Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Basi kua mwalimu wake ila hapo kwenye namba tatu umeongopea maana kuna ujumbe huko chini umesadifu kua wewe ni muongeaji sana .

Punguza kuongea na acha kumfatilia kila anapo zingua .

,Mpe pigo la kiakili kwa sababu ulisha mwambia anakosea ila anaendelea wewe kua busy na majukumu yako usionyeshe kushtuka wala nini , kua busy tu na kazi zako na mwema kwake kwa week angalau moja lazima atauliza kulikoni na akiuliza tuu anzeni hapo hapo kuyajenga.

NB. WANAUME TUKIKOSEA ALAFU MWANAMKE AKAJUA NA AKAKAA KIMNYA HUAGA TUNAHISI HATIA MOYONI , ILA UKINYANYUA MDOMO NDIYO UMECHOCHEA KOSA

Kama ni uongo nipigwe mawe nipo hapa
kwani tulikua tunaibiana ushauri au[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanawake bwana mnamambo ya ajambu. Mwanaume anayeweza kuhudumia familia utegemee awe anakugegeda wewe tuu🤣🤣🤣🤣

Wee ukitaka wako peke yako chukua akina mzabzab ambao hatuna hela na tuna vibamia. Wenye hela lazima wagegede mbussusu nyingi.

Alafu itakuwa so called bitches give him something special
 
Iko hivi mimi nitatoa ushauri kwa wanawake wote walioko humu, walioolewa na wasioolewa,

Kwanza mnapotaka kuolewa msiangalie mfuko wa mwanaume, bali muuanglie tabia yake.inawezekana kunamwanaume alikuwa anakupenda kwa zati, lakini ukamtosa,ukaenda kuolewa na huyo sababu anapesa ila hakuwa na upendo kwako, na wewe labda ndiye uliyelazimisha ndoa

Hapo hamna jinsi, huyo mwanaume anakudharau,hata kuja badilika kamwe tabia yake tegemea kukuletea magonjwa na ukonde sababu ya stress kumsubiria mtu kama mlinzi wake

Nini kifanyike hapo inabidi uachane tu na hiyo ndoa, utampata tu mume atakayekufaa,kuliko uanze kuishi na stress na mtu atakeyekuwa amekupa magono na ukimwi
 
Kuingia kwenye ndoa ni jambo moja na kudumu kwenye ndoa ni jambo jingine.

Uvumilivu, busara, upendo, kujitoa na mshikamano ni baadhi ya 'matunda ya Roho' yanayotakiwa ili ndoa iweze kudumu. Wengi waliyoyakosa, waliishia njiani.
Hapa ndio wanawake wengi hawapajui....
 
Tulia wewe, mwanaume akiingia kwenye ndoa ndio hupata zaidi vishawishi unakuta mke ndio ametoka uzazi amejiachia balaa hapo unaandika ila ukute umevaa mikanga tupu na minywele umeiachia tu.

Tulia nawe jikague vizuri, haiwezekani ndoa ya miaka miwili unaanza kulalamika mtu anakucheat. Mpe mambo jipake poda nukia oga osha mashuka, nyumba ing'ae acha kumsemesha upuuzi kila saa na acha kumkaguakagua simu yake na kumdadisi alikuwa wapi instead anza kumpa pole kwa kazi na kumwambia maneno mazuri.

Ongea nae mambo yanayokuudhi kwa upendo na upole na mfanye ajisikie aibu kwa anayoyafanya pia uasiache kumkumbusha viapo vyenu kanisani na usiache pia kumuombea kwa Mungu.

Pia ongea nae kwa upole kuhusu hisia zako kwake jinsi unavyompenda na namna anavyokuumiza kwa matendo yake. Mfahamishe kwamba wewe ni mwanadamu haupendi kujuta kuolewa nae na haupendi ifike pahala muachane au mvunje ndoa sababu ambazo anaweza kuzuia yeye mwanaume wako.

Tell him your feelings dewply kwa upole. Tafuta sehemu mtoe out na umwambie unataka kukaa nae faragha ya dinner. Mjadili bila yeye kunywa pombe ili aelewe maana akilewa atakuchukulia poa.

Jaribu kumuelezea namna ambavyo pombe inamzidi pia angalia kama inasababishwa na stress za kazi au nini? Ongea nae acha kukimbilia kutafuta ushauri mwingi maisha ni yako wewe.

Pambana ndoa sio Big Brother House. Fikiria mwanao je ataishi na wababa wangapi? Unamuacha huyu utakutana na malaika? Wanaume ndio sisi sisi tu hatuna tofauti sana we just sin differently.

Komaa na ndoa we tafuta jamaa akuliwaze kimyakimya huku unatunza ndoa kwa maana kuishi pamoja ili mtoto akue mazingira salama.

Frankly speaking, nimeupenda sana ushauri wako mkuu. Ndani yake umenena kwa kutumia busara ya kiAfrika na umejaribu kumueleza uhalisia wa kwamba sisi wanaume wengi wetu tunafanana ujinga.

Sijui ni kwamba sijakua ama nina ideals za feminism ila huwa nakasirishwa sana na namna tunavyomdidimiza mwanamke hasa wa kiAfrika, japo hata wanawake wa kiArabu wanapitia changamoto nyingi pia.

Story aliyoleta mtoa mada iko one-sided hivyo naacha benefit of the doubt. Lakini kama mwanamke angekua ndo analewa kupitiliza na ku'cheat mara kwa mara (hata mara moja tu), ungemshauri mwanaume the same thing? Na kama hapana, kwanini?

Jamii zetu mpaka dini imewafanya wanawake kuwa submissive na kuvumilia vitu ambavyo ni vya kipumbavu sana. Kwa review yangu ndogo, hii yote inatokana na hali ya uchumi.

Ni ukweli usiopingika kwamba, mwanamke kama mwanaume wako kakuzidi mbali kiuchumi na yupo na wewe sio sababu anakupenda sana bali anataka tu kuwa na mtu kwa sababu mbalimbali, UTATESEKA SANA. Hakuna rangi utaacha kuona.

Nina dada zangu wengi sana, nina mama yangu ambaye nimeona alivyonyanyasika na dharau za hapa na pale, nina wapwa zangu wakike kibao na hopefully ipo siku nitakua baba wa mtoto wangu wa kike. Natamani sana ifike siku wanawake waondokane na hiki kitanzi. Sipendi wala sitopenda kuona jambo kama hili linatokea kwa ndugu yangu ama kwa mwanamke mwingine yeyote.

A day should come when women know their worth. A day should come when women become economically and sexually liberated. A day must come when women choose happiness over social validation.

Ninae mpenzi wangu, nampenda sana ila bado nina tamaa za hapa na pale kwakua ni asili yetu. Ila namheshimu enough that siwezi fanya ujinga wa kumuonyesha kwa makusudi kwamba nina'cheat, NEVER.

USHAURI WANGU KWA MTOA MADA;

Dada yangu kama unajiweza kiuchumi na umeshafanya jitihada zote kusuluhisha tatizo lako ila bado brother anaendelea, nakushauri uchague amani yako. Why put up with a toxic marriage kwa sababu tu ya mtoto/watoto na wakati unajiweza kiuchumi?

Wanaume asilimia kubwa tuna'cheat na wala hili jambo haliwezi kukoma leo. Tumeshaumbwa na tamaa ambayo mara nyingi inazidi akili. Kwa experience yangu ndogo, tunapenda mara moja ila tunatamani mtu mpya karibia kila siku tunayozunguka huko duniani. Hili wala halihitaji atoke mwalimu wa kiJerumani aje kufundisha hili jambo.

Ila tu, kama anakupenda ama anakuheshimu, kamwe hawezi kutaka ujue kwamba ana'cheat delibarately. Mpaka anakua reckless na kukuonyesha makusudi kwa mienendo yake, hapo tayari ushajua unasimama wapi hivyo usisubiri mpaka yakukute madhara ya moja kwa moja ukiwa kwenye jitihada zako za kupanda mihogo kwenye rami.

Kama unajiweza kiuchumi, naweka msisitizo kwenye "KAMA UNAJIWEZA KIUCHUMI" (maana asikudanganye mtu bwana njaa mbaya sana), na wewe tafuta mtu unaempenda uanzishe nae mahusiano. Kama utaamua kuivunja ndoa, well and good. Kama unampenda sana na hutamani kumuacha basi fanya kama alivyoeleza mkuu kwenye ushauri wake hapo juu.

Kumbuka kwamba wote tunaoshauri hatutakuwa na wewe either ukiamua kuvunja ndoa ama ukiamua kubakia kwenye ndoa. Madhara na faida za maamuzi yako yataendelea kuja upande wako wewe mwenyewe.
 
Wanaume hatupendi kelele.
Huenda wewe una kelele sana na hiyo ndo sababu kuu ya ulevi wa mumeo na uchepukaji.

Cha kufanya we mwache kwa muda hata wa mwezi mmoja bila kumpigia kelele za uliwa wapi, kila siku nasema hili, we mwanaume mlevi sana, hujali familia, mbona wenzio hawako ivo nk nk.

Uwe busy na kazi au biashara yako, akiona umebadilika kazi itakua kwake sasa kuanza kufatilia kwanini hupigi kelele tena, au unachepuka akikuuliza ndo hapo mtakaa sawa.

Kelele, vikao na mshataka kwa wazazi haviwezi mbadilisha.
Hili ndio jibu mujarabu kwa mtoa mada.
 
Tulia wewe, mwanaume akiingia kwenye ndoa ndio hupata zaidi vishawishi unakuta mke ndio ametoka uzazi amejiachia balaa hapo unaandika ila ukute umevaa mikanga tupu na minywele umeiachia tu.

Tulia nawe jikague vizuri, haiwezekani ndoa ya miaka miwili unaanza kulalamika mtu anakucheat. Mpe mambo jipake poda nukia oga osha mashuka, nyumba ing'ae acha kumsemesha upuuzi kila saa na acha kumkaguakagua simu yake na kumdadisi alikuwa wapi instead anza kumpa pole kwa kazi na kumwambia maneno mazuri.

Ongea nae mambo yanayokuudhi kwa upendo na upole na mfanye ajisikie aibu kwa anayoyafanya pia uasiache kumkumbusha viapo vyenu kanisani na usiache pia kumuombea kwa Mungu.

Pia ongea nae kwa upole kuhusu hisia zako kwake jinsi unavyompenda na namna anavyokuumiza kwa matendo yake. Mfahamishe kwamba wewe ni mwanadamu haupendi kujuta kuolewa nae na haupendi ifike pahala muachane au mvunje ndoa sababu ambazo anaweza kuzuia yeye mwanaume wako.

Tell him your feelings dewply kwa upole. Tafuta sehemu mtoe out na umwambie unataka kukaa nae faragha ya dinner. Mjadili bila yeye kunywa pombe ili aelewe maana akilewa atakuchukulia poa.

Jaribu kumuelezea namna ambavyo pombe inamzidi pia angalia kama inasababishwa na stress za kazi au nini? Ongea nae acha kukimbilia kutafuta ushauri mwingi maisha ni yako wewe.

Pambana ndoa sio Big Brother House. Fikiria mwanao je ataishi na wababa wangapi? Unamuacha huyu utakutana na malaika? Wanaume ndio sisi sisi tu hatuna tofauti sana we just sin differently.

Komaa na ndoa we tafuta jamaa akuliwaze kimyakimya huku unatunza ndoa kwa maana kuishi pamoja ili mtoto akue mazingira salama.
Kwa wanaume wa aina hii mazungumzo hayatoshi. Kama anakula mpaka Malaya?.

Huyu inaonekana hayo mambo yako damuni. Kuondoa long-term effect ya mahusiano hayo Bora yavunjike tu. Hata hivyo nasikia harufu ya damu hapo ndoa nyingi zinazoishia kuuawa mmoja wapo zinapitaga njia ngum ya migogoro mfululizo kama hii
 
Humu kuna unafiki sana mada ya usaliti ikiletwa na Mwanamke ushauri wa Wanaume ni Vumilia,ila mada ikiletwa ná Mwanaume ushauri ni piga chini hakufai[emoji2372]
Sio unafiki. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume kuchepuka na mwanamke kuchepuka.
 
Achukue huu ushauri aufanyie kazi utamfaa.
Ukisha achana nae akipata atakae mueka sawa itakuaje?
Wewe bado mdogo jaribu kumuelewesha vizuri, kama familia anahudumia vizuri hakuna shida.
Nenda kanisani kwa padre aliewafungisha ndoa muelezee yanayokusibu nadhani ataitwa na wazee wa kanisa tu.
Akishindwa na hapo achana nae tunawahitaji single mother mtaani sana tu.
 
Ebu comments ziwe fupfupi ili huyu mwanamke anae jiita binti apate jibu...😊
 
Mke wangu wewe hujui tu kwanini nachepuka.

Ulevi naweza acha hata leo ila kwenye kuchepuka labda uweze kunifinyia kwa ndani kama flora. Alafu tatizo lingine wewe kuna kitu hunipi ambacho nikienda kwa jackline ananipa
 
Back
Top Bottom