Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Tatizo la hapa JF kila mtu ni mtaalam wa kila jambo. Na wakati mwingine wauliza maswali kama makoye sr (ingawa simuamini) wanauliza Padre jinsi ya kuishi na mwanamke ndani. Unategemea nini? Padre hajawahi na hatawahi kuoa, atakueleza nini kama si ndoto za alinacha
 
Kumbuka leo ni tofauti na kesho katika Afrika
 
Kwahiyo 80 mio ni ndogo ? Kwa biashara unajua kuna watu wana import kwa 80mio ? Na wanazungusha hiyo hela ?

ama ananunua kwa supplier hapa Tz kwa 80 mio ? Hiyo hiyo kama hujaishi kwenye industry ya biashara ni ngumu kunielewa,
Unafanya biashara wewe..?
 
Jamii forum ni uwanja mpana sana Kuna watu wa Kila aina, ushauri wenu ni wa muhimu sana kwangu naendelea kusoma comments zenu, mwaka mzima nimekaa tu nyumbani sasa nataka niwe na cha kufanya asanteni sana
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Kuna memmber humu alitoa muongozo mzuri sana wa maisha kabla na baada ya kustaafu, ila ile thread siikumbuki ilikuwa na title gani? Labda waombe Admins waipost tena hapa, lakini katikamambo makubwa niliyojifunza ni kuwa makini na aina ya biashara unayoichagua na mazingira utakakoamua kuishi isiwe mjini, nenda nje ya mji ambako utapanua wigo wa kufanya shughuli zaidi za kufuga na kilimo
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Upo mkoa gani?
Unaweza kununua viwanja kwenye skwata huko. Sema majohe nk. Kiwanja ml 10 kisha unajenga chumba na sebule unapangisha. Ml 80 ukiisimamia vizuri hukosi vyumba 10. Kila chumba 150 kwa mwezi
Ni ushauri tu
 
Achana na biashara,sijui ufugaji,achana na kilimo,mazao....
Kwa 80m wekeza kwenye nyumba ya/za wapangaji na fremu(hii ni fixed asset),lenga pato/kusanyo la 1.5m kwa mwezi,nakuhakikishia huta kuja kunisahau

Jenga Rooms 20 (15 za makazi na 5 frame),uswazi room moja kila kitu inakula 3.2-3.5m
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80
 
Ukweli Sina uzoefu na biashara nilmudu kujenga nyumba ya kuishi na nyingine ya kupangisha ndo inanisaidia pamoja na pensheni ya Kila mwezi, asante Kwa ushauri
Sawa kwa kuwa huna uzoefu,achana na wazo la biashara.

Ukiwekeza UTT kwa riba ya around 15% kwa mwaka kwa hiyo mil80 kila mwezi utavuna around milioni 1 na pesa yako ipo palepale.

Sasa ukichukua hiyo mil1 jumlisha na pensheni yako ya kila mwezi unapata pesa fulani nzuri tu ya kukuwezesha kuishi tena kiboss tu hata hutatia huruma,usisumbue ubongo wako sasa hv baba yangu,kula jasho lako bila stress
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Binafsi nikifikia stage ya kuacha kazi nimepanga kuanza biashara ya Hardware na Kirikou kwaajili ya kubebea bidhaa za Wateje(Delivery)pia nitanunua mashine ya kufyatua tofali, option ya pili nitanunua heka kadhaa za shamba nitaanza ufugaji wa Kuku mchanganyiko na mbogamboga kibiashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…