Baada ya Utawala wa Magufuli, nini kitatokea?

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,272
2,419
Kadri siku zinavyoenda ubaya, visasi, utengano na husda baina ya jamii yetu iliyojengewa umoja na upendo hali inaendelea kuwa tete. Si wale wapinzani hata wanaccm, wote wamepata kuonja machungu haya.

Kuna uwezekano mkubwa Taifa likaingia kwenye visasi baada ya awamu hii kumaliza muda wake. Kuna uwezekano watu wakawa wanashinda kwenye benchi za mahakama au polisi kwasababu ya visasi na hali inayojengwa mioyoni mwao.

Si kwamba namtishia uhai au amani kama yeye anavyowatishia Watanzania wenzie (Cyprian Moja) anawakilisha wengi ambao hawana kinga yoyote baada ya utawala huu. Lakini bado hatujachelewa kuyamaliza au kuachana na huu upuuzi.

Maana sitaki kusikia kuwa nasi nitafika siku tuwe na GACHACHA za kule Rwanda bali tunaweza tukatibu ili gonjwa nyemelezi mapema.

Mh. Dr. J.P. Magufuli, wewe ndiye Rais wa nchi hii ...naomba tu ebu simama katika uongozi,katika haki,busara,hekima kama mwalimu uwezi kukemea mambo aya,tulete watanzania pamoja,tuunganishe maana sisi ni baba na mama mmoja.

Tusisubiri kutibu ugonjwa wakati tunaweza kutumia kinga na ugonjwa huu usitupate sisi watanzania.

Tumezaliwa apa Tanzania, tumelelewa na kusomesea apa Tanzania, makaburi ya wazee wetu yapo apa Tanzania.

Familia zetu zipo apa Tanzania, tumefundishwa upendo,umoja,mshikamano kama moja ya nguzo muhimu za ustawi wa Tanzania na jamii zote.

Mh.Dr.Magufuli ,tusikubari kugawanywa kisa itikadi,kisa wanaharakati nk....NINI KITATOKEA BAADA YA AWAMU YA TANO
 
Japo hili ni swali muhimu sana, jibu lake ni simple, kulikuwa na awamu ya kwanza ikapita ikaja awamu ya pili nayo ikapita ikaja awamu ya tatu vivyo hivyo nayo ikapita na awamu zinakuja na zinapita hadi sasa ni awamu ya tano nayo pia ikifika muda wake, itapita, kitakachofuata baada ya awamu ya tano kuisha au kupita, itaingia awamu ya Sita, kila awamu na mambo zake kama ilivyo kwa kila zama na zama zake.
P
 
Baada ya awamu ya 5 :

Wapo watakaoikimbia TZ,

Wapo watakaoanzisha fujo na vurugu ili kuonesha kuwa awamu ya 5 ilitenda vyema.

Mahakama na mahabusu zitaongeza wateja.

Ukanda na Ukabila utatamalaki.

Miradi mingi isiyo na tija itasimama na kutengeneza hasara kubwa ambayo haijawahi tokea tangu TZ ipate Uhuru.

Wakulima na Wafanyakazi watarejeshewa matumaini ya kuwa na maisha bora (siyo bora maisha ya awamu ya 5 )

Amani, upendo, mshikamàno na udugu wa waTZ utarejea tena.

Haitatokea tena watu kutekwa, kuteswa, kuuawa, kupotezwa au KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA.

Haitatokea tena Watu kutishwa na kutiwa hofu kama pichani hapo chini.

Wakulima hawatakopwa tena na serikali.
 
Attachments

  • 1566837386572.jpeg
    1566837386572.jpeg
    89.3 KB · Views: 27
Hapa ndiyo namkumbuka JK Nyerere. Alimzuia Ali Hassan Mwinyi asibadili Katiba kuongeza ukomo wa kutawala ambao Mwinyi alikuwa anautaka kwa kupitia midomo ya wapambe. Lakini vike vile alizuia kupata viongozi wabovu kama Malecela, Kolimba na Lowassa.

Sasa hivi hatuna Nyerere. Ninachokiona tunahitaji Mungu tu atunusuru kutoka kwenye huu mtego. Tupate mrithi ambaye ni 'sober' na ambaye hatokani na msukumo wa Jiwe. Amini usiamini kwa hali iliyopo ya kuvunja katiba Jiwe anaweza kumuachia Bashite.

Akitoka kwenye kambi hasimu za CCM yaweza kuwa shida kubwa. Imagine mtu kama Membe anakuwa Rais, hiyo revenge itakuwa balaa.

Upinzani umetendewa vibaya sana katika historia ya nchi yetu. Naamini wakishinda immediately baada ya Jiwe revenge itakuwa mbaya sana. Hebu pata picha Tundu Lissu anakuwa Rais na Mbowe PM, hapatakalika.

Kwa hiyo tunahitaji sampuli kama za akina Jaji Agustino Ramadhani, Prof Mark Mwandosya, Dr Bilal au hata Nahodha. Sampuli ya watu nje ya mfumo uliopo madarakani sasa hivi na uliopo upinzani ndiyo wanaweza kuleta maridhiano ya kitaifa.

JPM aondoke hata 2020 kwa kuwa anajenga uadui sana kati ya Watanzania
 
Kwel mkuu, hii miaka minne huyu jamaa katugawa sana watanzania, now days tunaishi kwa chuki, uminywaji wa demokrasia, haki, sheria kandamizi zinatungwa kila leo ila nachoshangaa bado wapo watanzania wenzetu wanamsifu huyu mtu
 
Baada ya utawala wa magufuli ritutashuhudia:

1. Kukua kwa uchumi kwa kasi zaidi kwa kuwa miundombinu ya kuwezesha uchumi huo kufikiwa yanaboreshwa na kutengenezwa sasa. Na hii ndio legacy ambayo itakumbukwa juu ya utawala wa magufuli kwa miaka mingi.

2. Kukua na kuenea kwa kasi dhana na falsfa ya kujitegemea kwa nchi kwa vizazi vingi vijavyo. Falsafa hiyo imepata uhai mpya chini ya utawala wa Magufuli.

3. Vitendo vya wizi, ukabaji, ubakaji, ujambazi na uhalifu wowote mwingine utakuwa umepungua na kuweza kuisha kabisa. Hii ni kwa sababu watu wenye matendo hayo wanadhibitiwa sana chini ya utawala wa Magufuli.

4. kujengeka kwa mifumo imara ya kitaasisi ambayo ina nguvu ya kudhibiti na kuzuia uhalifu,wizi, ufisadi, rushwa na mienendo miovu katika jamii, sehemu za kazi n.K

5. Kujengeka kwa taifa lenye wazalendo halisi wa nchi yao na kuondokana na taifa la kianaharakati linachochea machafuko ,fujo,migomo na maandamano isiyo na tija wala umuhimu.

Hiyo ndio Tanzania baada ya Magufuli . kama huu uzi uishivyo naomba na comment hii idumu ili miaka 50 ijayo watoto na wajukuu zetu wasome hii comment.
 
Hapa ndiyo namkumbuka JK Nyerere. Alimzuia Ali Hassan Mwinyi asibadili Katiba kuongeza ukomo wa kutawala ambao Mwinyi alikuwa anautaka kwa kupitia midomo ya wapambe. Lakini vike vile alizuia kupata viongozi wabovu kama Malecela, Kolimba na Lowassa.

Sasa hivi hatuna Nyerere. Ninachokiona tunahitaji Mungu tu atunusuru kutoka kwenye huu mtego. Tupate mrithi ambaye ni 'sober' na ambaye hatokani na msukumo wa Jiwe. Amini usiamini kwa hali iliyopo ya kuvunja katiba Jiwe anaweza kumuachia Bashite.

Akitoka kwenye kambi hasimu za CCM yaweza kuwa shida kubwa. Imagine mtu kama Membe anakuwa Rais, hiyo revenge itakuwa balaa.

Upinzani umetendewa vibaya sana katika historia ya nchi yetu. Naamini wakishinda immediately baada ya Jiwe revenge itakuwa mbaya sana. Hebu pata picha Tundu Lissu anakuwa Rais na Mbowe PM, hapatakalika.

Kwa hiyo tunahitaji sampuli kama za akina Jaji Agustino Ramadhani, Prof Mark Mwandosya, Dr Bilal au hata Nahodha. Sampuli ya watu nje ya mfumo uliopo madarakani sasa hivi na uliopo upinzani ndiyo wanaweza kuleta maridhiano ya kitaifa.

JPM aondoke hata 2020 kwa kuwa anajenga uadui sana kati ya Watanzania
CCM ni laana kwa Taifa letu
 
Back
Top Bottom