waislamu kwa kukamata vibaka wa kiislam kwa sababu wanadhalilisha dini ya kiislam.
kikwete awaombe radhi waislam kwa kuudhalilisha uislamu kwa kuahidi kitu ambacho hakitekelezeki.
ccm iombe radhi kwa kuudhalilisha uislamu kwa kumuita rostam gamba.

mpaka hapo nadhani waislam watakuwa wametendewa haki na kutenda haki.

umenena vyema sana Mpwa lakini tuwe wawazi na wakweli, hivi wale wote pale waliomkamata ni wakristo tu hapakuwa na muislamu pale (hata kwa jina lake tu) ? Ni kweli pale kulikua na "vita" dhidi ya uislamu? kwanini kila kitu tunakihusisha na uislamu(kuonewa)? yaani hautuwezi kufikiri nje ya uislamu? hivi kuwa muislamu ni kuwa mlalamishi hata kwa mambo ya kawaida kabisa? hebu sema ukweli toka moyoni mwako, lile ni hijabu au ni mtandio? je kitendo cha mama yule kuvunja sheria halali za uchaguzi? mbona hatukuangalia hapo? au ytuseme ailikamatiwa Msikitini? hapana tunajidhalilisha kwa kuwa na mawazo mgando au tuseme sasa kuwa nyie wenzetu na ndugu zetu ndio mnaopandikiza hizo chuki za dini maana kama mtu amabye ninahisi una uelewa mpana wa mambo unatoa hoja za namna hii itakuaje kwa wale ndugu zetu kule wasio na elimu na ambao wanatuchukulia sisi (mimi, wewe na wengine) kuwa ndo wenye majibu sahihi kwa hoja kama hizi? je wanetu wajifunze nini toka kwetu? warithi chuki? hapana, tuanze kuwaza kwa upya, na uwe na siku njema Mpwa
A very sensible and timely caution lakini ni watu wachache sana watakaoisoma hii contribution yako kwa umakini unaohitajika. Watu hapa wamejikita katika jazba na chuki zao dhidi ya chama hiki au kile, imani hii au ile. Lakini wahenga husema, samaki ndani ya maji hajui umuhimu wa maji. Wimbi la ukombozi likimtoa ufukweni na kumrejesha baharini ndipo anapotambua kwamba uhai wake bila maji si chochote. Lakini humu ndani hii thread yako itaishia kubezwa na kutukanwa, na utakuwa na bahati kama hutaambiwa kwamba hujasoma, mnywa kahawa, mvaa msuli, mtu wa madrasa n.k. Tena wengine wanaosema hivyo elimu zao ni duni kuliko wale wanaowakosoa. Pathetic!

Tuacheni siasa za kidini, na ukabila.
Masuala ya kuhusianisha CDM + Uikristo V/s CCM + Uislamu hayatatusaidia,
Inajulikana fika kua adui wa maendeleo ya Tanzania na Watanzania ni CCM + wanaoi-support, udini unatoka wapi?
Mwishowe tutasahau adui yetu ni nani kisha tuanze kugeuzana maadui wenyewe kwa wenyewe tukimuacha kubwa la maadui anapeta tu!!!

aaaahhh nilikua sijaangalia ID yako, kutokana na id yako uko sahihi
Mimi nilisema jamani chama hichi ni hatari kwa uislam, wakipewa nchi hawa marufuku kuvaa hijabu, marufuku vipaza sauti misikitini, waislamu fungueni macho.

Masuala ya kisiasa tuyaache yatatuliwe kisiasa na maswala ya kidini yaachwe yamalizwe kidini.Masuala ya kuunganisha masuala ya siasa na dini mtazidi kutuharibia nchi.Hata mahakama ya kadhi mnataka kuifanya issue ya kisiasa wakati ni issue ya kiibada zaidi(waislamu na mambo yao).Hizo ni dalili za kufirisika kifkra!hakuna lolote na mtazikwa hivohivo na lawama zenu baada ya kujilipua mabomu hali makundi mengine ya dini yanazidi kusonga mbele na kustawi na kuwaletea waumini wao na watanzania kwa ujumla maendeleo ya kimwili na kiroho

mtu akishakuwa kafiri hata kwenye ukweli yeye anaona kaonewa tatizo watu wengi wanajibu kwa ushabiki na haiwezekani hata siku moja ukaleta hoja inayohusu waislam ukaacha kutukanwa au jf ni ya makafiri

kwa kuwa ni muislamu aachwe afanye uhalifu, hawa masheikh watuambie ni lini uislamu umeanza kuruhusu mipango ya wizi wa kura.

kwa kuwa ni muislamu aachwe afanye uhalifu, hawa masheikh watuambie ni lini uislamu umeanza kuruhusu mipango ya wizi wa kura.
Hao mashehe wenyewe ni wizi lakini ukweli ni kuwa CDM inachukia Uislamu

Huu ni uzalilishaji usiovumilika!

Chadema hawana heshima kabisa

Naungana na wewe CDM hawana heshima kabisa,ila CCM ndio wanaeshima za kuhongwa suti na waarabu,kutukana viongozi wa vyama vingine ni heshima kubwa sana kwako.

Baada ya wewe kusema maneno haya yaliyo jaa busara na hekima basi mie sitasema lolote bali nitasoma wengine wanasemaje .I wish tungalikuwa waislam wengi kama wewe wenye kuona ukweli .

Ndugu yangu sasa inatupasa tujipange kutengeneza chama huru cha waislam chenye fikra chanya na sio hiki kinachotumiwa na wanasiasa kwa ajili ya matakwa yao bila ajali aibu wanayoitengenezea dini yetu tukufu.

Mkuu hatetewi mama ila suala la kumvua hijab/mtandio ambao unaambatana na imani ya dini yake ndilo suala hapa. Hao masheikh hawajaingilia siasa wamesema kuhusu vazi. Mambo haya huanza taratibu na kisha huwa makubwa na mara nyingine hupigwa fwatwa. Kumbukeni yaliyompata Mrema.
tusitishane kwa ujinga

Achana na Copy and paste wote tunajua, tuambie jibu fupi, Kiongozi wa Pagan hapa Tanzania ni nani na Ibada zao wanafanyia wapi ni hayo tu

Ungeelewa maana ya hilo neno pagan swali lako lisingekaa lilivyokaa!

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom