Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Ushafeli... Biashara ulipaswa kujifunza na kufanya tokea enzi hizo ukiwa umeajiriwa.. Ndiyo finally unataka uanze kujifunza biashara saa hizi? Tena kwa kushauriwa kuwa fanya biashara fulani!!!
 
Kwa bahati mbaya umekwishachelewa. Ulipaswa kujipanga miaka miwili kabla ya kustaafu. Fixed deposit hailipi, ni kama mtaji mfu. Hiyo pesa inatakiwa izunguke ili kuweza kuzaa kuliko kuiacha tu Benki ambao wanaitumia kama mtaji wao. Biashara ina mizungu yake. Shangaa una nyanya nzuri sana pale sokoni lakini hupati mnunuzi Jirani yako ana nyanya wengine huziita "masala" lakini anauza kwa watengeneza chips kama tomato source na zinakwisha asubuhi tu.
Mtihani
 
Mi nashauri upumzike tu...Kustaafu ni kupumzika na wala si kurudi kazini iwe biashara au ajira. Usijpe mapresha ya bureeeeeee!
 
Weka kiasi UTT hata millioni 60 itakayobaki fanya biashara ambayo una uzoefu nayo.Jitahidi kuomba sana mola wako usijichanganye na promo za toa sadaka ubarikiwe,kuweka kambi kwa demu yoyote, usijaribu kuzaa mtoto na mwanamke yeyote ikibidi kakate mirija,usigawe hela kwa watoto Wala ndugu zako, usifanye starehe yoyote kishamba, wakikuuliza hata mke kuwa vipi hela imetoka waambie bado na endelea kuwa na huzuni na mtu mwenye mawazo mengi.Ukiwa unafanya maombi na Mungu KUHUSU utulivu na akili kwenye hizo hela usipige kelele ikibidi nenda mbali nyumbani kwako au hakikisha hakuna mtu anayekusikiliza kwani kabla ya Mungu huwa Kuna wambea wanasikiliza hadi unachomwambia Mungu wako.Andika wosia na chagua mtoto mwenye akili ili ukitangulia aendeleze ulichoanzisha. La mwisho, ukikutana na demu usiwe na zaidi ya elfu 20 mfukoni na ugonge kimoja tu usepe, masikini huwa wanataka kikomesha ila mwisho wanakomeshwa wao
 
Kwanza tukafanye kikao kitambaa cheupe tabata
Pale kuna mawazo mazuri sana
DSC_0469.JPG
 
Chonde chonde ziache huko huko mzee wangu au kama ukizitoa huko benki kaziwekeze UTT kwani nafikiri riba yao ni nzuri,around 15%.

Kama wakati ulivyoajiriwa hukuwahi kufanya biashara usithubutu kuanzisha biashara sasa hivi.
Solution.
Hata akinunuwa shares TCC, BREWERYS, TWIGA, OXYGEN (TOC) nk.nk. siyo mbaya.
Anakula dividends kila mwaka na hela Iko safe kwa makampuni hayo...
 
Solution.
Hata akinunuwa shares TCC, BREWERYS, TWIGA, OXYGEN (TOC) nk.nk. siyo mbaya.
Anakula dividends kila mwaka na hela Iko safe kwa makampuni hayo...
Hakika mkuu,cha muhimu hiyo pesa asiifanyie biashara yeye kama yeye
 
Weka Utt utapata laki nane kwa mwezi jumlisha nusu mshahara unayopata kila mwezi hukosi moja na nusu.
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Hiyo 80m ukiweka kwenye biashara yote utalia kilio cha umbwa.. weka kwanza fungu la kumi kwenye biashara usome upepo.


Alafu asilimia 20 ya hela itakayo baki nenda huko vijijini kunako anguka mvua za kutosha na vyanzo vya maji tafuta hekari kadhaa halali zisiwe mapori tengefu alafu anza kilimo cha umwagiliaji na ufugaji huko


Kama unataka hela za haraka hakikisha wewe ni jasusi kwanza ingia na 55m kwenye madini ya dhahabu tupige kazi
 
cheza na wajukuu, piga glasi murua ya maziwa na mama yoyoo, au fuga tu kuku na kibustani cha kinyumbani nyumbani ukisindikiza umri lakini pia ukikazia kajizoezi.

kumbuka ulipaswa kustaafu bado ukiwa kwa job. ulipaswa tayari una tips za biashara ukiwa atleast una motomoto na kazi yako, uko kwenye teenage.

ninakoishi wastaafu wengi, walinunua basi hizi Rosa, na wengine walifungua baa kubwa wakaishia kuwala mabamedi wao na kufirisika jumla.
kwenye magari hawakuwa wazoefu walidanganywa kuhusu gharama za vipuri wakaibiwa. na kuhusu baa waliishia kuzigida pombe na marafiki zao.
 
comments za huu Uzi wa Mzee Makoye zimenichekesha sana!! Nahisi JF inatakiwa kuanza ku filter na ku block baadhi ya members. Unakuta kabisa member kazi yake ni kutoa ushauri wa kijinga!! Sasa member kama huyo kweli anahitajika hapa JF? Au basi JF ianzishe forum ya comedians ili members kama hawa wawe restricted huko tu! Sio kuleta ushauri wa kipuuzi katika mijadala ya maana kama ya huyu Mzee Mstaafu Makoye.
FACEBOOK GRADUATED
 
Ziweke kwanza Fixed Account bank ya TCB wanatoa hadi 12% annually. Hapo kila mwezi utakuwa unapata karibu laki 8 wakati ukifikiria biashara ya kufanya.
NB. KWA KUWA SASA UNA MDA WA KUTOSHA JARIBU BIASHARA YA KUNENEPESHA NGOMBE KISHA KUWAUZA BAADA YA MDA FULANI INALIPA SANA NA HAINA CHANGAMOTO NYINGI
ONYO 1. USIJARIBU KILIMO
ONYO 2. USIJARIBU BIASHARA YA MAGARI YA ABIRIA.
Kila la kheri.
Mkuu kama hutojali ninaomba elimu ya kunenepesha ng'ombe.
 
Ushauri: Tumia 500,000 kwa mwezi X 12= 6,000,000 kwa Mwaka, Nadhani now una umri 61+15=76
6,000,000 X 15= 90,000,000.
Hiyo pesa utatumia kwa maika 15 bila stress, Ikiisha iyo ndo unaanza kutumia ile iliyokua inaingia mwisho wa mwezi uliyo iacha kwa miaka 15,

Hapo maisha yako yatakua marefu mkuu, umri huo hauhitaji stress, Biashara tuachie sisi coz kilichonikuta mimi kwenye biashara, ingekua wew ungekua ushakufa kwa presha, its more than 10M nimepata loss, hapa najipang upya kuanza tena biashara.

Huo ushauri nikama ushajenga, unausafiri mzuri, nyumbani hakikisha unamifugo rahisi kama kuku, pia unashamba la mazao ya kudumu, na shamba moja la mazao ya chakula, hivyo vitu vitakufanya uwe na kazi kila uamkapo asubuh utapanga ratiba yako uanze na kipi.
NB:Kama hujawai fanya biashara Relax mzee wangu.

Huku Pwani vijijini wazee wanaishi miaka mingi kwa sababu hawaumizi vichwa kuwa na vitu vikubwa ambavyo tunaviona kwenye social media, kila jambo lina muda wake, acha tamaa.

Mwisho kabisa tafuta crue yako baada ya shughuli zako ukipumzika, hapa ni bora uwe na watu wa ibada, kama mkristo kundi hilo lipo kanisani shiriki ibada then rudi home, kama islamic nenda msikitini baada ya swala kula kashata na chai, then rudi home.
 
Ziweke kwanza Fixed Account bank ya TCB wanatoa hadi 12% annually. Hapo kila mwezi utakuwa unapata karibu laki 8 wakati ukifikiria biashara ya kufanya.
NB. KWA KUWA SASA UNA MDA WA KUTOSHA JARIBU BIASHARA YA KUNENEPESHA NGOMBE KISHA KUWAUZA BAADA YA MDA FULANI INALIPA SANA NA HAINA CHANGAMOTO NYINGI
ONYO 1. USIJARIBU KILIMO
ONYO 2. USIJARIBU BIASHARA YA MAGARI YA ABIRIA.
Kila la kheri.
Good advice I agree
 
Back
Top Bottom