Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Unyafanya uliyomlaumu mwenzio akiyafanya..!!! By the way, Mamy K, hiyo K kirefu chake ni nini?
Kirefu chake Khan, la kihindi.....lina historia yake.
Kuna muda tunazivunja hizi ndoa kwa kujihesabia utakatifu sana.....ukishateleza kuna mambo unajikuta unavunga tu afu siku zinasonga mnazeeka wote.
 
Kuna jamaa yetu ni mlevi kupindukia,
Alishajua kuwa tunamsema vibaya kwa ulevi wake,

Kuna siku tuko na shemej yetu jamaa alifunguka mazima kuhusu tabia ya mkewe,
Mkewe aliwai toka na shem wake wa tumbo moja,

Jamaa akamgeuka mkewake unakataa!?

Dah yule shem akainamia chini kimya,

Jamaa akaturudia na sisi akatuuliza ni nani anaweza vumilia hili tukio?

Tukabaki midomo wazi,

Mambo ya ndoa bana usikilize pande zote, ila hii ya upande 1, ni kuchangamsha genge,

Mlianza vizur iweje sasa?
Yeye alikuwa wapi mpaka mke anayafanya hayo?
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
Jitahidi ku-update, punguza ustaarabu chumbani!
Ukiwa chumbani na mumeo usilete ustaarabu kuwa kahaba mkiwa chumbani. U will thank me later!
 
Hakuna utakapokwenda kusiwe na changamoto, jaribu kupambana nazo hizo za mumeo.
 
Haya mambo sio marahisi kiivyo
Kuna sister ake na brother yangu mmoja wa kazini alikuwa ananisimulia maswahibu ya dada yake, waliachana na mumewe baada ya kumfuma akijisevia house girl (dada yake anajiweza kiuchumi tena ni zile product za mbeya) na anacheo serikalini

fast forward now age imesogea kidogo sasa soko limeshuka hivyo yeye ndio anawinda wanaume ila wanaume wanamkimbia anaishia broke guys (wale bodaboda waliokula hela ya boss wanatafuta marejesho) kinachomkera jamaa ni vile wale boda hata upeo wao ni mdogo hivyo wanasimuliana hovyo hovyo
Sasa mtoa mada anatakiwa kufanya maamuzi kwa kuzingatia mustakabali mpana wa leo na kesho
Bodaboda wanapenda type hizo za wanawake.
 
Mleta uzi wewe ni Muongo Pro Max... Kwanza umetudanganya waziwazi kua wewe ni msichana kumbe tayari umezaa asee.

Yani hapo unapojiona wewe bado ni msichana ndo tatizo linapoanzia au nadanganya ndugu zangu.
 
Humu kuna unafiki sana mada ya usaliti ikiletwa na Mwanamke ushauri wa Wanaume ni Vumilia,ila mada ikiletwa ná Mwanaume ushauri ni piga chini hakufai🤷🏼‍♀️
Yan wanaume jaman, Yan apo ingekua ni mwanaume anasema ivyo wote wangeshauri apige chini, ila saiv wanatoa ushauri rahisi as if wanawake hawana mioyo, MUNGU atutie nguvu
 
Back
Top Bottom