Mrs Joho 001
Member
- Aug 5, 2023
- 52
- 126
Natamani kuvunja ndoa yangu.
Habari zenu wakuu, natumai mko poa. Nimekuja na nia ya dhati kutafuta ushauri kuhusu jambo langu ambalo linanitatiza.
Mimi ni msichana mwenye umri chini ya miaka 30. Nina mtoto mmoja wa kiume. Nimekuwa katika ndoa na mume wangu kwa takriban miaka miwili sasa.
Sababu za maamuzi yangu ni kama ifuatavyo:
1. Uchepukaji uliokithiri: Huyu mume wangu amekuwa akinihadaa sana. Sijawahi kuona kitu kilichoniumiza zaidi ya kugundua kuwa anatoka na wanawake wengine. Ameomba msamaha kila mara ninapomfumania, lakini bado anarudia tabia hiyo. Kesi zetu zimekuwa nyingi kwa wazazi na nadhani wamechoka kutusuluhisha.
2. Ulevi uliopitiliza: Mume wangu ni mlevi sana. Kurudi nyumbani asubuhi ni jambo la kawaida kwake. Nimeshazungumza naye na kumweleza jinsi ninavyojisikia kuhusu tabia yake ya kunywa kupindukia, ingawa anahudumia familia vizuri. Lakini, hupati muda na familia kabisa. Inanidhalilisha sana kwa sababu tunakaa na mdogo wake nyumbani, hivyo najihisi vibaya sana anaporudi asubuhi.
Ndoa yetu imefungwa kanisani na tumekuwa tukiishi pamoja kwa miaka miwili tu. Nashauriwa nifanye nini kuhusu maamuzi yangu haya, maana sijisikii furaha kabisa katika ndoa hii. Na mimi ni mchanga sana kuishi kama hivi hadi kifo kitutenganishe.