Baharini kuna MASHETANI na MIZIMU mikubwa tena ogopa sana visiwa vidogodogo ambavyo watu hawaishi, aiseeh! umenikumbusha mkasa mmoja ulio nipata mimi na wenzangu sita tulipotea baharini muda wa siku tano,
tuliondoka na MASHUA inayo tumia upepo kutoka kijiji cha KIGOMBE tukielekea MKOKOTONI ZANZIBAR amini tupo mkondo mkubwa wa bahari upepo ukakata siku nne nzima hakuna upepo hata kidogo MASHUA ikakokotwa na maji tukapotea ajabu ni kwamba ukiona chombo kingine cha upepo ukikifuata kinapotea huu mkasa ni mrefu nikipata nafasi nitakuja elezea kwa kina.