Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Mtasema kila kitu ila muda utahanua. Nyie ndio wale wahafidhina alokuwa anasema mama
 
Acheni kupopoma.
WaTanzania hatuna shukurani wala mchango wa kusaidia kusonga mbele kazi kurudishana Nyuma tu.
Ulitaka Yale Yale ya aliyeenda yaendelee kujirudia sio.
Huu ni ujinga!
 
Asilimia kubwa ya wanaopinga siasa za kistaarabu ni wafuasi wa jiwe, wafuasi wa zito wanaoona wameachwa nyuma kwa kinachoendelea ss hv, wafuasi wa covid 19 na wahafidhina ambao wao bila siasa za ghiliba hawawezi kupata mile age.
 
Huyo mnafiki muache kama alivyo, ameamua kujitoa akili makusudi anapiga kelele zisizokuwa na maana.

Wakati wapinzani wakionewa, ni wao waliokuwa wakiandika humu upinzani sio uadui, leo Samia ametamka hayo maneno, wanageuka Mbowe kalambishwa asali, ni ujinga ujinga mwepesi sana.
 
Hujajibu swali, umerukia tu kuandika insha ndefu.
Narudia swali, CHADEMA na CCM wamekubaliana nini?
 
Watz hawastahili kupambaniwa kwa namna yoyote, ukipata nafasi ya kuwatandika basi watandike kweli kweli.
 
Watanzania wengi wana PhD lakini hawajui hicho kingereza, kama nasema uongo mwambie Profesa Ndalichako aongee sentensi kumi za kiingereza fluently bila hesitations.

Unafikaje phd bila kuwa na uelewa wa hiyo lugha? Hizo research unafanyaje?
 
Swali la msingi sana.Aeleze alivyotaka CDM ingefanya siasa za aina ipi?Je,wapigane ngumi?Waue watu?Wafanye ugaidi?Wapindue serikali?Watukane asubuhi ya leo hadi keshoye kwa mtiririko?Au ana chama chake mbadala akilete kifanye atakacho?
 
Swali la msingi sana.Aeleze alivyotaka CDM ingefanya siasa za aina ipi?Je,wapigane ngumi?Waue watu?Wafanye ugaidi?Wapindue serikali?Watukane asubuhi ya leo hadi keshoye kwa mtiririko?Au ana chama chake mbadala akilete kifanye atakacho?
Sasa ndo wavae viatu vya Cheyo na Shibuda kwa kasi namna hii?.

Maana hata kina Cheyo argument yao ya kujikomba kwa CCM ni hiyohiyo mnayoita siasa za "kisataarbu"
 
Wao lazima waendelee kukosoa tu,wakusifia wapo hao MACHAWA!! Na sasa wabunge watakuwa na wakati mgumu sana kwani toka wamebaki wenyewe bungeni hakuna wanalowasemea wananchi!!wanaowasemea wananchi wapo nje ya bunge!!!
Chadema sasa hivi wanasifia na kukosoa tofauti na huko nyuma walikuwa wanakosoa tu mwanzo mwisho, hivyo sasa hivi kuna mabadiliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…