Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
NO REFORMS, NO ELECTION!
 
Familia ya mstaafu ipewe kipaumbele tafadhali.Sikiliza familia yako wanasemaje kwanza juu ya uwekekezaji wa hiyo 80mls.Kama hawana mawazo basi tulia kwanza kwa muda ukifanya risk assessment ya biashara na uwekezaji huku ukitafuta wataalamu ambao wako willing kukusaidia bila malipo au kwa malipo kidogo.Epuka matapeli
 
Fuga ngombe , kuku na samaki sato na kambale, pia wekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji 🤔
EEEeeenHEEEEE,

Mkuu 'min-me'; usifanye mzaha bwana na maisha ya watu. Ulisha jaribu kuzifanya kazi hizo?
Kazi hizo kwa pesa ya kustaafu ni hatari mara kumi.
Ni bora kabisa kuwekeza kwenye hii mifuko yenye kuaminika inayotoa riba ya kutosha kila mwaka.
Ni kuchagua tu mifuko yenye uhakika wa pesa yako kubaki salama.

Hata hivyo, siyo mbaya kuwekeza kwenye baadhi ya shughuli hizo ulizo pendekeza; lakini isiwe ni kwa kiasi kikubwa. Unaweza kupanua kadri mafanikio na uzoefu wa kazi yenyewe unapozidi kuimudu.
 
tenga milion tano tu, anzisha kilimo cha mpunga au mahindi ila mahindi sikushauri sana ni gharama pia losi ipo karibu labda kama upo karibu na bonde utamwagilia.

pili hyo milion 25 iliyobaki kanunue mpunga vijijn uweke store mashine za mpunga ni bure kabxa, saiv junia sie tunanunua kwa laki moja. hapo utakuwa na junia 250.

mwez wa tatu au pili mwakan utaukoboa bei itakua imechangamka.
huenda kila junia ukawa na faida ya 50,000 na zaid endapo ukivuka 3000 kwa kilo.

50M kanunue bond au share na makampun yaliyo imara uwe unapata gawio.
Hii nimependa japo inahitaji mtu mzoefu anayefahamu biashara hii kiundani
 
Kwanza tukafanye kikao kitambaa cheupe tabata
Pale kuna mawazo mazuri sana
Halafu umuunganishe na tutoto twa afu mbili!Humtakii mema Mzee wangu
20241217_155806.jpg
 
Hiyo pesa sio nyingi ukiitumia vibaya tu inaisha. Hata kama utafanya biashara basi hakikisha mtaji hauzidi milioni 10.
 
Tumia mil 40, Kwa mchakato wote weka mashine yoyote kutokana na mazingira yako. Mashine ya mpunga,alizeti, mahindi n.k. afu simamia kwa umakini.
 
Mmmh milion 80 mbona kama bado hvi kwa biashara serious mkuu..

Naomba fanya hv tafuta tafuta upate hata milion 100 hv ndo uje tukupe ushauri

Evelyn Salt
☺️☺️☺️huyu kijana wetu kachanganya mafaili. huyu sio wa jukwaa hili. itakuwa alidhani yupo kule MMU. asamehewe tu.
 
Biashara ya kulea watoto inatosha ,anza kuwakaba wakutumie pesa kila mwisho wa mwezi ...Wakishindwa tafuta wakili uwapeleke Mahakamani.
 
Back
Top Bottom