kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,175
- 3,221
Habaini ndugu zangu, Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 42, kama mnakumbuka nilileta mkasa ulio nitokea mwezi ulio pita kuhusu mzee wangu baada ya kuuza nyumba yake kwa shilingi milion 165 amegoma kabisa kunipa mgao mimi mtoto wake, baada ya kugoma nikafata utaratibu wa kisheria kumfikisha kwenye vyombo vya kisheria, nilianzia kwenye ofisi ya mtaa (walininyima haki yangu baadae nilikuja kugundua ofisi ya mtaa wanashirikiana na baba kutaka kunizurumu haki yangu kama mtoto),
Nikapanda mpaka ngazi ya kata (uko nako sikupata haki yangu kama mtoto), nikapanda moja kwa moja mahakamani (uko nako sijapata haki yangu) na maamuzi ya mahakama yalitoka siku ya jana 04.02.2022, baada ya uamuzi kutolewa mahakamani cha kushangaza wakati narudi nyumbani (mimi nilipanda usafiri wa daladala kivyangu) nilipofika nyumbani nashangaa kukuta nguo zangu zimetolewa nje kwenye begi langu na kikaratasi kimewekwa chini kimeanikwa kama kinavyo someka hapo
Wakuu huyu baba angu kila ngazi nahisi anaonga ili ashinde kesi kwa kuwa yeye ana pesa, nataka kufanya juu chini nikakate rufaa ili niendelee kupigania haki yangu ya kupata mgao wa pesa kama mtoto wa pekee na ni mtoto wake mkubwa wa tatu na pia nimesoma mpaka chuo kikuu (nilieleza nina elimu kubwa tu ya BCom ya marketing kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam shule ya UDBS).
Nilishapata mpaka mchumba ambaye nilitegemea nikipata huu mgao niweze kumuoa ila mpaka mpenzi wangu anaanza kutokunielewa maana mzee pesa hataki kutoa, na kuna mtu alikuwa anauza gari aina ya nissan dualis nilishamuambia asiuze hiyo gari anivumulie kuna pesa naifatilia ntalinunua tu ilo gari, ila cha kushangaza huyu baba angu mipango yangu yote ananivurugia, naombeni msaada wa wanasheria wazuri nataka nimpeleke kwenye mahakama ya rufaa uyu mzee maana mimi ni mtoto wake kabisa na ni mtoto wake wa tatu kuzaliwa na pia nimesoma sana nina elimu kubwa sana naitajika nipewe kipaumbele.
Mnisaidie ndugu zangu.