Denis Gregory
Member
- Jan 10, 2020
- 97
- 120
Habari za muda huu waheshimiwa, Salam.
Kabla ya yote, nipende kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa maoni mtakayokwenda kuandika hapa, nami nitayachakata kwa uhalisia. Asante sana.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nina kiasi cha Tsh Milioni 30,000,000 ambacho kiko tayari kwa ajili ya uwekezaji. Lengo langu ni kuanzisha biashara halali, yenye mzunguko mzuri na inayoweza kukua baada ya muda
Ili mnishauri vizuri na kwa uhalisia, ningependa kuweka mambo machache wazi
Eneo la Uwekezaji Nipo tayari kuwekeza katika maeneo yenye fursa iwe Dar es Salaam, Pwani, au mikoa mingine yenye mzunguko kulingana na fursa ya biashara yenyewe
Sekta ninazofikiria Niko wazi kupokea mawazo kwenye sekta mbalimbali kama vile biashara ya bidhaa za ujenzi/vifaa (Hardware), kilimo-biashara na ugavi (logistics/supply), au biashara yoyote ya jumla na rejareja yenye mzunguko wa haraka wa pesa
Uzoefu: Nina uzoefu wa kiasi fulani wa kusimamia miradi na biashara, lakini nahitaji maoni yenu kuhusu changamoto za sasa za soko (mwaka huu wa 2026) na wapi kuna mianya mizuri ya faida
Naomba mnisaidie kwenye maeneo haya
Ni wazo gani la biashara linalofaa zaidi kwa kiwango hiki cha mtaji kwa sasa
Changamoto gani kubwa ninazopaswa kuzichukulia tahadhari kwenye hiyo biashara
Mapendekezo ya maeneo (Location) ambayo biashara hiyo inaweza kuchangamka haraka
Mawazo yenu, tahadhari, na uzoefu wenu vitakuwa na mchango mkubwa sana kwangu.
Karibuni sana kwa miongozo na ushauri. Shukrani!