Nani ni nani katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli?

Lior

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
766
1,957
Wakati Afrika ya Kusini ikimtegemea John Dugard, aliyewahi kufanya kazi Umoja wa Mataifa, Israeli wamepitisha jina la Malcom Shaw, kutoka Uingereza kuongoza majopo yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

1705290826184.png

Muonekano wa chumba ndani ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, huko The Hague Uholanzi. Picha: ICJ Na Sylvia Chebet TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Magwiji wa sheria na wataalamu wengine kutoka mashirika makubwa ya kimataifa wameanza kupimana mbavu katika shauri la Afrika Kusini dhidi ya Israeli ambalo limeanza kusikilizwa kwenye Mahakama hiyo, iliyoko The Hague, Uholanzi.

Katika jalada lenye kurasa 84 la shauri hilo, Afrika Kusini inaishutumu Israeli kwa mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Msingi wa kesi yake upo katika maelezo kamili ya vitendo vya mauaji ya Israel kufuatia shambulio dhidi ya kundi la Hamas, lillitokea Oktoba 7, mwaka jana.

Kesi hiyo inaangazia mauaji na uharibifu mkubwa uliofanywa na Israeli, ikiwa ni pamoja na kuikatia mji wa Gaza, huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji, chakula, dawa na mafuta.

Katika kesi hiyo, Afrika ya Kusini imeazimia kukomesha mashambulizi ya kijeshi ya Israeli ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 23,000, wakiwemo watoto 10,000.

Pande zote mbili ziliwasilisha hoja zao mbele ya majaji mjini The Hague . Jopo la majaji 17, linategemewa kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya shauri hilo kwenye mahakama hiyo.

"Madhali hili ni suala la kisiasa, kila hoja itakuwa na uzito wake kwenye maamuzi haya," mtaalamu wa sheria Nabil Orina anaiambia TRT Afrika, akiongeza kuwa "majaji tisa zaidi watahitajika kukamilisha akidi." Wafuatao, ndio wataalamu wa sheria watakaounda timu kutoka pande zote.

Afrika ya Kusini

John Dugard, mtumishi wa zamani wa Umoja wa Mataifa ndiye atakayeongoza jopo la Afrika ya Kusini.

Mbobezi wa Sheria za Kimataifa kutoka Afrika ya Kusini, Dugard ana uzoefu na ICJ, baada ya kuhudumu kama jaji wa muda mwaka 2008.

Dugard amekuwa wazi kukosoa vikali vitendo vya Israel, akisema kuwa, "Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na baraza lake la mawaziri wanahusika na kutekeleza anachokiita uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na, pengine, uhalifu wa mauaji ya kimbari."

Wataalamu wengine wa sheria kwa upande wa Afrika Kusini ni pamoja na Wakili Mwandamizi Adila Hassam, Tembeka Ngcukaitobi, na wakili wa kimataifa Max Du Plessis.

Kikosi cha Afrika Kusini kinachoongezwa nguvu na Blinne Ni Ghralaigh kutoka Ireland na Muingereza Vaughan Lowe. Timu itawajumuisha pia wakili wengine wakiwemo Tshidiso Ramogale, Sarah Pudifin-Jones na Lerato Zikalala.

Timu ya Utetezi kutoka Israeli

Israel imemchagua wakili wa Uingereza Malcolm Shaw kuiwakilisha katika mahakama ya ICJ.

Shaw anatajwa kama mmoja ya wataalamu wa sheria za kimataifa na amewahi kutetea kesi hapo The Hague.

Muingereza huyo amejijengea jina kwa kutoa ushauri kuhusu migogoro ya kimaeneo; sheria ya bahari; haki za binadamu; kujitawala, usuluhishi wa kimataifa,” hii ni kwa mujibu wa wasifu wake uliohifadhiwa katika makabrasha ndani ya mahakama ya Essex, Kusini-Mashariki mwa Uingereza.

Kwa nyakati tofuauti, Shaw pia amehusika kutoa ushauri wa kisheria kwa nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Ukraine na Serbia.

Mbali na ICJ, Shaw amewahi pia kuhusika katika kesi katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, Mahakama ya Haki ya Ulaya, na Mahakama nyingine kubwa duniani.

Nguli huyo pia anatajwa kuwa mmoja wa mawakili wanne, kuiwakilisha Israeli katika vikao vya ICJ, japo majina na wasifu wa mawakili bado haujawekwa wazi.

Jopo la Waamuzi

ICJ inaundwa na majaji 15 waliochaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kwa ajili ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka tisa.

Kulingana na sheria na miongozo ya ICJ, nchi ambayo inahusika na kesi na haina Jaji katika jopo hilo, ina wajibu wa kupendekeza Jaji wa muda, kama ilivyotokea kwa Afrika ya Kusini na Israeli.

Ni kwa muktadha huo, Afrika ya Kusini imemteua Dikgang Moseneke, aliyekuwa naibu wa Jaji Mkuu nchini humo na gwiji wa masuala ya kisheria, wakati Israeli ilimchagua Aharon Barak, Rais wa zamani wa Mahakama Kuu wa nchi hiyo.

Pia alitetea uamuzi wa Israeli wa kujenga ukuta wa kujitenga kupitia Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kufuatia uamuzi wa 2004 wa ICJ kutangaza kuwa ni kinyume cha sheria.

Majaji wengine 15 wa mahakama hiyo wanatoka nchi tofauti.
Joan Donoghue - Marekani ndiye rais wa mahakama hiyo huku Kirill Gevorgian - Urusi akiwa makamu wa rais.

Kutoka Afrika, jopo hilo linaundwa na Abdulqawi Yusuf kutoka - Somalia, Julia Sebutinde - Uganda na Mohamed Bennouna - Mmorocco.

Majaji wengine wa ICJ ni pamoja na Xue Hangin - China, Peter Tomka - Slovakia, Ronny Abraham -France, Mbrazili Leonardo Nemer Caldeira Brant, Dalveer Bhandari wa India, Patrick Lipton Robinson wa Jamaica, Hilary Charlesworth wa Australia, Nawaf Salam wa Lebanon, Yuji Iwasawa wa Japan na Mjerumani Georg Nolte.

SWALI: Kwa maoni yako ni timu gani itaibuka mshindi kutokana na wasifu wa kila mmoja?

Source: TRT Africa
 
Kipigo kiko pale pale, magaidi 3,000 wa dini waliingia Israel wakiwa na nia ya kufuta Wayahudi kama jinsi dini yao imeamrisha.
Baada ya kudhibitiwa, wakateka watu na kwenda kujificha ndani ya akina mama na watoto, huku bado wakiendelea kufyatua makombora kwenda Israel, hapakuwa na jinsi ila kuwapiga popote walipo, bado wanapigwa, yule alla Akbar wao amewakimbia, hata Iran na Waarabu wameshindwa kuwasaidia.
 
Kipigo kiko pale pale, magaidi 3,000 wa dini waliingia Israel wakiwa na nia ya kufuta Wayahudi kama jinsi dini yao imeamrisha.
Baada ya kudhibitiwa, wakateka watu na kwenda kujificha ndani ya akina mama na watoto, huku bado wakiendelea kufyatua makombora kwenda Israel, hapakuwa na jinsi ila kuwapiga popote walipo, bado wanapigwa, yule alla Akbar wao amewakimbia, hata Iran na Waarabu wameshindwa kuwasaidia.
Jikite kwenye swali ndugu. Soma kuelewa sio kujibu
 
Kesi zenyewe za ICJ hazina impacts yoyote,labda records tu kwamba taifa fulani lilifanya kitu fulani
Tusiangalie impact ya kesi, tuangalie umahiri wa hao wana sheria, je nani atamgalagaza mwenzake kwa hoja nzito?
 
Hapo washinde au washindwe hakuna jipya maana hayo maamuz yanabaki kabatini tu nothing more
Nimeuliza kwa hao wanasheria wawili nguri, mchuano wao nani atamzidi mwingine bila kuangalia impact ya kesi.
 
Tanzania tunafeli sana! Paramagamba hivi yuko wapi ?

Israel wana akili kubwa, hata japo hiyo vita wameanza wao lakini pia kesi watashinda.

IQ yao iko vizuri.
 
Tanzania tunafeli sana! Paramagamba hivi yuko wapi ?

Israel wana akili kubwa, hata japo hiyo vita wameanza wao lakini pia kesi watashinda.

IQ yao iko vizuri.
Kwa hiyo John Dugard atagalalagwa na Malcom Shaw.

Huyo paramagamba 😂 nimecheka sana
 
Kesi hii itakuwa na Historia ya Afrika kusini kusimama kwa ajili ya nchi nyingine.
Kabla ya kuliweka jambo hili labda na sisi tuone umuhimu au kitokuwepo umuhimu wa kufanya hivyo.
1. Je ICJ ina mamlaka ya kutekeleza maamuzi yake kwa kutumia chombo kipi? Mfano ka SA akishinda Israel atawajibishwa na nani kwa kufanywa nini? Kama hakuna basi ninaina nyingine ya upotezaji wa rasilimali na kujijengea popuratilty tu ya wahusika amabo haina faiida kwa wahanga wa tukio.

2. Je SA ameona ni Palestine tu ambaye anasitahili kutetewa katika majanga ya uonezi yanayoendelea hususan katika Afrika yetu? Je wanasheria hawaini ukiukwaji wa haki za kiraia dhidi ya serkali zao zilizopo madarakani kwa wizi na ufisadi? Au hili liko nje ya sheria ? Je hawaoni kinachotokea DRC , Somalia na maeneo mengine ambako raia wengine wamefanywa wakimbizi. Au ni mihemiko ya vyombo vya habari ambavyo hurusha taarifa kwa malengo yao?.

3. Je sheria za kivita za kujihami na ingagement zinasemaje ikiwa utashambuliwa na adui akiwa kwenye makasi ya raia , shule au sehemu zinazofanana ha hizo?. Yaani IDF ilitakiwa itendeje pale raia wake wakiwa wamechukuliwa mateka na kuingizwa kwa namna ya kivamiza cha Kijeshi? Je ingetumia diplomasia na si njia ya kijeshi?.

4. Hamas ambayo ina mamlaka ya Gaza na chama na wanaharakati wenye mafunzo ya kijeshi wenye ushawishi kwa raia wana wajibu juu ya kutumia maeneo ya raia kama sehemu za mashambulizi? Au raia wa Gaza walitakiwa kutoa ushirikiano na IDF?

Mwisho naamini hiyo kesi ni ya kuongeza CV kwa kila upande lkn haitakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa upande wowote
 
Back
Top Bottom