mmh, ujue kinacholeta utata ni huu mkanganyiko wa tamaduni tunaopitia.
Zamani hata mama afariki na aache mtoto mchanga, mtoto huyo atalelewa na mwanamke tu, aidha kwa ngazi ya mama mkubwa, mdogo, shangazi, bibi.
Na kwa asili ya kitanzania ya zamani baba hakuweza kupakatana na bintiye bila sababu maalum, labda kama mgonjwa.
Kwa hali ya sasa ambapo wanamme nao wanalea na kufunga pampaz, hiyo ni changamoto.
Ila, hata kama utamfunga pampaz binti yako wa mwaka mmoja, je utaendelea kumuogesha hadi ana miaka 6?
Au utaendelea kumfanyia yale ulomfanyia akiwa na mwaka mmoja hadi awe na miaka 10?
Hata kama unamlea peke yako, kuna vitu utaanza kumfundisha kufanya mwenyewe hadi anafika miaka 6, vitu kama kwenda kujisaidia ama kuoga atakuwa anaweza.
Kingine, lazima kupakatana kati ya binti na baba yake kupungua akianza kufikia miaka mitano, inaweza ikapungua kidogo kidogo, hadi anafikisha miaka 8 ikakoma kabisa.
Mabinti wenyewe siku hizi wengine wanabalehe wakiwa na miaka 10 tu.
Hili swali ni la muhimu sana sijui kama watu wanaelewa; utaona wengi hawajafikiria situation ambayo mama hayupo Baba kaachiwa mtoto wa kike wa mwaka mmoja. Anamlea vipi bila kumbeba, kumkumbatia au kumpakata?