Nilivyoanza Biashara ya Tofali bila kujua nitakachokutana nacho

Nilivyoanza Biashara ya Tofali bila kujua nitakachokutana nacho

Wakipekee

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
6,514
Reaction score
11,384
Habari wanaJF...

Oke! Baada ya salamu nirudi kwenye mada yangu, jinsi gani biashara ndogo ya tofali ilivyonipa faida kubwa kwa jasho na damu.

Miezi kama minne nyuma nilipata idea ya kuuza tofali za kuchoma. Hii idea ilikuja baada ya kuteseka sana kupata tofali wakati wa ujenzi wa nyumba yangu.

Nilisumbuka sana. Kila nikienda kununua kwa wauzaji naambiwa kwamba tanuru nilizoziona tayari zimeshanunuliwa. So kama nataka tofali niweke oda yangu mapema, lakini itabidi nisubiri kama wiki tatu hadi nne.

Nikaona sio kesi, nikalipia.
Sasa baadae nikaja nikajiuliza, kama tofali ni adimu hivi, mbona kuna fursa nzuri tu hapa?

Nikawaza na mimi niingie kwenye hii biashara.

Nikapiga hesabu zangu fresh. Kuna jamaa nikamfuata ambaye ni muuzaji wa tofali, nikamuuliza utaratibu ukoje na mimi naweza kufanya hii biashara?

Jamaa hakua na roho mbaya. Akaniunganisha na bwana mmoja hivi ambaye huwa anafyatua tofali.

Huyu bwana nikakaa nae chini na kumpa mkakati wa namna gani nahitaji kufanya hii business. Jamaa akasema, Mbona ni simple tu. Tena kuna eneo ambalo hutoa tofali nzuri sana. Kama nipo tayari, akaongee na mwenye eneo tuanze kazi.

Kesho yake huyu bwana, tumuite Daudi, akaja kunipa feedback kwamba mwenye eneo hana shida. Kikubwa, kwenye kila tofali elfu 5 yeye atachukua tofali buku.

Hapa ni wakati wa kuuza. Kwa kifupi, ukiuza tofali elfu tano utampa hela ya tofali 1000.

Nami nikaona mbona deal liko bomba... Maana nilitegemea ataomba hela kwanza kama nakodisha kumbe tutagawana kwenye mauzo what a deal..

Sikujua! 😂

Basi ipo hivi.
Mfyatuaji wa tofali hulipwa shilingi 30 (thelathini) za Kitanzania kwa kila tofali atakalofyatua. Lipasuke, lisipasuke, hiyo sio shida yake.

Kwa mfano akipiga tofali 1000, wewe utampa shilingi elfu 30.

Ila kuna bonus atakupa kama tofali 200 kwenye kila tofali buku kufidia zile zitakazopasuka. Na ni lazima zipasuke tu maana hekaheka ni nyingi.

Basi nikakaa na kupiga hesabu hapo.

Nikawaza, vipi kama tutapiga tofali 10,000?
Tofali moja nauza shilingi 200.
Kwa hiyo tofali 10,000 ni shilingi milioni 2.

Mfyatuaji nikimlipa shilingi 30 kwa tofali, hapo nitakuwa nimetumia laki 3 tu kwenye kufyatua.

Nikaanza kuona kama nimeokota dodo chini ya mpera.

Lakini kuna kitu nilikua sijakijua...

Kumbe Biashara kwenye karatasi na biashara kwenye uhalisia ni vitu viwili tofauti kabisa.

Nilianza kazi nikiwa na confidence kubwa. Kwa hesabu zangu niliona kama nikizalisha tofali nyingi na kuziuza, nitapata faida nzuri sana.

Lakini changamoto zikaanza kuja moja baada ya nyingine.

Mfano, msimamizi wangu ambae alikua ni Daudi nilimpa hela akanunue kuni za kuchomea tofali na hela ya kulipia Balaji Toyo ya kusomba. Jamaa akala hela na kukimbia.

Hapo nikapata pigo la kwanza.

Kama hiyo haitoshi, tofali zilikua zinapasuka sana.

Wapiga tofali nao walikua na uzembe sana. Leo wapo, kesho hawapo. Na wakati mwingine ushawalipa tayari, lakini kazi haijaisha.

Kazi ikaenda slow vibaya mno. Nilijuta na kupaniki!

Nikaanza kula hasara.

Hapo ndipo nikagundua kwamba kumbe tatizo sio tu kupata biashara nzuri. Kuna suala la namna unavyosimamia hiyo biashara. Kosa langu lilikua kuamini watu.

Na kubwa zaidi, nilikua nawalipa kabla ya kazi kuisha.

Baada ya kugundua udhaifu wangu nikakaa chini na nikaamua kubadilisha system kabisa.

Nikaweka lengo kwamba watu wapige tofali elfu 35 ili baada ya hekaheka zote za tofali kupasuka, kuharibika au kuungua vibaya, mimi nibaki na tofali elfu 30. Mpango ukawa ni tofali kwanza then manunuzi ya malighafi za kuchoma itakua baadae..

Hapo nikazidi kuongeza umakini zaidi.

Kumbuka, tofali moja nauza kwa shilingi 200, na mimi napigiwa kwa shilingi 30.

Japo gharama haikuishia hapo tu.

Kulikuwa na vibao vya kupigia, majembe, chakula, malipo ya wasombaji, kuni, usafiri na gharama nyingine ndogo ndogo ambazo ukizikusanya zinakuwa pesa kubwa.

Baada ya kupitia yote hayo, na kua serious nikaanza kuona biashara ikikaa sawa.

Mwisho wa siku nilikuja kufanikiwa sana.

Kwa kifupi nilifanikiwa kupata tofali elfu 30 na usher. Nikaziuza zote bila shida yoyote.

Tofali 30,000 na.. × shilingi 200 = shilingi milioni 6 na laki kadhaa..

Nikala milioni 6 yangu kiroho mbaya. Lakini nilikiona cha moto. 😂😂😂

Mwenye eneo nikamchana chake mi nikapita hivi. Kwa sasa naendelea na mishe zangu tu hapo nitarudi tena mwakani muda wa kiangazi maana sahivi naogopa mvua zinaweza kuanza muda wowote ikala kwangu...

Kwa hiyo kama kuna funzo moja kubwa nililopata kwenye biashara hii ya tofali ni kwamba, wazee

Usidharau biashara ndogo.

Wakati mwingine biashara unayoiona ni ndogo ndiyo inaweza kukufundisha mambo makubwa sana.

Na zaidi ya yote, usisubiri mpaka uwe na mtaji mkubwa ndio uanze kutafuta fursa.

Wakati mwingine fursa ipo kwenye kitu unachokiona kila siku.

Unachotakiwa ni kujiuliza tu...

“Kwa nini hiki kitu ni tatizo, na mimi naweza kulitatuaje?”

Hapo ndipo biashara inaweza kuanzia. Mi niliona kwenye tofali we unaweza kuona kwenye angle nyingine tu...

Tosha kwa leo... Kama una swali lolote unaweza uliza...
 
Brock za moto sana kwenye mtaji nilitaka kujalibu nimekutana na hesabu nzito kwanza unatakiwa upate eneo wastan nusu heka,umeme,maji,mchanga,siment,mlinzi wa siment,tra hapo kazi haijaanza tayar umeshapoteza hata 6m+ wakati tofar ya kuchoma ukiwa na 4m wewe ni mshua mkubwa hapo mchawi mvua tu
 
Kuna siku nilikua JKT kambi xyz sasa Co alienda kwenye mkutano wa kijiji kumbe kuna mchango wa ujenzi wa zahanati 😁😁, sasa bwana afande hapa na pale kujisachi pochi imepoaaa akaona hata isiwe tabu akaahidi tofali 6000 akawaambia mwezi ujao atazileta aloo alooo tulifyetua zile tofali kwa jasho na damu 😭😭😭😭 ukipewa kibao ni cha moto, ukisema uhamie kwenye maji ndo balaa 😁😁 komesha yote ni kwenye jembe kule kuchimba , kuvuruga udongo balaa

Mwisho tulizimaliza na wakati zinaenda bahati nzuri mkuu wa jkt miaka ile Afande Meja general kitundu alikuwepo kikosini alitupongeza na alikuwepo wakati wa kukabidhi
 
Mlipewa pongezi ya maneno?
 
JKT kuna hela mkuu..?😁😁 tulikula utawala siku mbili mwendo wa shangwe tuu
Umenikumbusha Dodoma jamaa zangu walizingua Kuna bi mkubwa Fulani mjeda akaita wenzake wakaja saiti wakabebwa kwenda kubeba zege kutwa nzima Kuna majengo yalikuwa yanajengwa malipo walikula msosi nyama nyingi Sana, jioni hapo wakarudishwa wako hoi tunawacheka tu
 
Mi nashangaa kuna watu wanamlaumu Magufuli kubana matumizi, hii nchi ina nguvu kazi kubwa sana kiasi kwamba hata njaa isingekuwepo

Wafungwa wangelima

Jkt wangejenga majengo ya serikali na nyumba za raia kwa bei nafuu

Ila sasa umaskini wa raia ndo mtaji wa wanasiasa 🚮
 
Kuna siku nilikua JKT kambi xyz sasa Co alienda kwenye mkutano wa kijiji kumbe kuna mchango wa ujenzi wa zahanati 😁😁, sasa bwana afande hapa na pale kujisachi pochi imepoaaa akaona hata isiwe tabu akaahidi tofali 6000 akawaambia mwezi ujao atazileta aloo alooo tulifyetua zile tofali kwa jasho na damu 😭😭😭😭 ukipewa kibao ni cha moto, ukisema uhamie kwenye maji ndo balaa 😁😁 komesha yote ni kwenye jembe kule kuchimba , kuvuruga udongo balaa

Mwisho tulizimaliza na wakati zinaenda bahati nzuri mkuu wa jkt miaka ile Afande Meja general kitundu alikuwepo kikosini alitupongeza na alikuwepo wakati wa kukabidhi
sio 841 hii kuie mlima Nguruwe
 
Brock za moto sana kwenye mtaji nilitaka kujalibu nimekutana na hesabu nzito kwanza unatakiwa upate eneo wastan nusu heka,umeme,maji,mchanga,siment,mlinzi wa siment,tra hapo kazi haijaanza tayar umeshapoteza hata 6m+ wakati tofar ya kuchoma ukiwa na 4m wewe ni mshua mkubwa hapo mchawi mvua tu
Milion 4 nyingi sana moja na nusu tu unakimbiza vizuri tu kikubwa ujue unachokifanya...
 
Kuna siku nilikua JKT kambi xyz sasa Co alienda kwenye mkutano wa kijiji kumbe kuna mchango wa ujenzi wa zahanati 😁😁, sasa bwana afande hapa na pale kujisachi pochi imepoaaa akaona hata isiwe tabu akaahidi tofali 6000 akawaambia mwezi ujao atazileta aloo alooo tulifyetua zile tofali kwa
Hii biashara kutoboa kazi sana bora uwekeze tu kwenye tofali za cement.
Huwezi fanya chochote zaidi ya kuharibu tu mazingira.
mfano
jasho na damu 😭😭😭😭 ukipewa kibao ni cha moto, ukisema uhamie kwenye maji ndo balaa 😁😁 komesha yote ni kwenye jembe kule kuchimba , kuvuruga udongo balaa

Mwisho tulizimaliza na wakati zinaenda bahati nzuri mkuu wa jkt miaka ile Afande Meja general kitundu alikuwepo kikosini alitupongeza na alikuwepo wakati wa kukabidhi
Da pole sana 😂😂😂
wakiwa 6 ni tofal 3k kwa siku kumi ni 30k, unahakikisha vp wote wanakuwa na kasi sawa au inayolingana sio laz

Hii biashara kutoboa kazi sana bora uwekeze tu kwenye tofali za cement.
Huwezi fanya chochote zaidi ya kuharibu tu mazingira.
Ni kweli lakini kwa mtu ambaye hana mtaji wa kuwekeza tofali za block anawezaje kufanya?
 
Ni kweli lakini kwa mtu ambaye hana mtaji wa kuwekeza tofali za block anawezaje kufanya
 
Back
Top Bottom