Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Familia ya Freeman Aikael Mbowe wametangaza kifo cha Baba Mdogo wa Mbowe aitwaye Manase Alphayo Mbowe aliyefariki baada ya kupata mshtuko baada ya kupata taarifa za mwanaye kutuhumiwa Ugaidi

Amefariki Hospitali ya Machame Julai 23, alikopelekwa baada ya kupata mshtuko

Freeman Mbowe ametuhumiwa kupanga njama za ugaidi na kuua viongozi wa serikali

1627031031738.png


MANASE Alphayo Mbowe, baba mdogo wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 23 katika Hospitali ya Machame mkoani Kilimanjaro, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Ijumaa na James, mtoto wa Freeman wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akisema, alishtushwa baada ya kusikia tuhuma zinazomkabili mwanae za ugaidi

James amesema, babu yake huyo alifariki dunia akipatiwa msaada wa kupumua kwa kutumia mashine ya oksijeni, hospitalini hapo lakini “leo asubuhi akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo amefariki dunia.”

James amesema, taratibu za mazishi yake zitatangazwa baadae baada ya familia kukutana.

Amesema, enzi za uhai wake, babu yake huyo aliwahi kufanya kazi serikalini ikiwemo ofisi ya Rais. Ameacha watoto watano, wa kike mmoja na wa kiume wanne.

Mbowe Baba.jpg

Manase Mbowe enzi za uhai wake
 
Back
Top Bottom