Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Baada ya Miaka 2, natamani Ndoa yangu ivunjike

Mambo ya ndoa ni noma sana,sema Wanaume wengi huwa hatusemi mapungufu ya wenza wetu kama wenyewe walivyo vimbelembele kusema ya kwetu.
Mie nijuavyo matatizo 90% kwenye ndoa yanachangiwa na Wanawake.
Sisi wanaume tuna kifua tunatunza mengi. Tofauti na wanawake, wao kifua hawana ni kumwagika tu
 
Imekua too Much , 31yrs

Huyo atakutesa kutulia ni kwenye 55 huko tena Mungu akiingilia kati
Sasa angalia utaweza na magonjwa
I think you have goals better than being married
Wadada wengi huwa tunataka kuolewa,umesha olewa umeshavaa shera hakuna kipya
Inuka anza kutimiza ndoto zako sio kila ndoa hufika kufa na kuzikana

Kabla ya kuvunja official jitenge nae umsome ukiona haogopi kuachana na wewe jua huyo sio mume
Akijirudi mkae muongee na muwekeane mikakati ya kusonga mbele
 
Mshachokana, daaaah! Kuishi single na penyewe ni Ngoma nzito maake inakulazimu uwe na ngozi ngumu kweli kweli kutokana na ninavyowaona wamama wanaoishi single.

Fanya vile moyo wako unaridhia
 
Asante kwa ushauri mkuu
Chambua ushauri wa watu vyema,huyo anayekushauri eti umpate wa kukuliwaza wakati bado upo ndoani,aisee,matokeo yake huwa hayatabiriki ikigundulika.Matokeo yake huweza kua mazuri kwako au mabaya,hatakama mumeo ana tabia mbaya.
 
Kama mmeo anasimamia majukumu Yake vizuri huna haja ya kuachana naye.

Jaribu kumwambia kuhusu madhara ya kunywa pombe kupitiliza afu mmwombe Mungu atamsaidia mumeo kubadilika
.
Hapo suluhu ni kukata ndoa tu. Sion mwisho mzuri hapo
 
Dahi,hizi ndoa hizi!mimi hapo nashauri umshikrikishe Mungu kwenye hilo,maana maamuzi yoyote utakayoyafanya ndoa ikavunjika wewe ndio wa kulaumiwa,kwani ulikula kiapo utamvumilia mwenzako kwenye shida na raha.Kibaya tunachojidanganya wengi ni kuwa tukiachana na wanandoa wenzetu tutakutana na raha,lakini una weza kuachana naye na hali yako ikawa mbaya zaidi mpaka ukajuta,wakati utakuta mwenzako sasa kampata anayemvumilia na kaweza kumtuliza vizuri na maisha yakawa bora zaidi...
 
Kiufupi mfikishe kwa mshenga wake azungumze nae, ukitoka hapo na wewe utakuwa mtu wa kutanga tanga.

Unaweza kupata mtu wa kutulia lkn nadra sana ukizingatia na poa una mtoto tayari.
 
Ukisha achana nae akipata atakae mueka sawa itakuaje?
Wewe bado mdogo jaribu kumuelewesha vizuri, kama familia anahudumia vizuri hakuna shida.
Nenda kanisani kwa padre aliewafungisha ndoa muelezee yanayokusibu nadhani ataitwa na wazee wa kanisa tu.
Akishindwa na hapo achana nae tunawahitaji single mother mtaani sana tu.
tunawahitaji single mother mtaani sana tu...mtego huu,akili kumkichwa
 
Natamani kuvunja ndoa yangu.

Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.

Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.

Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:

1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.

2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.

Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.
a mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo
Ndoa za kigalatia ni mtihani,
kitutenganishe.
 
Kwa umuri wenu 28 na 31yrs sidhani kama hiyo ndoa inaweza ku-survive hapo wengi mko kwenye age of adventure and regrate, kama unashida na ndoa tafuta mwanaume alio pevuka umri kuanzia 38yrs au tafuta mwanaume mwenye shida ya pesa mnyenyekevu ila sio masikini sana.

Sawa Mkuu
 
Nashukuru mungu, familia nilioitamani ndio nitakayo ishi nayo, we joho huyo ndie mume wako, fanya kubuni njia zitakazo mchomoa huko, na vumilia kuyapokea matokeo unayoyahitaji.
 
Back
Top Bottom