inategemeana wewe ni mtu wa utamaduni gani. kama ni wa wamagaribi, hata akiwa mzee unaweza kumpakata na kumbusu tu. ila kama ni wangu mimi, miaka mitano au sita mwisho. akishafika kama kumi hivi anaweza kukaa karibu yangu na kubanana tu labda kwenye kochi au kwenye gari etc, ila akifika kuanzia kumi na tano, distance kubwa inaanza kuwepo. nikikaa kochi moja, hata kama kuna nafasi pale itabidi yeye atafute kochi lingine, hiyo ndo adabu ya kiafrica. pia kuingia chumbani kwangu marufuku kuanzia miaka sita ivi. ulaya utakuta mtoto ana miaka kumi na tano anaenda kuwaamusha baba na mama wakiwa wamelala kitandani kwa kuwashika blanketi....baba ana bukta tu, mama ndo ivo bado wana uchovu wa kupigana mabao jana yake, ndo maana si ajabu sana kwa ulaya, nasema si ajabu imetokea mara nyingi mno, watoto kuwakuta wazazi wao wakiwa uchi wa mnyama wakifanya mapenzi laivu..na maisha yanaendelea.
Hapo kwenye blue umezidisha. Mtoto ana haki ya kuingia chumba cha wazazi anytime anataka, akiwa mkubwa anaweza kupiga hodi kabla ya kuingia. sioni sababu ya kutoingia hata kama una miaka 30.