Baba wa Joshua aomba serikali ya Tanzania iongee na nchi rafiki za HAMAS ili waachie mwili wa mwanae

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
29 December 2023
Kilimanjaro International Airport
Tanzania

BABA WA JOSHUA AOMBA SERIKALI YA TANZANIA IONGEE NA NCHI RAFIKI ZA KUNDI LA HAMAS
BABA MZAZI WA JOSHUA MOLLEL AMWAGA MACHOZI, AREJEA TANZANIA BILA MWILI WA MWANAE ALIYEUWAWA NA HAMAS



View: https://m.youtube.com/watch?v=DTeLiUa7QVs

Mzee Mollel ameongea mara baada ya kutua ktk uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro akitokea Israel ambapo alialikwa na serikali ya Israel kufuatia mwanae Joshua kutekwa na kuuawa na kundibla HAMAS tarehe 7 Oktoba 2023

Mzee Mollel asema amepewa taarifa za kina na jeshi la Israel IDF na viongozi wa Israel kuhusu kilichotokea na kuwa wamemshauri Mzee Mollel kuiomba serikali ya Tanzania iongee na nchi za Uturuki, Qatar n.k ili kundi hilo waweze kuuachia mwili wa mwanae uweze kurejeshwa Tanzania.

Mzee Mollel asema kuwa kundi hilo liliua na kuteka watu kutoka Mataifa mbalimbali bila kujali uraia au rangi ya mtu. Na Mzee Mollel aliweza kufika hadi katika kambi ya wafanyakazi wa kilimo ambapo mwanae na watu wengine walikubwa na uharamia huo.

27 December 2023

Family of Tanzanian national call for release of his body held by Hamas​


1703860369681.png

The Foreign Ministry held a special ceremony in memory of Tanzanian national Joshua Mollel, an agronomy student who came to Israel from Tanzania to study, and who was murdered on October 7. His body was abducted by Hamas terrorists from Kibbutz Nachal Oz and taken to Gaza. Mollel's father, Loitu, called on the international community to act for the immediate release of his son's body from Gaza so that he can bring him for a proper burial.

TOKA MAKTABA:
WATANZANIA WATAKA BALOZI WA PALESTINA ALAANI NA PIA KUWEZESHA MWILI WA JOSHUA UPATIKANE
Balozi wa Palestine nchini Tanzania Mh. Hamdi Mansour Abuali alimwe barua mara moja na kutimuliwa kama persona non grata

Balozi wa Palestina badala ya kwenda wizara ya mambo ya nje kutafuta kuungwa mkono na Tanzania anaamua kuugawa umma wa waTanzania kwa kwenda msikitini kuomba kuungwa mkono na sehemu ya jamii inayounda Tanzania.

Video hapa chini ikionesha Mh. Balozi Hamdi Mansour Abuali akiwa anafanya shughuli zinazohatarisha usalama wq nchi kinyume na mikataba ya Vienna protocol kuhusu kazi za balozi

View: https://m.youtube.com/watch?v=auOKnvgArZ8&pp=ygUSQmFsb3ppIHdhIHBhbGVzaW5h

Waarabu wanawachukulia kwa tahadhari kubwa wapalestina, lakini sisi waswahili tuna fuata mkumbo

BALOZI wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali amewashukuru Watanzania wanaoendelea kupaza sauti zao kulaani mashambulizi ya makombora yanayofanya na Taifa la Israel katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina.
Balozi Abuali,ametoa shukrani hizo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya Waumini mara baada ya swala ya kuombea amani katika nchi ya Palestina .

Aidha,Balozi Abuali,amesema mashambulizi hayo yamekuwa yakitoa roho za watu wasiokuwa na hatia.


Kwa upande wake Kaimu Mkoa wa Dar es Salaam,Shekh Walid Alhad Omar,amesema uhusiano wa Tanzania na Palestina ni wa siku nyingi hivyo na kuwataka watanzania kulaani kile kinachoendelea Palestina.

Huyu balozi aitwe wizara ya mambo ya nje kuonywa kuacha kukosoa sera za mahusiano kimataifa za Tanzania kutoingilia upande wowote, aache kutaka kuchochea maandamano.

Balozi huyu wa Palestina hajui mipaka yake ya kidiplomasia, muda mwingi anataka kutuamrisha kufanya mambo yasiyokwenda na sera za nchi yetu kimataifa za diplomasia ya kiuchumi, watalii waje wengi kupitia Tanzania Royal Tour, wawekezaji,

Anaweza kutimuliwa kutokana na mienendo yake isiyokuwa ya cheo cha balozi . Kule Chad balozi alitimuliwa kwa kufanya kazi sizizo za kibalozi.

Gov't of Chad orders Gordon Kricke to leave country within 48 hours for 'non-respect of diplomatic customs', ministry says.
Le Monde.fr
https://www.lemonde.fr › 2023/04/10
Chad expels German ambassador, blaming 'impolite attitude'

10 Apr 2023 — The German ambassador to Chad, declared persona non grata by the government for his "impolite attitude", was
 
hawawezi kupata huo mwili utakuwa umeshaoza na hamas hawana freeza. na huyo balozi wa palestina anaongea uchafu tu hapo hadi anatia kinyaa.
Labda tusubiri vita viishe eidha kwa Hamas kukimbia au kujisalimisha au kuuwawa wote, au kuwe na kusimama kwa vita (Pause).

Baada ya hapo kilichobakia hata kama ni mfupa mmoja wa Ndugu yetu urejeshwe Nyumbani ili upewe mazishi yanayostahili.
 
Back
Top Bottom