Baadhi ya Taasisi za serikali na taasisi kubwa za binafsi acheni kuwadumaza na kuwarudisha kwenye umaskini wajasiriamali wadogo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,303
Kuna mambo yanaendelea kwenye nchi hii yanaonekana madogo lakini kadiri siku zinavyoenda yanaweza leta shida. Wote tunajua nchi yetu kama zilivyo nchi nyingi duniani ina uhaba mkubwa wa ajira. Tofauti na nchi kama China ni kuwa nchi karibu zote za Afrika zinaenda kuwa na tatizo kubwa zaidi kutokana na kutokuwa na viwanda. Kiufupi tatizo la ajira linazidi kuwa tishio. Wamejitokeza watu mbalimbali wazito nchini kuwasihi vijana kujiajiri lakini kinachoendelea kwa sasa ni ukatili na unyama kwa hawa vijana wadogo.

Iko hivi, ni kuwa vijana hufungua biashara zao ndogondogo ambapo kwenye harakati za kuuza bidhaa au huduma hutafuta kazi kwenye taasisi za serikali na zile za binafsi. Wenye bahati hupata tenda za kwenye taasisi hizo. Miaka ya nyuma ni taasisi za serikali tu zilikuwa zikilaumiwa kutolipa kwa wakati wazabuni kiasi cha kutishia mitaji yao. Lakini kwa nyakati hizi kumeibuka tatizo kubwa hata kwa taasisi binafsi kutolipa wazabuni kwa wakati au kuwadhulumu kabisa. Utakuta shule binafsi inamwambia kijana mwenye steshenari awapelekee vifaa fulani vya shule kwa makubaliano kwamba wakifikisha mzigo watalipwa ila matokeo yake kunatokea uzungushwaji kiasi kwamba kama kijana alikopa anajikuta matatani na kuonekana tapeli.

Isitoshe huu utaratibu wa taasisi binafsi kutumia majina yao kuwarubuni wazabuni unatumika na baadhi ya wamiliki kupunguza gharama za uendeshaji wa taasisi zao bila kujali maumivu ya wengine. Mtu kama una taasisi tafadhali lipa vijana wakishafanya kazi yako. Ni upuuzi mtu anafanya kazi dola ikiwa Tsh 2300 anakuja kulipwa dola ikiwa Tsh 2600. Hiyo ni hasara.

Taasisi za serikali sitaki kuziongelea sana kwa leo kwasababu zinajulikana jinsi nyingi zilivyo vichomi hasa mashule. Tafadhali tusapoti vijana kwa kulipa mapema badala ya kuwalipa kwa taabu.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kuna mambo yanaendelea kwenye nchi hii yanaonekana madogo lakini kadiri siku zinavyoenda yanaweza leta shida. Wote tunajua nchi yetu kama zilivyo nchi nyingi duniani ina uhaba mkubwa wa ajira...
Kwenye vikao vyenu vya CCM huwa hamuongelei hili?

CCM ni serikali sasa nashangaa sijui ndiyo yale mambo mkalitazame hili?

Kama katibu mwenezi anatatua matatizo ya watu badala ya chama sasa ndiyo serikali yenyewe hiyo.
 
Mimi siko kwenye hivyo vikao.
 
Kuna mambo yanaendelea kwenye nchi hii yanaonekana madogo lakini kadiri siku zinavyoenda yanaweza leta shida. Wote tunajua nchi yetu kama zilivyo nchi nyingi duniani ina uhaba mkubwa wa ajira. Tofauti na nchi kama China ni kuwa nchi karibu zote za Afrika zinaenda kuwa na tatizo kubwa zaidi kutokana na kutokuwa na viwanda. Kiufupi tatizo la ajira linazidi kuwa tishio. Wamejitokeza watu mbalimbali wazito nchini kuwasihi vijana kujiajiri lakini kinachoendelea kwa sasa ni ukatili na unyama kwa hawa vijana wadogo.

Iko hivi, ni kuwa vijana hufungua biashara zao ndogondogo ambapo kwenye harakati za kuuza bidhaa au huduma hutafuta kazi kwenye taasisi za serikali na zile za binafsi. Wenye bahati hupata tenda za kwenye taasisi hizo. Miaka ya nyuma ni taasisi za serikali tu zilikuwa zikilaumiwa kutolipa kwa wakati wazabuni kiasi cha kutishia mitaji yao. Lakini kwa nyakati hizi kumeibuka tatizo kubwa hata kwa taasisi binafsi kutolipa wazabuni kwa wakati au kuwadhulumu kabisa. Utakuta shule binafsi inamwambia kijana mwenye steshenari awapelekee vifaa fulani vya shule kwa makubaliano kwamba wakifikisha mzigo watalipwa ila matokeo yake kunatokea uzungushwaji kiasi kwamba kama kijana alikopa anajikuta matatani na kuonekana tapeli.

Isitoshe huu utaratibu wa taasisi binafsi kutumia majina yao kuwarubuni wazabuni unatumika na baadhi ya wamiliki kupunguza gharama za uendeshaji wa taasisi zao bila kujali maumivu ya wengine. Mtu kama una taasisi tafadhali lipa vijana wakishafanya kazi yako. Ni upuuzi mtu anafanya kazi dola ikiwa Tsh 2300 anakuja kulipwa dola ikiwa Tsh 2600. Hiyo ni hasara.

Taasisi za serikali sitaki kuziongelea sana kwa leo kwasababu zinajulikana jinsi nyingi zilivyo vichomi hasa mashule. Tafadhali tusapoti vijana kwa kulipa mapema badala ya kuwalipa kwa taabu.

Bila kuwataja tra, Polisi, Latra, ewura, Tcra, na wa namna hiyo watadhani ujumbe wako hauwahusu.

Gao ndugu ni kichomi. wameuwa biashara nyingi za watu.

Ni mzigo na hawana ubunifu wala weledi katika uendeshaji biashara au shughuli zozite za uzalishaji mali.
 
Back
Top Bottom