Kisa kilitokea UK(ukerewe)wamefika katikati ya ziwa bimkubwa mmoja anawaambia jamani nimefika watu wa kachanganyikiwa ikabidi washushe nanga na kuanza kushusha mzigo wake tuweke wapi?anawaambia tupeni tu hapa mzigo ulipoisha jamaa wakaondoka zao.Haya mambo kama hadithi but yanatokea kwenye ulimwengu huu.
Kaka haya mambo yapo, yapo sana tu.
Watu wanamuona Mshana jr mzushi, lakini ukikaa na waliofanya kazi ya uvuvi kwa miaka mingi huwa wanatoa story mambo wanayokumbana nayo Baharini mpaka unaweza kuona Kama hadithi vile.
Kwa mfano; kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1990 au kati kati ya 1990 kuja 2000,niliwahi kusoma Kwenye gazeti la Majira Mwandishi alieponea chupu chupu pamoja na wengine kufa kwenye Meli ya uvuvi.
Mwandishi anasema Safari yao ilianzia Mafia, lakini siku hiyo ilikuwa sio siku ya uvuvi, Samaki walikuwa nao Tayari kwenye Meli, washamaliza kuvua wanarudi Dsm.
Mle ndani ya Meli kulikuwa na wachina 2 ambao ndio walikuwa wamiliki, na wafanyakazi wa ki-TZ idadi yao sikumbuki.
Mwandishi anasema Safari ilienda vizuri tu, kuna sehemu walifika wale wafanyakazi wakamwambia (Mwandishi) ile sehemu ina kina kirefu sana cha maji na ni eneo lenye Samaki wengi lakini ni kipande chenye mauza uza sana.
Kwa mujibu wa Mwandishi muda huo wanapita eneo hilo ilikuwa jioni kabisa.
Ghafla wakaona kiwingu, yaani maji yalikuwa yamefunikwa na ukungu dk chache baadae Mwandishi anasema zikaja dhoruba za kutisha, dk chache baadae ule ukungu ukatoweka.
Ile sehemu ambayo kulikuwa kumefunikwa na ukungu, ulipotoweka wakawa wanaiona Meli Inazama Mwandishi hakujua Kama ya uvuvi au vipi.
Baadae hali ilipokuwa mbaya mmoja ya wale wachina alikuwa kavaa mkufu, akauvua akautupa Baharini, kwenye Meli mle kulikuwa na Mbuzi, akaenda akachukua mmoja akamtupa Baharini pia, halafu akarudi ndani ya Meli, baada ya yule mchina kufanya vile dhoruba ikaanza kupungua nguvu taratibu, na ile Meli waliyokuwa wakiiona ikizama ikapotea Machoni mwao.
Mwandishi nakumbuka alisema lilikuwa tukio la kutisha ambalo kifo kilikuwa nje nje.
Mpaka leo nikijumlisha matukio ya baadhi niliyokuwa nahadithiwa na wazee wavuvi, na lile la yule Mwandishi, nikisikia kuhusu mauza uza ya Baharini huwa sipingi.