KERO Mashirika ya kigeni yanayojiita Humanitarian au International NGO's na kasumba za ubaguzi kwa waajiriwa wazawa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mashplayer

Member
Oct 25, 2011
15
21
Habari za Asubui wana JF,

Naomba kuleta mada kwenu kuhusu haya mashirika ya kigeni yanayojiita ya kusaidia binadamu (humanitarian) au kujiita mashirika ya kimataifa yasiokuwa ya kiserikali (INGO). kwa mfano; Medecins sans frontieres, Medecins du monde na mengine mengi.

Kwanza kabisa mimi ni mwajiriwa wa moja ya haya mashirika na kilichonileta huku ilikuwa sio mshahara au maslahi mazuri bali ukosefu wa ajira wa muda mrefu na kukaa sana mtaani bila kazi maalum.

Nilipata shavu kwenye hizi shirika za kigeni humanitarian, lakini nilichokutana nacho huku nafikiri sijawahi kutana nacho toka nimeanza kufanya kazi kwenye mashirika binafsi.

Kwanza kabisa ogopa shirika lenye chimbuko au kutokea uswisi au ufaransa, hawa jamaa ni wabaguzi sijawai kuona. Pili, viwango vyao vya mishahara ni vibovu sana na hata mazingira ya kazi kwa wazawa ni magumu sana. Kuna muda unajikuta upo kama mtumwa ndani ya nchi yako kwa sababu tu hauwezi kuacha kazi mana mtaani ni pagumu sana na kazi hakuna. na haya mashirika wanatumia kigezo hiko kama fimbo ya kuchapia wazawa.

Pia, wanatumia sana loop holes za sheria zetu za tanzania ili kutukandamiza, kwa mfano, kuna kitu kinaitwa internal regulations, hzi ni sheria za kikandamizi ambazo zimetungwa kulingana na sheria ya ajira ya Tanzania lakini wametumia mianya ya sheria hiyo ili kuwabana national staff.

Tukirudi kwenye mishahara, mtu anaitwa officer mshahara unaanzia laki 8 take home na hata kama ulitoka sehemu unalipwa zaidi watakuambia wao salary grid yao ipo fixed na hakuna makubaliano yoyote au negotiations zozote.

Hata ufanye kazi kama punda siku saba za wiki hakuna promotions au bonus yoyote, na hata ikitokea kuna nafasi zimetangazwa ambazo ni za level ya juu yako, itakubidi uiombe kama mtu alie nje ya shirika na ufanye interview na asilimia kubwa wanazikosa hizo nafasi.

Mwisho wa siku unajikuta unaletewa supervisor na utamfundisha kazi. na lengo kuu la wao kufanya hivi ni kwasababu wanataka watu wapya kutoka nje ya shirika wasiojua mienendo ya shirika. na mara nyingi wale wasiokuwa na uvumilivu huwa wanaacha kazi baada ya muda mfupi wa kuajiriwa.

Serikali yetu imelala wakati vijana wao wananyanyaswa kwenye nchi yao na wageni. mashirika haya pia ya sheria au policy inayosema mzawa au national staff kwenye field level hawezi kufika level ya manager bali ataishia level ya supervisor kushuka chini.

Mpaka muda huu toka nimeanza kazi, kuna watu kama nane wameacha kazi au kufukuzwa kwa makosa ya kipumbavu.

Sasa naendelea kujiuliza kwanini nafasi za juu za mashirika haya bado zimeshikiliwa na foreigners ambao hata sheria za tanzania hawazijui? hauwezi ukaleta HR manager kutoka vietnam au mexico au kenya ambae hajui sheria za nchi au project coordinator kutoka kenya, pakistan au nigeria wakati wapo watanzania wenye sifa na vigezo zaidi ya hao wanaokuja kushika hizo nafasi.

Kwa mfano, wana tabia ya kutangaza nafasi lakini lengo kuu ni kucheza na sheria za nchi wakati wanajua kabisa wazawa watakaoomba hizo nafasi hakuna atakaepewa kwasababu wanataka kutengeneza hoja au mazingira kuwa hakuna mwenye vigezo ili walete watu wao wabaguzi kuja kushika hizo nafasi.
Mfano: HOM ni mkenya na DHOM alikuwa ni mkenya pia,lakini amemaliz muda wake ameondoka na nafasi wameitangaza lakini nina uhakika hiyo nafasi haitopata mtu na ataletwa raia wa kigeni kushika hiyo nafasi.

Kama kuna mhusika yoyote wa uhamiaji, wizara ya afya au serikali kuu ambae yumo humu tafadhali sana tunaomba muwachunguze hawa masharika kabla ya kuwaruhusu kufanya kazi ndani ya nchi yetu.

Vijana wa kitanzania wanateseka na kunyanyasika ndani ya nchi yao kwa kigezo tu cha kutokuwa na ajira.

Naomba kuwasilisha!

Mkereketwa Mzawa anaefanya kazi MSF
 
Ndivyo yalivyo hayo Mashirika,lipo lingine linajiita GOOD NEIGHBORS ni la Kikorea,nalo ni Shirika la kihuni linajifanya linahamasisha miradi ya maendeleo vijijini lakini kiuhalisia linahamisha USHOGA. Wananchi hupewa sharti kwamba wajaze fomu wakikiri kwamba ni washiriki wa mapenzi ya jinsia moja ili waletewe misaada kama zana za kilimo nk.

Ukitaka udumu kwenye hilo Shirika ni ujipendekeze sana kwa kimama fulani ki-Country Director(Kikorea)na kidada fulani ki-Head of HR kinaitwa Helena. Yaani ni Umbea na Majungu tu kwenye hili Shirika,wao kufuata Sheria za Nchi ni kwa kinyumenyume.

Na hawakomi,miaka minne iliyopita aliyewahi kuwa Mkuu wao hapa Tanzania alifukuzwa nchini na Serikali kwa makosa mbalinbali ya kunyanyasa wazawa lakini hata aliyekuja mambo ni yaleyale na Serikali inashindwa kuchukua hatua.

Nilifanya kazi mwaka mmoja na hili Shirika, kazi ya kuhamasisha USHOGA ilinishinda nikaamua kuacha kazi
 
Duuuuh
 
Habari za Asubui wana JF,

Naomba kuleta mada kwenu kuhusu haya mashirika ya kigeni yanayojiita ya kusaidia binadamu (humanitarian) au kujiita mashirika ya kimataifa yasiokuwa ya kiserikali (INGO). kwa mfano; Medecins sans frontieres, Medecins du monde na mengine mengi.

Kwanza kabisa mimi ni mwajiriwa wa moja ya haya mashirika na kilichonileta huku ilikuwa sio mshahara au maslahi mazuri bali ukosefu wa ajira wa muda mrefu na kukaa sana mtaani bila kazi maalum.

Nilipata shavu kwenye hizi shirika za kigeni humanitarian, lakini nilichokutana nacho huku nafikiri sijawahi kutana nacho toka nimeanza kufanya kazi kwenye mashirika binafsi.

Kwanza kabisa ogopa shirika lenye chimbuko au kutokea uswisi au ufaransa, hawa jamaa ni wabaguzi sijawai kuona. Pili, viwango vyao vya mishahara ni vibovu sana na hata mazingira ya kazi kwa wazawa ni magumu sana. Kuna muda unajikuta upo kama mtumwa ndani ya nchi yako kwa sababu tu hauwezi kuacha kazi mana mtaani ni pagumu sana na kazi hakuna. na haya mashirika wanatumia kigezo hiko kama fimbo ya kuchapia wazawa.

Pia, wanatumia sana loop holes za sheria zetu za tanzania ili kutukandamiza, kwa mfano, kuna kitu kinaitwa internal regulations, hzi ni sheria za kikandamizi ambazo zimetungwa kulingana na sheria ya ajira ya Tanzania lakini wametumia mianya ya sheria hiyo ili kuwabana national staff.

Tukirudi kwenye mishahara, mtu anaitwa officer mshahara unaanzia laki 8 take home na hata kama ulitoka sehemu unalipwa zaidi watakuambia wao salary grid yao ipo fixed na hakuna makubaliano yoyote au negotiations zozote.

Hata ufanye kazi kama punda siku saba za wiki hakuna promotions au bonus yoyote, na hata ikitokea kuna nafasi zimetangazwa ambazo ni za level ya juu yako, itakubidi uiombe kama mtu alie nje ya shirika na ufanye interview na asilimia kubwa wanazikosa hizo nafasi.

Mwisho wa siku unajikuta unaletewa supervisor na utamfunindisha kazi. na lengo kuu ya wao kufanya hivi ni kwasababu wanataka watu wapya kutoka nje ya shirika wasiojua mienendo ya shirika. na mara nyingi wale wasiokuwa na uvumilivu huwa wanaacha kazi baada ya muda mfupi wa kuajiriwa.

Serikali yetu imelala wakati vijana wao wananyanyaswa kwenye nchi yao na wageni. mashirika haya pia ya sheria au policy inayosema mzawa au national staff kwenye field level hawezi kufika level ya manager bali ataishia level ya supervisor kushuka chini.

Mpaka muda huu toka nimeanza kazi, kuna watu kama nane wameacha kazi au kufukuzwa kwa makosa ya kipumbavu.

Sasa naendelea kujiuliza kwanini nafasi za juu za mashirika haya bado zimeshikiliwa na wazungu ambao hata sheria za tanzania hawazijui? hauwezi ukaleta HR manager kutoka vietnam au mexico au kenya ambae hajui sheria za nchi au project coordinator kutoka kenya, pakistan au nigeria wakati wapo watanzania wenye sifa na vigezo zaidi ya hao wanaokuja kushika hizo nafasi.

Kwa mfano, wana tabia ya kutangaza nafasi lakini lengo kuu ni kucheza na sheria za nchi wakati wanajua kabisa wazawa watakaoomba hizo nafasi hakuna atakaepewa kwasababu wanataka kutengeneza hoja kuwa hakuna mwenye vigezo ili walete watu wao wabaguzi kuja kushika hizo nafasi.

Kama kuna mhusika yoyote wa uhamiaji, wizara ya afya au serikali kuu ambae yumo hum tafadhali sana tunaomba muyachunguze haya masharika kabla ya kuyaruhusu kufanya kazi ndani ya nchi yetu nzuri.

Vijana wa kitanzania wanateseka na kunyanyasika ndani ya nchi yao kwa kigezo tu cha kutokuwa na ajira.

Naomba kuwasilisha!

Mkerekewa Mzawa anaefanya kazi MSF
Kuna kishirika kinaitwa Red Sweater kipo monduli nacho ni kishirika hovyo mno, pale Wana promote sexual corruption, Director anafukuza wafanyakazi kama njugu, Manager anatomba wafanyakazi wa kike Kwa lazima. Bogus organization
 
Hao wanokandwa kwann wasikusanye ushahidi wakamu expose huyo manager au wanafurahia kuliwa?
 
Mleta mada umeongea mengi lakini kukujibu

1 Mashirika yote ya kigeni huwa wana idadi ya watu wanaoruhusiwa kuwaleta watakaoamua wenyewe Kumbuka hizo pesa za misaada au mitaji wanatoka nayo kwao kwa hiyo. Lazima wawe na watu wao wa kusimamia hizo shughuli na pesa zao.Uhamiaji wanaruhudu watu sita .Wao wenyewe wenye hela zao ndio huamua wamlete nani kwa nafasi ipi mara nyingi vyeo vya juu na vya fedha,na usimamizi vitengo mara nyingi hushika wao wenyewe iwe NGO ya kimataifa au kampuni ya kimataifa ya uwekezaji .Hivyo mwajiriwa mzawa kushika vyeo hivyo vikubwa vya juu huwa sio rahisi japo wengine huachia lakini hawalazimiki

2.Mishahara huwa kuna utofauti wao wa nje hulipwa mishahara yao kule kwao makao makuu kwa dola wakati sheria zetu xinataka mwajiriwa mzawa alipwe kwa viwango vya dani ya nchi kwa pesa ya ndani alipoajiriwa na NGO iliposajiliwa.Ikisajiliwa Tanzania kama tawi utalipwa kwa sheria na viwango vya Tanzania sio vya nje.Wao wenye shirika watalipwa kwa viwango vya kwao nchini kwao na sheria za kwao

Sheria za nchi zinakubana wewe mzawa.Ukitaka kufaidika upate uhamisho wa shirika hilo hilo utoke Tanzania uhamishiwe hata kenya hapo.Mshahara utabadilika utalipwa kwa viwango vya kimataifa vya kwao sio vya kenya au Tanzania sababu sasa unakuwa mfanyakazi wa head office

Ushauri vuta subira chapa kazi kuna siku waweza kuona kama uko vizuri wakakupeleka branch zingine nchi zingine
 
Habari za Asubui wana JF,

Naomba kuleta mada kwenu kuhusu haya mashirika ya kigeni yanayojiita ya kusaidia binadamu (humanitarian) au kujiita mashirika ya kimataifa yasiokuwa ya kiserikali (INGO). kwa mfano; Medecins sans frontieres, Medecins du monde na mengine mengi.

Kwanza kabisa mimi ni mwajiriwa wa moja ya haya mashirika na kilichonileta huku ilikuwa sio mshahara au maslahi mazuri bali ukosefu wa ajira wa muda mrefu na kukaa sana mtaani bila kazi maalum.

Nilipata shavu kwenye hizi shirika za kigeni humanitarian, lakini nilichokutana nacho huku nafikiri sijawahi kutana nacho toka nimeanza kufanya kazi kwenye mashirika binafsi.

Kwanza kabisa ogopa shirika lenye chimbuko au kutokea uswisi au ufaransa, hawa jamaa ni wabaguzi sijawai kuona. Pili, viwango vyao vya mishahara ni vibovu sana na hata mazingira ya kazi kwa wazawa ni magumu sana. Kuna muda unajikuta upo kama mtumwa ndani ya nchi yako kwa sababu tu hauwezi kuacha kazi mana mtaani ni pagumu sana na kazi hakuna. na haya mashirika wanatumia kigezo hiko kama fimbo ya kuchapia wazawa.

Pia, wanatumia sana loop holes za sheria zetu za tanzania ili kutukandamiza, kwa mfano, kuna kitu kinaitwa internal regulations, hzi ni sheria za kikandamizi ambazo zimetungwa kulingana na sheria ya ajira ya Tanzania lakini wametumia mianya ya sheria hiyo ili kuwabana national staff.

Tukirudi kwenye mishahara, mtu anaitwa officer mshahara unaanzia laki 8 take home na hata kama ulitoka sehemu unalipwa zaidi watakuambia wao salary grid yao ipo fixed na hakuna makubaliano yoyote au negotiations zozote.

Hata ufanye kazi kama punda siku saba za wiki hakuna promotions au bonus yoyote, na hata ikitokea kuna nafasi zimetangazwa ambazo ni za level ya juu yako, itakubidi uiombe kama mtu alie nje ya shirika na ufanye interview na asilimia kubwa wanazikosa hizo nafasi.

Mwisho wa siku unajikuta unaletewa supervisor na utamfunindisha kazi. na lengo kuu ya wao kufanya hivi ni kwasababu wanataka watu wapya kutoka nje ya shirika wasiojua mienendo ya shirika. na mara nyingi wale wasiokuwa na uvumilivu huwa wanaacha kazi baada ya muda mfupi wa kuajiriwa.

Serikali yetu imelala wakati vijana wao wananyanyaswa kwenye nchi yao na wageni. mashirika haya pia ya sheria au policy inayosema mzawa au national staff kwenye field level hawezi kufika level ya manager bali ataishia level ya supervisor kushuka chini.

Mpaka muda huu toka nimeanza kazi, kuna watu kama nane wameacha kazi au kufukuzwa kwa makosa ya kipumbavu.

Sasa naendelea kujiuliza kwanini nafasi za juu za mashirika haya bado zimeshikiliwa na wazungu ambao hata sheria za tanzania hawazijui? hauwezi ukaleta HR manager kutoka vietnam au mexico au kenya ambae hajui sheria za nchi au project coordinator kutoka kenya, pakistan au nigeria wakati wapo watanzania wenye sifa na vigezo zaidi ya hao wanaokuja kushika hizo nafasi.

Kwa mfano, wana tabia ya kutangaza nafasi lakini lengo kuu ni kucheza na sheria za nchi wakati wanajua kabisa wazawa watakaoomba hizo nafasi hakuna atakaepewa kwasababu wanataka kutengeneza hoja kuwa hakuna mwenye vigezo ili walete watu wao wabaguzi kuja kushika hizo nafasi.

Kama kuna mhusika yoyote wa uhamiaji, wizara ya afya au serikali kuu ambae yumo hum tafadhali sana tunaomba muyachunguze haya masharika kabla ya kuyaruhusu kufanya kazi ndani ya nchi yetu nzuri.

Vijana wa kitanzania wanateseka na kunyanyasika ndani ya nchi yao kwa kigezo tu cha kutokuwa na ajira.

Naomba kuwasilisha!

Mkerekewa Mzawa anaefanya kazi MSF
Uko MSF wapi? Nyarugusu? au Nduta?
 
Pia sio mashirika yote ni ya hovyo
Tuko tunakula bata Chuga huku kiroho safi na International NGOs
 
Ahsante kwa muongozo.

Pia muache kuwakandia walio Gavo kwa kuwaambia wana maslahi duni kisa huko mnapokea ahueni kwa masimango
Mkuu huku ni kama gavoo tu, binafsi sijawahi kuwakandia kabisa coz hata mimi bado natupia application nikiona nafasi za serikali zimetangazwa. kwa sasa ni bora serikali kuliko sekta binafsi huku manyanyaso na masimango ni mengi.
 
Pia sio mashirika yote ni ya hovyo
Tuko tunakula bata Chuga huku kiroho safi na International NGOs
zipo International NGOs zinajielewa na zinatambua umuhimu wa maslahi bora ya mtu. sana sana zenye ufadhili wa usaid ndio ziko vizuri ila hzi za wafaransa ni nyoko. wanahisi kama wamekusaidia sana kukupa ajira.
 
Nilisikia MD wa MSF Nduta analipwa 2.8M gross
Hyo laki 8 ni kwa title ipi
huyo analipwa hiyo kwasababu ni national staff lakini angekuwa expat angelipwa kwa dola hela ndefu na kulipwa per diem kila siku 40k, rent free housing, kufuliwa, kupikiwa mpaka chakula wananunuliwa na shirika. na kama wakienda likizo wanapelekwa na gari za ofisi mpaka dar au na ndege lakini mzawa unajitegemea upande saratoga kwa hela yako na hakuna per diem wala malazi bure wala chakula bure. alaf mshahara wa kisenge.
laki 8 ni kwa position zote ambazo ni level 3 kama unaijua MSF utaelewa ninachosema.
 
Back
Top Bottom