Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 384
- 757
Mambo ya kuepuka kama baba wa familia
Siku moja tukiwa kazini tunaendelea na majukumu, nikapokea simu ya rafiki yangu akiomba ruhusa kwa bosi ya kutokufika ofisini kutokana na changamoto za kiafaya, mie nikatimiza wajibu wangu na nikawa naendelea na ratiba zangu, nikiwa naenedelea na kazi zangu rafiki yake na rafiki yangu akawa anapita kwenye ofisi zetu akanijulia hali na kunipa habari za rafiki yangu.
Habari ambayo nilipokea sio kwamba ni habari ngani kusikia lakini ni jambo ambalo sikulitarajia, kwa sababu alikuwa ni mtu wa ibada na shughuli za kanisa , habari ile ilikuwa ni kwamba ndugi yetu anastres mara baada ya kupokea taarifa ya kwamba mchepuko wake ni mjamzito ndio maana kashindwa kufika ofisini.
Changamoto za michepuko kwa wanaume linaelekea kuwa jambo la kawaida siku kadri ya siku. Wakati natafakari nakakumbuka matukio kadhaa ya baadhi ya watu ambao tunafahamia nao ambao kwa namna moja au nyingi matatizo hayo yalipelekea ndoa zao kuingia mogogoro mikubwa.
Mara nyingi wababa tunazani kwamba ni haki yetu kuwa na wake zaidi ya mmoja au zaidi ya wale ambao tumepewa kwa mujibu wa taratibu za dini, lakini cha kushangaza hatuna uvumivu kwa wake zetu wakitutenda.
Madhara ya michepuko kwenye familia ni mengi ila yanategemea kati ya familia na familia, nimeshuhudia ndoa zilivunjika na kuwaacha watoto wakiwa wamechanganyikiwa hawajui cha kufanya kutoka na makosa ya wazazi wao
Takwimu nyingi zinaonyesha wanawake wana ishi miaka mingi ukilinganisha na wanaume, na inawezekana hatujui sababu kwanini wanawake wanishi miaka mingi
Rafiki yangu huyu alikuwa na familia yake na mke na watoto lakini hapo hapo nje ya ndoa alipata mchepuko na mtoto juu, na jambo ili kulifanya kuwa siri kwa miaka mingi.
Siri za michepuko zinaua mioyo ya wanaume taratibu pasipi kujua, sijasomea mambo ya afya lakini nachojua upendo unakaa moyoni , sasa fikiri unawatu wawili hawajuani uko ndani ya moyo nini kitatokea?
Kuna mmoja wa jirani yangu yeye alikimbia mji kwa sababu alimpatia mwanfunzi ujauzito na kukimbia na kuitelekeza familia, ushawai kufikiria unatafutwa na polisi na familia ya binti uliyempa ujauzito na bado umeacha mke na watoto wako?
Unaweza kusema haha hainawezekana hii, ni mambo ambayo sio tume hadithiwa tumeyaona kwa macho ya nyama, unamuuliza mtu kwani ilikuwaje? Unajua mke wangu ananifanyia hivi? Mara hoho unajua mke wangu ndio sababu nk? Je uko tayari kuhatarisha maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine?
Unafikiri ukifa kwa pressure au strock hasara kwa nani? Hasara kubwa watapata watoto wako na mke wako ila wazazi wako watapata hasara kubwa kukupoteza.
Kunasikua unapigiwa simu na semeji yako anakwambie rafiki yako amekuwa anaumwa sana siku hizi uwe unamwombea mtumishi? Kumbe mtu haumiwi chochote ni moyo tu umejaa siri kiasi unafika mahali unakuwa kama mgonjwa?.
Kuna siku nilisoma meme kwenye mitandao mtu anasema ulishawai kuchanganywa na mchepuko hadi ukatamani umuahadithie mke wako? Inawezekana tukafanya kichekesho lakini ndio ukweli ulivyo kuna watu wanachangaya mambo hadi wanachanganyikiwa kumbe ni mambo ya siri.
Unakuta mtu anajitete haha mbona babu zetu walikuwa na wake wanne ? Kwanini mimi niwe na mke mmoja? Akili za kimaskini kwanini tuchukue tabia za kimaskini za mababu zetu na zile tabia za kitajili tunaziacha
Siku moja nilikuwa naongea na mdogo wangu nikamwambia unaweza kuona ni sawa kuwa na wake zaidi ya mmoja kwa sababu babu alikuwa hivyo lakini mbona hauna mashamba na utajiri kama wababu? Kwanini unataka kurithi umaskini wa babu lakini hautaki utajiri wababu.
Nilimwomba Mungu katika kitu ambacho tunaweza kurithishana sio tabia za umaskini hizo mimi sizitaji nataka tabia za utajiri.
Siku moja mzee wangu mmoja alinielezea kama kijana wake akaniambia mtoto wangu usije ukachekupuka, akanielezea kilichomkuta yeye na mke wake na akaniambie usije ukachepuka, sikujua alitaka kuniambia nini lakini nilijua alitaka kunisaidia makosa aliyofanya kwetu ni shule tusijepitia kwenye makosa ambayo walipita wao
Mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku aliimba wimbo wa dunia haina huruma, ule sio wimbo ni ushuhuda wa mtu ambaye mazingira aliyokutana nayo yalipelekea kuchepuka na kupata mtoto, na kwa sababu dhambi ni aibu ya wati wote aliona kukaa na siri hiyo moyoni ni sumu ambayo inamuua kimyakimy akaaamua kusema ukweli tuna ona madhara aliyoyapata lakini Mungu alimsaidia akapata kupona.
Utakaa na siri hiyo mpaka lini? Kuna wengine wanasema siku nikifa mke wangu atajua watoto wangu ? Ndugu yangu kwanini unataka kufa na siri moyoni ? Unajua uko unakokwenda? Utapata amani na siri hizo, tumgeukia Mungu tutubu , tuache dhambi , hapo zamani Mungu hakuyaona aya ila anasema tubuni turejee tupate nyakati za kuburudishwa kwa kuwako Bwana