Poleni Sana wanafamilia, mungu ampumzishe pema peponi
Familia ya Freeman Aikael Mbowe wametangaza kifo cha Baba Mdogo wa Mbowe aliyefariki baada ya kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mwanaye kutuhumiwa Ugaidi

Amefariki Hospitali ya Machame Julai 23, alikopelekwa baada ya kupata mshtuko

Freeman Mbowe ametuhumiwa kupanga njama za ugaidi na kuua viongozi wa serikali

View attachment 1864435
 
James Mbowe ameripoti kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa babu yake amefariki jana usiku baada ya kupata taarifa kuwa Freeman Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi.

Bado nafuatilia urasmi wa habari hizi!
 
Mbowe angetulia tu kwenye msiba wa kakake yote yasingemkuta haya, sema nimejifunza kitu kimoja, Cdm hawawezi siasa za maridhiano kama alizotaka kuzifanya mama mwanzoni, siasa za maridhiano haziwapi mileage
Siasa za maridhiano zikoje bwashee?

Chama kimoja?
 
Familia ya Freeman Aikael Mbowe wametangaza kifo cha Baba Mdogo wa Mbowe aitwaye Manase Alphayo Mbowe aliyefariki baada ya kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mwanaye kutuhumiwa Ugaidi

Amefariki Hospitali ya Machame Julai 23, alikopelekwa baada ya kupata mshtuko

Freeman Mbowe ametuhumiwa kupanga njama za ugaidi na kuua viongozi wa serikali



MANASE Alphayo Mbowe, baba mdogo wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 23 katika Hospitali ya Machame mkoani Kilimanjaro, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Ijumaa na James, mtoto wa Freeman wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akisema, alishtushwa baada ya kusikia tuhuma zinazomkabili mwanae za ugaidi

James amesema, babu yake huyo alifariki dunia akipatiwa msaada wa kupumua kwa kutumia mashine ya oksijeni, hospitalini hapo lakini “leo asubuhi akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo amefariki dunia.”

James amesema, taratibu za mazishi yake zitatangazwa baadae baada ya familia kukutana.

Amesema, enzi za uhai wake, babu yake huyo aliwahi kufanya kazi serikalini ikiwemo ofisi ya Rais. Ameacha watoto watano, wa kike mmoja na wa kiume wanne.

View attachment 1864583
Manase Mbowe enzi za uhai wake​
Ndugu zangu, wapendwa wangu, poleni sana na kuondokewa na mpendwa wetu, Manase Alphayo Mbowe. Kwanza Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin. Kwenu nanyi ndugu, namwomba Mungu Mwenyezi awape uvumilivu, subira na ujasiri katika kipindi kigumu hiki na hatimaye kuweza kuyatekeleza yale yanayotupasa kwa marehemu wetu kwa sifa na UTKUFU wa MUNGU.Amin
 
Back
Top Bottom