Familia ya Freeman Aikael Mbowe wametangaza kifo cha Baba Mdogo wa Mbowe aitwaye Manase Alphayo Mbowe aliyefariki baada ya kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mwanaye kutuhumiwa Ugaidi

Amefariki Hospitali ya Machame Julai 23, alikopelekwa baada ya kupata mshtuko

Freeman Mbowe ametuhumiwa kupanga njama za ugaidi na kuua viongozi wa serikali



MANASE Alphayo Mbowe, baba mdogo wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 23 katika Hospitali ya Machame mkoani Kilimanjaro, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Ijumaa na James, mtoto wa Freeman wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akisema, alishtushwa baada ya kusikia tuhuma zinazomkabili mwanae za ugaidi

James amesema, babu yake huyo alifariki dunia akipatiwa msaada wa kupumua kwa kutumia mashine ya oksijeni, hospitalini hapo lakini “leo asubuhi akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo amefariki dunia.”

James amesema, taratibu za mazishi yake zitatangazwa baadae baada ya familia kukutana.

Amesema, enzi za uhai wake, babu yake huyo aliwahi kufanya kazi serikalini ikiwemo ofisi ya Rais. Ameacha watoto watano, wa kike mmoja na wa kiume wanne.

View attachment 1864583
Manase Mbowe enzi za uhai wake​
Sio yeye tu kuna watanzania wengi tu wamekufa kwa sababu ya kupata huo mshtuko wa Mbowe kukamatwa kwa Ugaidi
 
RIP Manase
Jumong akituma pole tena mnitag
CCM ni chama cha kishetani, kidhalimu, kiharamia na kinajisi kinacholenga kuidhoofisha nchi yetu nzuri ajabu na tajiri aliyotupa MUNGU Mwenyezi. Ee Mungu, Muumba wa Mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, uturehemu.
 
Mwamba majanga yanamuandama ila anapambana hadi mwisho. Huyu mwamba simuelewagi kabisa ana moyo wa namna gani yaani hadhoofishiki. Hata hili litapita na atakuwa imara kuliko jana.
Mbali ya mambo mengine Makuzi pia yanachangia kwenye ujasiri wa mtu.
 
Mwamba ana trend kinoma Ila Sasa naona anapitia magumu,

Mimi nadhani wangempa favor Wamuache agonge fegi zake na whiskey japo alale kwa utulivu huko alipo.
 
Umetumia kipimo gani kujua chanzo cha kifo chake?
Mtungi wa gesi ya oxygen aliopatiwa baada kupata changamoto la upumuaji baaa ya kutoka kwenye msiba wa marehemu kaka yake na F. Mbowe. Jamaani hili janga la corona tusilifanyie mzaha. Tuchuke tahadhari zote tunazoshauriwa na watalamu wa afya. Misangamano ya watu iwe marufuku na wala kusiwe na kibali cho chote kuruhusu misongamano. Iwe kwenye nyumba za ibada, viwanja za michezo, sherehe za arusi, kwenye daladala, kwenye mabasi, majumbani na kwenye masoko iwe marufuku.

RIP baba yake mdogo na Mwamba.
 
Back
Top Bottom