KWELI Baadhi ya raia wa Afrika Kusini kuwataka wageni kuondoka nchini mwao

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaji mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi Machi 2023.

Nchi zetu hususan Tanzania zinapaswa kuhakikisha usalama kwa raia wao wanaoishi kule kihalali na ikiwezekana kuweka utaratibu wa kuwaondoa raia wake Afrika ya Kusini.

Matishio haya yamekuwa yakifanyika bila hatua zozote kuchukuliwa, hivyo inawezekana baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola vya Afrika ya Kusini ni wahusika wa hizi operesheni dhidi ya wageni.

Hatulipi ubaya kwa ubaya bali kumtenga mtu mbaya ni sehemu ya kumpa fundisho dhidi ya mtenda ubaya. Ni wakati sasa wa Nchi za SADC kuitenga Afrika ya Kusini na ikiwezekana Umoja wa Afrika (AU) kuiwekea vikwazo mpaka mamlaka zitakapoondoa vitisho dhidi ya usalama wa wageni ndani ya nchi hiyo.

_128690781_bbcm_south_africa_country_profile_map_200223.jpg
 
Tunachokijua
Mwanzoni mwa mwezi Mei 2022 kulitokea machafuko Afrika Kusini juu ya raia wa kigeni wanaoishi nchini humo ambapo vikundi mbambali vilijiunga ili kuhakikisha wanawafukuza raia wote wa kigeni wakidai kuwa raia wa kigeni ndio chanzo cha matatizo mbambali ikiwemo wizi, ubakaji, umaskini na ajira.

Umaskini ni moja ya sababu kuu za migogoro hiyo, huku Waafrika Kusini mara kwa mara wakiwashutumu wahamiaji kwa kuchukua kazi zao.

Kutokana na tukio la ubakaji la wanawake nane limeongeza chuki zaidi kwa wageni kutokana kukamatwa Zaidi ya 100 wengi wao wakiwa ni wageni ambapo Raia wengi wa Afrika kusini wameamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuwafakuza wageni pasipo kuaangalia sheria za uhamiaji.

Wahamiaji haramu na wahamiaji wa kisheria wote wameekwa kundi moja. Baadhi ya raia wa Afrika Kusini wameanzisha kikundi kiitwacho “Operation Dudula” ikimaanisha fukuza wageni ambapo wamelenga kufukuza wageni wote kuzunguka nchi yote.

Pia kikundi kingine kinaitwa “Khala Mntwana” wametaka wageni wote ambao hawatambuliki kisheria warudi mara moja nchini kwao ambapo kiongozi wao Veli Madodo aliwaambia DW raia inabidi wachukue sheria mkononi kwasababu serikali imeshindwa kufanya lolote
Hawa wasauzi wamezidi aiseee. Kwanini tusiwatinue na sisi huku kwetu...Inashangaza sana nchi iliyomo Africa kubaguana ili hali sisi tulimficha mandela wao hapo morogoro kipindi cha harakat za uhuru wa nchi yao.
 
Hawa wasauzi wamezidi aiseee....Kwanini tusiwatinue na sisi huku kwetu...Inashangaza sana nchi iliyomo Africa kubaguana ili hali sisi tulimficha mandela wao hapo morogoro kipindi cha harakat za uhuru wa nchi yao
Hiyo wanaweza wanaijeria tu
 
Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaji mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi Machi 2023.

Nchi zetu hususan Tanzania zinapaswa kuhakikisha usalama kwa raia wao wanaoishi kule kihalali na ikiwezekana kuweka utaratibu wa kuwaondoa raia wake Afrika ya Kusini.

Matishio haya yamekuwa yakifanyika bila hatua zozote kuchukuliwa, hivyo inawezekana baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola vya Afrika ya Kusini ni wahusika wa hizi operesheni dhidi ya wageni.

Hatulipi ubaya kwa ubaya bali kumtenga mtu mbaya ni sehemu ya kumpa fundisho dhidi ya mtenda ubaya. Ni wakati sasa wa Nchi za SADC kuitenga Afrika ya Kusini na ikiwezekana Umoja wa Afrika (AU) kuiwekea vikwazo mpaka mamlaka zitakapoondoa vitisho dhidi ya usalama wa wageni ndani ya nchi hiyo.

View attachment 2327394
Hii in hatari Sana ndugu zangu🥺🥺
 
Hawa wasauzi wamezidi aiseee. Kwanini tusiwatinue na sisi huku kwetu...Inashangaza sana nchi iliyomo Africa kubaguana ili hali sisi tulimficha mandela wao hapo morogoro kipindi cha harakat za uhuru wa nchi yao.
Waambieni ndg zenu warud huku bongo kwasasa ajira kibao mama anaupiga mwingi. Dr Bashiru
 
Hawa wasauzi wamezidi aiseee. Kwanini tusiwatinue na sisi huku kwetu...Inashangaza sana nchi iliyomo Africa kubaguana ili hali sisi tulimficha mandela wao hapo morogoro kipindi cha harakat za uhuru wa nchi yao.
Tafuta pesa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom