Balozi wa Palestina Nchini aomba Dunia ipaze sauti kulaani vita dhidi ya Israel

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Watanzania wameombwa kupaza sauti zao kulaani mashambulizi yanayofanywa na Taifa la Israel kwenye Ukanda wa Gaza eneo la Palestina.
945a8e0b-95b4-4abc-905d-4484a17bc990.jpeg
Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Palestina Nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya machafuko yanaendelea kati ya Israel na Palestina.

Balozi Abuali amesema mashambulizi hayo yamekuwa yakitoa roho za watu wasiokuwa na hatia.

Balozi Abuali amesema mbali na kuondoa roho za watu machafuko hayo yamewaacha zaidi ya watu milioni 2.2 ya Palestina wakiwemo Watoto kukosa mahali pakukaa.

"Hakuna mafuta, hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna maji yaani kila kitu kimefungwa, zaidi ya watu 1300 wamekufa, Watoto wakiwemo 344, makazi 790 yameharibiwa huku zaidi ya Wapalestina 339,000 wameyakimbia makazi yao," amesema.

Hata hivyo, Balozi Abuali amezitaka Jumuiya za Kimataifa kupinga kile alichokiita ukatili unaofanywa na Israeli kwa Wananchi wa Palestina.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Mshikamano kati ya Tanzania na Palestina, Abdulaha Athuman amewataka Watanzania waungane kwa pamoja kulisaidia Taifa la Palestina kulaani kile kinachofanywa na Israel kwa Taifa la Palestina.

Athumani amesema Taifa la Palestina kwa miaka mingi limekuwa likisaidia Mataifa ya Afrika ikiwemo ukombozi wa uhuru kwenye baadhi ya nchi za Afrika.
 
Attachments

  • 8892f278-ad75-48d3-9410-0a8006172b71.jpeg
    8892f278-ad75-48d3-9410-0a8006172b71.jpeg
    51.1 KB · Views: 1
Hakuna mwenye akili timamu atamsikiliza huyu bwana.

Wapelestina wa Gaza wana chaguo moja katika mawili yaliyopo: kujitenga na magaidi wa Hamas ili maisha yao yaheshimiwe; au kushikamana na magaidi ya Hamas ili wafe pamoja na magaidi.

Ninaowaonea huruma ni watoto wadogo ambao hawana maamuzi zaidi ya maamuzi ya wazazi wao.
 
Yaani umamchokoze mtu mwenyewe akikupiga uanze kumlaani!!! Hatuko serious kabisa na sisi Watanzania tusiingie kwenye mtego huo zaidi tuwaombee wapigane kiustaarabu
 
Kwahiyo walivyowalipua wenzao ilikuwa sawa
Nao wametunguliwa ndio wanataka tupaze sauti.

Kunya anye kuku,akinya bata amehara.

Hiyo huruma anatakiwa aionyeshe kwa pande zote,siyo upande wake tu .
Inshort hakuna mtu anayeentertain vita.

Shallom Israeli,Taifa teule la Mungu.
 
Watanzania wameombwa kupaza sauti zao kulaani mashambulizi yanayofanywa na Taifa la Israel kwenye Ukanda wa Gaza eneo la Palestina.
Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Palestina Nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya machafuko yanaendelea kati ya Israel na Palestina.

Balozi Abuali amesema mashambulizi hayo yamekuwa yakitoa roho za watu wasiokuwa na hatia.

Balozi Abuali amesema mbali na kuondoa roho za watu machafuko hayo yamewaacha zaidi ya watu milioni 2.2 ya Palestina wakiwemo Watoto kukosa mahali pakukaa.

"Hakuna mafuta, hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna maji yaani kila kitu kimefungwa, zaidi ya watu 1300 wamekufa, Watoto wakiwemo 344, makazi 790 yameharibiwa huku zaidi ya Wapalestina 339,000 wameyakimbia makazi yao," amesema.

Hata hivyo, Balozi Abuali amezitaka Jumuiya za Kimataifa kupinga kile alichokiita ukatili unaofanywa na Israeli kwa Wananchi wa Palestina.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Mshikamano kati ya Tanzania na Palestina, Abdulaha Athuman amewataka Watanzania waungane kwa pamoja kulisaidia Taifa la Palestina kulaani kile kinachofanywa na Israel kwa Taifa la Palestina.

Athumani amesema Taifa la Palestina kwa miaka mingi limekuwa likisaidia Mataifa ya Afrika ikiwemo ukombozi wa uhuru kwenye baadhi ya nchi za Afrika.

Hivi wangeyafuata makubaliano ya Oslo kipi kingeharibika?
 
vita ni hamas na himaya yake dhidi ya israel na himaya yake, msipotoshe kana kwamba israel anapigana na palestina, mbona west bank hawaguswi? shida ni hao gaza juzi walifanya sherehe kusikia waisrael 1000 wameuliwa na wengine kutekwa... ila yakirud kwao wanataka huruma.
akitaka awe fair awalaani kwanza hamas walioleta uchokozi kwa ukubwa huo, ilihali wanajua Israel isingekaa kimya.
vita vya kujitakia.
 
Kwahiyo walivyowalipua wenzao ilikuwa sawa
Nao wametunguliwa ndio wanataka tupaze sauti.

Kunya anye kuku,akinya bata amehara.

Hiyo huruma anatakiwa aionyeshe kwa pande zote,siyo upande wake tu .
Inshort hakuna mtu anayeentertain vita.

Shallom Israeli,Taifa teule la Mungu.
Labda wao ndiyo wana haki zaidi ya kuishi kuliko waisrael
 
Back
Top Bottom