Sawa upo huru,
1) uliupataje UHURU HUO baada ya kufuatilia mambo yao, huwa hawakuachii hivi hivi?
2) Kawaida yao hao ukigusa mambo yao wanajua kwenye ving'amuzi vyao na waweza kukushambulia umejizatiti vipi au kwa nini wewe hawakufuati? vinginevyo wanafaidika na mada zako
3) Kama una kinga ni ipi hiyo ambayo yaweza kuwa msaada kwa wengine?
Naomba nifafanulie maswali hayo hapo juu ili hata TUNAOkuhisi kivingine tukuelewe mana katika MADA ZAKO HUWA UNATOA KAFUNUNU flani ka KICHAWI.
Tukilejea kwenye mada ya uzi huu, maoni yangu ni kuwa kwenye maji wachawi husafiri pia kama ulivyosema mwenyewe kuwa kuna njia za kwenda kuzimu. Wakitaka kufika huko watatumia nini, lazima wapiti kwenye maji. Nchi kavu wanaanguka sana na ungo wanapopita sehemu zenye walokole mana nguvu za kichawi kwa walokole hazifui dafu. Baharini kama akipaa na ungo anakwenda tu. Mchawi hawezi kumwangusha mchawi mwenzake, kwani Marekani na ulaya wanafikaje, si lazima wavuke maji!!