TANZIA Mwandishi nguli wa maudhui ya kiingereza, Zephania Ubwani afariki dunia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,508
8,129
Mwandishi mkongwe wa habari nchini, aliyekuwa akiandikia Gazeti la The Citizen linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) mkoani Arusha, Zephania Ubwani amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua ghafla wakati akiwa katika majukumu ya kikazi katika Hoteli ya Kibo Pallace jijini humo.

images (31).jpeg

Katika picha, Mzee Ubwani(kulia) akipokea tuzo enzi za uhai wake nchini Uganda akiibuka kinara kuripoti maudhui ya elimu ya juu​

Taarifa zilizopatikana kutoka Arusha zinasema Ubwani wakati anamfanyia mahojiano mmoja wa watoa habari wake ndani ya hoteli hiyo, alijisikia vibaya na alipatiwa msaada wa kupelekwa Hospitali ya AICC iliyopo jirani na hoteli hiyo lakini alifariki dunia wakati anachunguzwa kilichokuwa kikimsumbua.

Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV Arusha, Asraji Mvungi aliyekuwa naye wakati akifanya mahojiano hayo, amesema tatizo la kiafya lilianza kumtokea saa 8 mchana leo wakati wanamfanyia mahojiano mkurugenzi mkuu wa Costech.
 
Back
Top Bottom