Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,303
- 12,852
Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.
Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.
Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.
Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.
Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.