Baada ya Utawala wa Magufuli, nini kitatokea?

Baada ya Utawala wa Magufuli, nini kitatokea?

Mbona mambo ya nakwenda vizuri

Ninyinyi watu wachache mafisadi ndio mambo yenu yamesimama kwa sababu wazururaji

Ndio maana mnaona kuwa mambo hayaendi dickhead
Wewe mwenyewe huna uhakika wa kupata mlo mmoja wa siku, usikute unashindia kashata na maji ya kandoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya utawala wa magufuli ritutashuhudia:

1. Kukua kwa uchumi kwa kasi zaidi kwa kuwa miundombinu ya kuwezesha uchumi huo kufikiwa yanaboreshwa na kutengenezwa sasa. Na hii ndio legacy ambayo itakumbukwa juu ya utawala wa magufuli kwa miaka mingi.

2. Kukua na kuenea kwa kasi dhana na falsfa ya kujitegemea kwa nchi kwa vizazi vingi vijavyo. Falsafa hiyo imepata uhai mpya chini ya utawala wa Magufuli.

3. Vitendo vya wizi, ukabaji, ubakaji, ujambazi na uhalifu wowote mwingine utakuwa umepungua na kuweza kuisha kabisa. Hii ni kwa sababu watu wenye matendo hayo wanadhibitiwa sana chini ya utawala wa Magufuli.

4. kujengeka kwa mifumo imara ya kitaasisi ambayo ina nguvu ya kudhibiti na kuzuia uhalifu,wizi, ufisadi, rushwa na mienendo miovu katika jamii, sehemu za kazi n.K

5. Kujengeka kwa taifa lenye wazalendo halisi wa nchi yao na kuondokana na taifa la kianaharakati linachochea machafuko ,fujo,migomo na maandamano isiyo na tija wala umuhimu.

Hiyo ndio Tanzania baada ya Magufuli . kama huu uzi uishivyo naomba na comment hii idumu ili miaka 50 ijayo watoto na wajukuu zetu wasome hii comment.
Upotolo mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh Tundu Lisu ndio mwenye kuliweza hili jukumu la kutuvusha salama. Huyu bulldozer wako alishafeli tangu mwaka wa kwanza hadi huu wa tano

Jitu linacheza na hazina ya taifa kama vile alitafuta yeye! Haheshimu bunge, haheshimu mahakama, haheshimu NEC, hatuheshimu sisi watanzania tuliomuajiri na bado anazidi kutufokea kama povu la mbege.

Ule uwanja wa chato ilitakiwa bajeti yake ipitishwe bungeni lakini yeye anatoa oda kipumbavu kabisa bila kufuata taratibu.
Baada ya hapo anampa tenda ndugu yake badala kuwepo ushindani.... Kibaya kabisa kwenye hazina ya taifa kaweka tena mtoto wa dada yake hivyo nchi inaendeshwa kihunihuni tu. Nani ampe kura huyu mharibifu?
Tangu aingie madarakani watu walio kinyume na mawazo yake wamekuwa wakipoteza, kubambikiwa kesi, kuwa kwenye hatihati ya kuondolewa uraia, kufilisiwa na maovu mengine mengi.

Kageuza taifa kuwa la kinafiki kwa kiwango cha ajabu! Vyombo vya habari kavigeuza vyakwake mwenyewe, NEC na mahakama ndio usiseme.
 
Kitachofuata ni kazi na bata tu maana hamna namna ingine. Unless huyo raisi ajaye awe hajakulia bongo na kushuhudia ugumu wa maisha kwa awamu hii ya 5! 🤣🤣🤣🤣🤣

Natabiri ufisadi wa kutisha na watu kujilimbikizia mali na hali itakuwa mbaya zaidi kuliko awamu ya 4! Watu wana hasira mtu akipata pa kupiga atakuwa anachapa hela zote.
 
Kadri siku zinavyoenda ubaya ,visasi,utengano na husda baina ya jamii yetu iliyojengewa umoja na upendo hali inaendelea kua tete. Si wale wapinzani ata wanaccm ,wote wamepata kuonja machungu haya.

Kuna uwezekano mkubwa Taifa likaingia kwenye visasi baada ya awamu hii kumaliza muda wake. Kuna uwezekano watu wakawa wanashinda kwenye benchi za mahakama au polisi kwasababu ya visasi na hali inayojengwa mioyoni mwao.

Si kwamba namtishia uhai au amani kama yeye anavyo watishia Watanzania wenzie ( Cyprian Moja) anawakirisha wengi ambao hawana kinga yoyote baada ya utawala huu. Lakini bado atujachelewa kuyamaliza au kuachana na huu upuuzi.

Maana sitaki kusikia kua nasi nitafika siku tuwe na GACHACHA za kule Rwanda bali tunaweza tukatibu ili gonjwa nyemelezi mapema.

Mh.Dr. J.P. Magufuli ,wewe ndiye Rais wa nchi hii ...naomba tu ebu simama katika uongozi,katika haki,busara,hekima kama mwalimu uwezi kukemea mambo aya,tulete watanzania pamoja,tuunganishe maana sisi ni baba na mama mmoja.

Tusisubiri kutibu ugonjwa wakati tunaweza kutumia kinga na ugonjwa huu usitupate sisi watanzania.

Tumezaliwa apa Tanzania, tumelelewa na kusomesea apa Tanzania, makaburi ya wazee wetu yapo apa Tanzania.

Familia zetu zipo apa Tanzania, tumefundishwa upendo,umoja,mshikamano kama moja ya nguzo muhimu za ustawi wa Tanzania na jamii zote.

Mh.Dr.Magufuli ,tusikubari kugawanywa kisa itikadi,kisa wanaharakati nk....NINI KITATOKEA BAADA YA AWAMU YA TANO
NI YEYEEEEEEEEEEEEEE
 
Kura yangu ni kwa Tundu Antiphas Lissu na sababu ni hizi

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!
Ningekuwa na uwezo ningekupa 1 million likes lkn basi tu. 🙏 🙏🙏
 
Sahihisha.

Ondoa title ya "Eng" kwa Magufuli, na ondoa tile ya "Msomi" kwa Lissu. Ingawa Lissu amesoma sana lakini siyo msomi kuliko Magufuli kwani naye amesoma sana, halafu Magufuli ni mkemia siyo siyo injinia.

Hakuna siku Lissu amesimama jukwani bila kumtaja Magufuli, na Magufuli hajawahi kumtaja Lissu katika mikutano yake hata siku moja labda kwa Lissu kujihisi tu; ni nani kati yao ananadi visasi?

Kampeini za Lissu zilianza vibaya kwa kuwa too personal badala ya kujikita kwenye sera; anakuja kuanza baada ya kuwa ameshapanda mbegu za chuki. Yeyote mwenye akili timamu anajua kuwa kampeini za Lissu ni against Magufuli personally kwani alianza hiyo zamani sana kabla hajarudi Tanzania.
Mkuu kweli unajibu hii thread au umejichanganya?
Maana hii thread wala aiongelei kampeini na imekuwemo humu siku nyingi ata kampeini azijaanza kufikiriwa
 
Mkuu kweli unajibu hii thread au umejichanganya?
Maana hii thread wala aiongelei kampeini na imekuwemo humu siku nyingi ata kampeini azijaanza kufikiriwa
Samahani hiyo post haikutakiwa iwe kwenye thread hii; nadhani ni kutokana na kusoma thread nyingi kwa wakati mmoja ndipo jibu la thread moja likaingia kwenye thread nyingine. Kulikuwa na thread inahusu mpambano na visasi baina ya "Dr. Eng. Magufuli" na "Wakili msomi Lissu" ndiyo nilikuwa najibu.
 
Japo hili ni swali muhimu sana, jibu lake ni simple, kulikuwa na awamu ya kwanza ikapita ikaja awamu ya pili nayo ikapita ikaja awamu ya tatu hivyo hivyo hadi sasa ni awamu ya tano nayo itapita, kitakachofuata baada ya awamu ya tano kuisha, itaingia awamu ya Sita, kila zama na zama zake.
P
Ndugu alie rudisha huu Uzi ahsante sana.
Kaka mkubwa nadhani sasa majibu yako sio sahihi kwa Uzi huu ....Tujifunze kuishi
 
Kitachofuata ni kazi na bata tu maana hamna namna ingine. Unless huyo raisi ajaye awe hajakulia bongo na kushuhudia ugumu wa maisha kwa awamu hii ya 5! 🤣🤣🤣🤣🤣

Natabiri ufisadi wa kutisha na watu kujilimbikizia mali na hali itakuwa mbaya zaidi kuliko awamu ya 4! Watu wana hasira mtu akipata pa kupiga atakuwa anachapa hela zote.
Wewe jamaa umepiga mule mule.
Japo hatuli bata kama ulivyosema
 
Back
Top Bottom