Baada ya Utawala wa Magufuli, nini kitatokea?

Baada ya Utawala wa Magufuli, nini kitatokea?

Awamu ya tank wabomoa nchi. Tunahitaji reconstruction baada ya hao jamaa kuikimbia nchi. Kwani uwezekano wa kuendelea kubaki hapa tz baada ya kuumiza wayu wengi no mdogo sana
Kwanini wakimbie nchi yao...waliofanya mazuri ni mengi na kama binadamu...wanamapungufu yao pia kama awamu zilizopita..kikubwa Kwa watanzania Ni kuendelea kupendana
Vibaraka wa Jiwe Makonda, Musiba, Hapi, Chalamila, Lucy Msafiri, Jeri Muro,Gambo, Mnyeti Musiba, Lugola, Waitara, Lemutuz, Musukuma, Lusinde sijui watakimbilia wapi?
Kikumbwa hakuna mtanzania atakimbia nchi yake...waliofanya mazuri ni mengi ila kama binadamu wana mapungufu yao pia..Ni wakati mwafaka sasa Kwa utawala huu...kama wanamapungufu ya kuwaleta watu pamoja wakayafanyia kazi nayo mapungufu...Kikubwa watanzania wenzangu...tuendelee kupendana..na kusameana Tanzania Ni yetu sote.tusibaguane Kwa misingi ya ukabila,ukanda au dini...na tumkatae Kwa nguvu zetu zote mtu anayetaka kupandikiza mbegu ya ubaguzi katikati yetu..Kuna minong'ono ya ubaguzi wa watu wa jamii fulani ipo Kwa nguvu sana chinichini...ila Mimi siamini katika...hilo..ninaamini watanzania bado Ni wamoja na wataendelea kuwa wamoja..tusipandikize chuki na maneno yasiokuwepo...ila kama yanayosemwa kweli yapo Ni wakati wa kuyapiga vita yasije yakaota mizizi..Mungu ibariki Tanzania na watu wake...
 
Kadri siku zinavyoenda ubaya ,visasi,utengano na husda baina ya jamii yetu iliyojengewa umoja na upendo hali inaendelea kua tete. Si wale wapinzani ata wanaccm ,wote wamepata kuonja machungu haya.
Ni kiongozi mkabila na fisadi kuwahi kutokea hafai kabisa.
Kuna uwezekano mkubwa Taifa likaingia kwenye visasi baada ya awamu hii kumaliza muda wake. Kuna uwezekano watu wakawa wanashinda kwenye benchi za mahakama au polisi kwasababu ya visasi na hali inayojengwa mioyoni mwao.

Si kwamba namtishia uhai au amani kama yeye anavyo watishia Watanzania wenzie ( Cyprian Moja) anawakirisha wengi ambao hawana kinga yoyote baada ya utawala huu. Lakini bado atujachelewa kuyamaliza au kuachana na huu upuuzi.

Maana sitaki kusikia kua nasi nitafika siku tuwe na GACHACHA za kule Rwanda bali tunaweza tukatibu ili gonjwa nyemelezi mapema.

Mh.Dr. J.P. Magufuli ,wewe ndiye Rais wa nchi hii ...naomba tu ebu simama katika uongozi,katika haki,busara,hekima kama mwalimu uwezi kukemea mambo aya,tulete watanzania pamoja,tuunganishe maana sisi ni baba na mama mmoja.

Tusisubiri kutibu ugonjwa wakati tunaweza kutumia kinga na ugonjwa huu usitupate sisi watanzania.

Tumezaliwa apa Tanzania, tumelelewa na kusomesea apa Tanzania, makaburi ya wazee wetu yapo apa Tanzania.

Familia zetu zipo apa Tanzania, tumefundishwa upendo,umoja,mshikamano kama moja ya nguzo muhimu za ustawi wa Tanzania na jamii zote.

Mh.Dr.Magufuli ,tusikubari kugawanywa kisa itikadi,kisa wanaharakati nk....NINI KITATOKEA BAADA YA AWAMU YA TANO
 
Huu uzi naona umeanza kutuonyesha mambo
 
Waizi wa rasilimali za Taifa, walafi na waliojilimbikizia Mali Kwa kutumia madaraka yao watalia na kusagana Meno.
 
Wana Jf binafsi natazama kwa jicho la taaluma hivi ni Nani ? Anaweza kutuvusha wote JPM na TAL wanafanya kazi ya siasa lakini bila Shaka tuangalie ni yupi mwenye Record za kutuvusha , maana maisha yanahitaji kuwa balanced , UCHUMI, MAISHA BINAFSI , MAENDELEO , AMAN , UTULIVU , KUFURAHI, KUABUDU , KULA KUSHIBA , KUIA NA KUOLEWA , na Kila aina ya kinachotakiwa lakini tusiache kuwaza juu ya MAGUMU kwa maana hakuna sehemu isiyokuwa na changamoto mtu mmoja akasema for every successful person have a painful story .

DONDOSHA MAONI YAKO Nani tumpe nchi kwa kuzingazitia kafanya Nini ? Lini ? Kwa ajili ya Nani ?

Wote tumpe kura
 
huyo engineer wako kama hakuivusha kwa miaka mitano hataweza kuivusha tena.
Mahaba ni kitu kizuru lakini yakizidi hupofusha-huyu engineer umemtoa wapi Jabulani? JPM ni Chemist.
 
Kura yangu ni kwa Tundu Antiphas Lissu na sababu ni hizi

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!
 
Japo hili ni swali muhimu sana, jibu lake ni simple, kulikuwa na awamu ya kwanza ikapita ikaja awamu ya pili nayo ikapita ikaja awamu ya tatu hivyo hivyo hadi sasa ni awamu ya tano nayo itapita, kitakachofuata baada ya awamu ya tano kuisha, itaingia awamu ya Sita, kila zama na zama zake.
P
Sema awamu ya sita inaingia kutokea cdm, usione haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya awamu ya 5 :

Wapo watakaoikimbia TZ,

Wapo watakaoanzisha fujo na vurugu ili kuonesha kuwa awamu ya 5 ilitenda vyema.

Mahakama na mahabusu zitaongeza wateja.

Ukanda na Ukabila utatamalaki.

Miradi mingi isiyo na tija itasimama na kutengeneza hasara kubwa ambayo haijawahi tokea tangu TZ ipate Uhuru.

Wakulima na Wafanyakazi watarejeshewa matumaini ya kuwa na maisha bora (siyo bora maisha ya awamu ya 5 )

Amani, upendo, mshikamàno na udugu wa waTZ utarejea tena.

Haitatokea tena watu kutekwa, kuteswa, kuuawa, kupotezwa au KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA.

Haitatokea tena Watu kutishwa na kutiwa hofu kama pichani hapo chini.

Wakulima hawatakopwa tena na serikali.
Pongezi sana mkuu kwa comment mzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadri siku zinavyoenda ubaya ,visasi,utengano na husda baina ya jamii yetu iliyojengewa umoja na upendo hali inaendelea kua tete. Si wale wapinzani ata wanaccm ,wote wamepata kuonja machungu haya.

Kuna uwezekano mkubwa Taifa likaingia kwenye visasi baada ya awamu hii kumaliza muda wake. Kuna uwezekano watu wakawa wanashinda kwenye benchi za mahakama au polisi kwasababu ya visasi na hali inayojengwa mioyoni mwao.

Si kwamba namtishia uhai au amani kama yeye anavyo watishia Watanzania wenzie ( Cyprian Moja) anawakirisha wengi ambao hawana kinga yoyote baada ya utawala huu. Lakini bado atujachelewa kuyamaliza au kuachana na huu upuuzi.

Maana sitaki kusikia kua nasi nitafika siku tuwe na GACHACHA za kule Rwanda bali tunaweza tukatibu ili gonjwa nyemelezi mapema.

Mh.Dr. J.P. Magufuli ,wewe ndiye Rais wa nchi hii ...naomba tu ebu simama katika uongozi,katika haki,busara,hekima kama mwalimu uwezi kukemea mambo aya,tulete watanzania pamoja,tuunganishe maana sisi ni baba na mama mmoja.

Tusisubiri kutibu ugonjwa wakati tunaweza kutumia kinga na ugonjwa huu usitupate sisi watanzania.

Tumezaliwa apa Tanzania, tumelelewa na kusomesea apa Tanzania, makaburi ya wazee wetu yapo apa Tanzania.

Familia zetu zipo apa Tanzania, tumefundishwa upendo,umoja,mshikamano kama moja ya nguzo muhimu za ustawi wa Tanzania na jamii zote.

Mh.Dr.Magufuli ,tusikubari kugawanywa kisa itikadi,kisa wanaharakati nk....NINI KITATOKEA BAADA YA AWAMU YA TANO
Sahihisha.

Ondoa title ya "Eng" kwa Magufuli, na ondoa tile ya "Msomi" kwa Lissu. Ingawa Lissu amesoma sana lakini siyo msomi kuliko Magufuli kwani naye amesoma sana, halafu Magufuli ni mkemia siyo siyo injinia.

Hakuna siku Lissu amesimama jukwani bila kumtaja Magufuli, na Magufuli hajawahi kumtaja Lissu katika mikutano yake hata siku moja labda kwa Lissu kujihisi tu; ni nani kati yao ananadi visasi?

Kampeini za Lissu zilianza vibaya kwa kuwa too personal badala ya kujikita kwenye sera; anakuja kuanza baada ya kuwa ameshapanda mbegu za chuki. Yeyote mwenye akili timamu anajua kuwa kampeini za Lissu ni against Magufuli personally kwani alianza hiyo zamani sana kabla hajarudi Tanzania.
 
Hapa ndiyo namkumbuka JK Nyerere. Alimzuia Ali Hassan Mwinyi asibadili Katiba kuongeza ukomo wa kutawala ambao Mwinyi alikuwa anautaka kwa kupitia midomo ya wapambe. Lakini vike vile alizuia kupata viongozi wabovu kama Malecela, Kolimba na Lowassa.

Sasa hivi hatuna Nyerere. Ninachokiona tunahitaji Mungu tu atunusuru kutoka kwenye huu mtego. Tupate mrithi ambaye ni 'sober' na ambaye hatokani na msukumo wa Jiwe. Amini usiamini kwa hali iliyopo ya kuvunja katiba Jiwe anaweza kumuachia Bashite.

Akitoka kwenye kambi hasimu za CCM yaweza kuwa shida kubwa. Imagine mtu kama Membe anakuwa Rais, hiyo revenge itakuwa balaa.

Upinzani umetendewa vibaya sana katika historia ya nchi yetu. Naamini wakishinda immediately baada ya Jiwe revenge itakuwa mbaya sana. Hebu pata picha Tundu Lissu anakuwa Rais na Mbowe PM, hapatakalika.

Kwa hiyo tunahitaji sampuli kama za akina Jaji Agustino Ramadhani, Prof Mark Mwandosya, Dr Bilal au hata Nahodha. Sampuli ya watu nje ya mfumo uliopo madarakani sasa hivi na uliopo upinzani ndiyo wanaweza kuleta maridhiano ya kitaifa.

JPM aondoke hata 2020 kwa kuwa anajenga uadui sana kati ya Watanzania
Kwahiyo ile slogan yetu ya kisiwa cha amani imesha toweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom