Serikali yasaini mikataba ya Tsh. Bilioni 43.3 kuboresha Taasisi 661 ili kurahisisha Huduma kwa Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeingia mikataba miwili yenye thamani ya Shilingi Bilioni 43.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kimtandao kwenye Taasisi 661 za Serikali ili kurahisisha huduma kwa Wananchi ambao walikuwa wanakutana na changamoto kubwa wanapohitaji huduma kwenye ofisi za Serikali Mijini na Vijijini.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mohamed Abdulla amezungumza baada ya kusaini mikataba hiyo kwa kusema “Usimikaji wa vifaa Nchi nzima, kituo cha uangalizi wa Mtandao na Vifaa vya kuunganisha taasisi za kiserikali zaidi ya 661 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali.”

Kwa upande wake Katibu Mkuu Baraza la Taifa la Biashara, Dkt Godwill Wanga anasema “Kuhudumia Wafanyabiashara na wawekezaji Nchini, kuelimisha umma juu ya matumizi ya teknolojia, kurahisisha mfumo wa malipo, kuonesha fursa za kidijiti ambazo zitasaidia kuimarisha uchumi.”

Naye Jackline Woiso ambaye ni Mjumbe wa Kikosi Kazi anasema “Kikubwa tunachoenda kufanya ni kurahisisha huduma za TEHAMA kwa Wananchi ambazo zitawasaidia kujiingizia kipato.”
 
Back
Top Bottom